Ratiba ya ligi kuu ya nbc leo 24/05/2026
Michuano ya ligi kuu ya NBC 2025/2026 Inaendelea leo ambapo mashabiki watashuhudia mitanange mikali yenye maamuzi makubwa katika mbio za kumsaka bingwa wa ligi kuu ya NBC haswa pambano la mnyama Simba Dhidi ya Dodoma Jiji Ambalo linatarajiwa kutimua vumbi katika viunga vya uwanja wa Mej. Gen. Isamuhyo, DSM.
Mei 24 inakuwa siku ya pilikapilika nyingine kwenye Ligi Kuu ya NBC, huku michezo minne ikitarajiwa kupigwa kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa 2:30 usiku.
TRA United itaanza ratiba ya siku kwa mchezo dhidi ya Fountain Gate saa 10:00 jioni. Katika muda huo huo, Mtibwa Sugar itaingia uwanjani kuivaa JKT Tanzania.
Baadaye, Simba SC itakuwa kazini dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo uliopangwa kuanza saa 12:15 jioni. Huu ni miongoni mwa michezo inayosubiriwa zaidi na mashabiki wengi kutokana na ukubwa wa klabu ya Simba na mvuto wa mchezo wenyewe.
Coastal Union itafunga ratiba ya siku kwa kukutana na Mashujaa FC saa 2:30 usiku.

Ratiba Kamili ya Mechi za NBC Leo Mei 24
- TRA United vs Fountain Gate – Saa 10:00 jioni
- Mtibwa Sugar vs JKT Tanzania – Saa 10:00 jioni
- Simba SC vs Dodoma Jiji – Saa 12:15 jioni
- Coastal Union vs Mashujaa FC – Saa 2:30 usiku
Mapendekezo ya Mhariri:







Leave a Reply