Orodha ya Waliochaguliwa Kujiunga JKT 2026/2027

Orodha ya Waliochaguliwa Kujiunga JKT 2026/2027

Jeshi la Kujenga Taifa limetoa wito kwa vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita mwaka 2026 kutoka shule zote za Tanzania Bara na Visiwani kuhudhuria Mafunzo ya JKT Kundi la Lazima, maarufu kama Mujibu wa Sheria.

Kwa mujibu wa taarifa ya JKT iliyotolewa tarehe 28 Mei 2026, vijana hao wamepangiwa makambi mbalimbali nchini na wanatakiwa kuripoti kuanzia tarehe 01 Juni hadi 07 Juni 2026. Orodha kamili ya Waliochaguliwa Kujiunga JKT 2026, makambi waliyopangiwa na maeneo ya makambi hayo inapatikana kupitia tovuti ya JKT.

Taarifa Muhimu Kuhusu Kujiunga JKT 2026/2027

Tarehe ya taarifa28 Mei, 2026
WalioitwaWahitimu wa kidato cha sita mwaka 2026 kutoka Tanzania Bara na Visiwani
Aina ya mafunzoJKT Kundi la Lazima, Mujibu wa Sheria
Tarehe za kuripoti01 Juni hadi 07 Juni 2026
Mahali pa kuangalia majinaTovuti ya JKT: www.jkt.mil.tz
Maelekezo kwa wenye ulemavu wa kuonekana kwa machoWaripoti Kambi ya Ruvu JKT, Mlandizi, Pwani

Tarehe za Kuripoti Makambini kwa Vijana Waliochaguliwa Kujiunga JKT 2026/2027

Vijana waliochaguliwa kushiriki Mafunzo ya JKT Mujibu wa Sheria 2026 wanatakiwa kuripoti katika makambi yao kuanzia tarehe 01 Juni hadi tarehe 07 Juni 2026.

Hii ndiyo ratiba ya kuripoti iliyotajwa kwenye taarifa ya JKT kwa kundi la lazima la mwaka 2026. Kila kijana anatakiwa kuhakikisha ameangalia kambi aliyopangiwa kabla ya safari ili kufika katika eneo sahihi ndani ya muda uliowekwa.

Waliochaguliwa Kujiunga JKT 2026 Mujibu wa Sheria

Makambi ya JKT 2026 Waliyopangiwa Wahitimu

JKT imesema vijana wamepangwa katika makambi mbalimbali nchini kwa ajili ya mafunzo hayo. Makambi yaliyotajwa ni:

  1. Rwamkoma JKT – Mara
  2. Msange JKT – Tabora
  3. Ruvu JKT – Pwani
  4. Kibiti JKT – Pwani
  5. Mpwapwa JKT – Dodoma
  6. Makutupora JKT – Dodoma
  7. Mafinga JKT – Iringa
  8. Mlale JKT – Ruvuma
  9. Mgambo JKT – Tanga
  10. Maramba JKT – Tanga
  11. Makuyuni JKT – Arusha
  12. Oljoro JKT – Arusha
  13. Bulombora JKT – Kigoma
  14. Kanembwa JKT – Kigoma
  15. Mtabila JKT – Kigoma
  16. Itaka JKT – Songwe
  17. Luwa JKT – Rukwa
  18. Milundikwa JKT – Rukwa
  19. Nachingwea JKT – Lindi
  20. Chuo cha Uongozi JKT, CUJKT Kimbiji – Dar es Salaam

Jinsi ya Kuangalia Orodha ya Waliochaguliwa Kujiunga JKT 2026/2027

Orodha kamili ya majina ya vijana waliochaguliwa, makambi ya JKT waliyopangiwa, maeneo ya makambi hayo na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo inapatikana kupitia tovuti ya JKT ambayo ni:

www.jkt.mil.tz

Ili kufahamu kambi aliyopangiwa, kijana anatakiwa kuingiza jina la shule au namba ya shule aliyohitimu elimu ya kidato cha sita.

Baada ya hapo, mbele ya jina la shule yake ataona neno “waliochaguliwa”. Akichagua neno hilo, ataweza kuona majina ya waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria mwaka 2026, kambi aliyopangiwa, wilaya na mkoa ilipo kambi hiyo.

JKT pia imeeleza kuwa ili kuona majina yote ya vijana na kambi walizopangiwa, mtumiaji anaweza kupakua JKT PDF 2026 iliyopo juu kulia katika ukurasa huo.

Vifaa vya Kwenda Navyo JKT 2026

Vijana waliopangiwa kuripoti katika makambi ya JKT 2026 wanatakiwa kwenda na vifaa vilivyotajwa kwenye taarifa ya JKT. Vifaa hivyo ni:

  • Bukta ya rangi ya Dark Blue yenye mpira kiunoni, mfuko mmoja nyuma, inayoshia magotini na isiyo na zipu.
  • T-shirt ya rangi ya kijani.
  • Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.
  • Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
  • Soksi ndefu za rangi nyeusi.
  • Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
  • Track suit ya rangi ya kijani au blue.
  • Nyaraka zote zinazohitajika katika udahili wa kujiunga na elimu ya juu.
  • Vyeti vya kuzaliwa.
  • Vyeti vya kuhitimu kidato cha nne.
  • Nauli ya kwenda kuripoti makambini na kurudi nyumbani.

Maelekezo kwa Vijana Wenye Ulemavu wa Kuonekana kwa Macho

JKT imetoa maelekezo maalum kwa wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho, yaani physical disabilities.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, vijana hao wanatakiwa kuripoti katika Kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi, Mkoa wa Pwani. JKT imesema kambi hiyo ina miundombinu ya kuwahudumia watu hao.

Lengo la Mafunzo ya JKT Mujibu wa Sheria 2026

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, amewakaribisha vijana wote waliohitimu kidato cha sita mwaka 2026 kujiunga na vijana wenzao katika mafunzo hayo.

Kwa mujibu wa taarifa ya JKT, mafunzo hayo yanalenga kuwajengea vijana uzalendo, nidhamu, ukakamavu, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. TAMISEMI Form Five Selection 2026/2027: Tarehe, Vigezo na Jinsi ya Kuangalia Majina
  2. Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Tano 2026
  3. Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Tano 2026/2027
  4. Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2026/2027
  5. Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2026/2027 Morogoro
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo