Simba SC vs Dodoma Jiji Leo 24/05/2026 Saa Ngapi?

Simba SC vs Dodoma Jiji Leo 24/05/2026: Muda wa Mechi, Takwimu na Wachezaji wa Kuangalia

Simba SC vs Dodoma Jiji leo ni moja ya mechi zinazobeba uzito mkubwa kwenye mbio za Ligi Kuu Bara, huku Wekundu wa Msimbazi wakihitaji ushindi ili kuendelea kuweka presha kwenye kilele cha msimamo.

Mchezo huo utapigwa Jumapili, Mei 24, 2026 katika Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 12:15 jioni. Simba inaingia kwenye mchezo huu ikijua ushindi unaweza kuirejesha juu ya msimamo kwa kufikisha pointi 58, wakati Dodoma Jiji nayo ikitafuta matokeo ya kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi.

Taarifa Muhimu za Mechi

MechiSimba SC vs Dodoma Jiji
TareheJumapili, 24 Mei 2026
MudaSaa 12:15 jioni
UwanjaKMC Complex, Dar es Salaam
MashindanoLigi Kuu Bara
Hali ya MsimamoSimba inahitaji ushindi kurejea kileleni; Dodoma Jiji ipo nafasi ya nane ikiwa na pointi 33

Simba SC vs Dodoma Jiji Leo 24/05/2026 Saa Ngapi?

Simba Inahitaji Pointi Tatu Kuendeleza Presha

Simba inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na lengo la kuendelea kushinikiza mbio za ubingwa. Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, kama Wekundu hao watashinda mchezo huu, watafikisha pointi 58 na kurejea tena juu ya msimamo.

Hata hivyo, kama Simba itashindwa kushinda, itasalia nafasi ya pili, hali ambayo itakuwa ahueni kwa Yanga ambao wapo kileleni kwa pointi 57.

Kocha Steve Barker amekuwa akimuanzisha Elie Mpanzu kama mshambuliaji kinara, huku Seleman Mwalimu akiachwa nje. Hilo linaifanya safu ya ushambuliaji ya Simba kuwa moja ya maeneo yatakayofuatiliwa zaidi kwenye mchezo huu.

Dodoma Jiji Yataka Kuendelea Kujijenga Kwenye Msimamo

Dodoma Jiji inaingia kwenye mchezo huu ikiwa nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 33. Timu hiyo inajua kuwa angalau pointi moja inaweza kuwa muhimu kwenye mbio zake za kujiweka vizuri zaidi.

Kocha wa Dodoma Jiji, Amani Josiah, amesema timu yake imejiandaa vizuri na inatambua presha iliyopo kwa Simba.

“Tumejiandaa vizuri kwenda kukutana na Simba, tutaingia tukiwa kama timu ya pili lakini mchezo utakuwa wa presha kubwa kwa Simba, tunawaheshimu ni timu nzuri lakini watahitaji matokeo kutokana na malengo yao lakini na sisi tunataka matokeo kujiweka sehemu nzuri zaidi.”

Dodoma Jiji pia inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Yanga, matokeo ambayo yaliweka historia kwa timu hiyo dhidi ya mabingwa hao watetezi.

Rekodi ya Simba Dhidi ya Dodoma Jiji

Takwimu zinaipa Simba nafasi kubwa kuelekea mchezo huu. Katika mechi 11 ambazo timu hizi zimekutana, Simba imeshinda mara 10 na kutoka sare mara moja.

Katika rekodi hiyo, Simba imefunga jumla ya mabao 22, wakati Dodoma Jiji imefunga mabao mawili pekee.

Hata hivyo, Dodoma Jiji iliitibulia Simba kwenye mchezo wao wa awali msimu huu baada ya kuilazimisha sare ya bila kufungana Februari 25, 2026. Katika mchezo huo, Simba ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini haikuweza kupata bao.

Mechi Tano za Mwisho za Simba na Dodoma Jiji

Simba imekuwa kwenye mwenendo mzuri katika mechi zake tano za mwisho. Imeshinda mechi nne dhidi ya Coastal Union, Mashujaa, Prisons na JKT Tanzania, huku ikitoa sare moja dhidi ya Yanga.

Kwa upande wa Dodoma Jiji, timu hiyo imeshinda mechi mbili katika tano za mwisho dhidi ya Yanga na Mtibwa Sugar, huku ikitoa sare tatu.

Hii inaifanya mechi ya leo kuwa muhimu kwa pande zote mbili; Simba ikihitaji kuendeleza mbio za ubingwa, na Dodoma Jiji ikihitaji matokeo ya kuimarisha nafasi yake.

Wachezaji wa Kuangalia Simba SC vs Dodoma Jiji Leo

Clatous Chama

Clatous Chama anaingia kwenye mchezo huu akiwa kwenye kiwango bora. Kiungo huyo wa Simba amebeba tuzo tano mfululizo za mchezaji bora wa mechi.

Chama amefunga mabao manane na kutoa asisti sita, akihusika kwenye jumla ya mabao 14. Katika mchezo wa mwisho dhidi ya Coastal Union, alitengeneza mabao yote mawili kwenye ushindi wa Simba wa 2-1.

Kwa kiwango hicho, ni wazi kuwa Dodoma Jiji italazimika kumfuatilia kwa karibu.

Elie Mpanzu

Elie Mpanzu amekuwa chaguo la kuanza kwenye safu ya ushambuliaji ya Simba chini ya Kocha Steve Barker. Mechi hii inampa nafasi nyingine ya kuendelea kuiongoza safu ya mbele ya Wekundu wa Msimbazi.

Edgar William

Kwa Dodoma Jiji, Edgar William ndiye kinara wao wa mabao akiwa amefunga mabao saba. Msimu huu tayari ameifunga Yanga pale KMC Complex katika mchezo ambao Dodoma Jiji ilifungwa 3-1.

Uwepo wake mbele unaweza kuwa moja ya changamoto kubwa kwa safu ya ulinzi ya Simba.

Matola: “Haitakuwa Mechi Rahisi”

Kocha msaidizi wa Simba, Suleiman Matola, amekiri kuwa mchezo huo hautakuwa rahisi kutokana na namna Dodoma Jiji ilivyoonyesha ushindani kwenye mchezo uliopita baina ya timu hizo.

“Haitakuwa mechi rahisi, ukiangalia matokeo ya mechi iliyopita tulipokutana nao walitupa wakati mgumu pamoja na upinzani mkubwa lakini pamoja na ugumu na ubora wao, tumejipanga kuhakikisha tunapata pointi tatu katika mchezo wa kesho (leo).”

Kauli hiyo inaonyesha namna Simba inavyouchukulia mchezo huu kwa umakini, hasa baada ya kupoteza pointi mbili kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Dodoma Jiji msimu huu.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Yanga vs Singida BS Leo 22/05/2026
  2. Dewji Aweka Bilioni 1 Mezani Simba Ikibeba Mataji Mawili
  3. Kikosi Cha Ivory Coast Kombe La Dunia 2026
  4. Kikosi cha Brazil Kombe la Dunia 2026: Neymar Ndani, Joao Pedro Akosekana
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo