Ratiba ya Michuano ya CAF 2026/2027 Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho

Ratiba ya Michuano ya CAF 2026/2027 Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza rasmi Ratiba ya Michuano ya CAF 2026/2027 kwa Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika. Msimu huo utaanza Septemba 4 hadi 6, 2026 kwa mechi za mkondo wa kwanza za hatua ya kwanza ya mchujo.

Ratiba hiyo inaweka wazi vipindi vya mechi kuanzia hatua za mchujo, makundi na mtoano hadi fainali. Tanzania imetajwa kuwa na Yanga na Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati Azam na Singida Black Stars zikiwa katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Msimu uliopita, klabu zote nne za Tanzania zilivuka hadi hatua ya makundi ya mashindano hayo, lakini hazikufuzu kwa hatua ya robo fainali.

Ratiba ya Michuano ya CAF 2026/2027 Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho

Ratiba ya hatua za mchujo CAF 2026/2027

Msimu wa 2026/27 utafunguliwa kwa hatua ya kwanza ya mchujo Septemba 2026. Baada ya hapo, hatua ya pili ya mchujo itachezwa Oktoba kabla ya kuanza kwa hatua ya makundi mwishoni mwa Novemba.

HatuaTarehe
Hatua ya kwanza – Mkondo wa kwanzaSeptemba 4–6, 2026
Hatua ya kwanza – MarudianoSeptemba 11–13, 2026
Hatua ya pili – Mkondo wa kwanzaOktoba 16–18, 2026
Hatua ya pili – MarudianoOktoba 23–25, 2026

Mechi za marudiano za hatua ya pili zitakamilika Oktoba 25, 2026. Baada ya hatua za mchujo kumalizika, mashindano yote mawili yataingia hatua ya makundi.

Ratiba ya hatua ya makundi

Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika itaanza mwishoni mwa Novemba 2026.

CAF imepanga mizunguko sita ya hatua hiyo kati ya Novemba 2026 na Januari 2027.

MzungukoTarehe
Mzunguko wa kwanzaNovemba 27–29, 2026
Mzunguko wa piliDesemba 4–6, 2026
Mzunguko wa tatuDesemba 18–20, 2026
Mzunguko wa nneJanuari 8–10, 2027
Mzunguko wa tanoJanuari 15–17, 2027
Mzunguko wa sitaJanuari 22–24, 2027

Mzunguko wa sita, unaopangwa kuchezwa Januari 22 hadi 24, 2027, ndio wa mwisho katika ratiba ya hatua ya makundi.

Ratiba ya robo fainali CAF 2026/2027

Baada ya hatua ya makundi, ratiba ya CAF inaonyesha kuwa robo fainali zitaanza mwishoni mwa Februari 2027.

HatuaTarehe
Robo fainali – Mkondo wa kwanzaFebruari 26–28, 2027
Robo fainali – MarudianoMachi 5–7, 2027

Mkondo wa kwanza wa robo fainali utachezwa Februari 26 hadi 28, huku mechi za marudiano zikipangwa Machi 5 hadi 7, 2027.

Ratiba ya nusu fainali

Nusu fainali zimepangwa kuchezwa Aprili 2027 kwa mikondo miwili.

HatuaTarehe
Nusu fainali – Mkondo wa kwanzaAprili 9–11, 2027
Nusu fainali – MarudianoAprili 16–18, 2027

Mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa Aprili 9 hadi 11, kabla ya marudiano ya Aprili 16 hadi 18, 2027.

Fainali za CAF 2026/2027 zitachezwa lini?

Fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika zimepangwa kuchezwa katika kipindi cha Mei 9 hadi Mei 31, 2027.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Kombe la Dunia Leo 01/07/2026
  2. Timu Zilizofuzu 16 Bora Kombe la Dunia 2026
  3. Timu za Afrika Zilizofuzu Hatua ya 32 Bora Kombe la Dunia 2026
  4. Ratiba ya Hatua ya 32 Bora Kombe la Dunia 2026
  5. Ratiba ya Mechi za Hatua ya 32 Bora Kombe la Dunia 2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo