Matokeo ya Yanga vs JKT Tanzania Leo 30/06/2026

Matokeo ya Yanga vs JKT Tanzania Leo 30/06/2026

Yanga SC leo Jumanne, Juni 30, 2026, ipo dimbani dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2025/2026, ukiwa ni mchezo wenye uzito mkubwa katika mbio za ubingwa.

Mchezo huu utapigwa saa 10:00 jioni katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam, huku macho ya mashabiki wengi yakiwa kwenye dakika 90 zitakazoamua hatima ya taji la msimu huu.

Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa kileleni mwa msimamo baada ya michezo 29, ikiwa na pointi 72. Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 70 kabla ya kucheza dhidi ya KMC FC katika Uwanja wa KMC Complex muda huohuo. Hiyo ina maana kuwa matokeo ya Yanga dhidi ya JKT Tanzania ndiyo yatakayobeba uzito mkubwa zaidi katika safari ya ubingwa.

Matokeo ya Yanga vs JKT Tanzania Leo

Yanga ScVSJKT Tanzania

Taarifa za Mchezo

  • Yanga SC vs JKT Tanzania
  • Muda: Saa 10:00 jioni
  • Tarehe: Jumanne, Juni 30, 2026
  • Uwanja: Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam
  • Mashindano: Ligi Kuu Bara 2025/2026

Matokeo ya Yanga vs JKT Tanzania Leo 30/06/2026

 

Yanga inahitaji ushindi ili kujihakikishia ubingwa bila kutegemea matokeo ya Simba dhidi ya KMC. Sare pia inaweza kuwa na nafasi ya kuibeba Yanga, lakini hesabu hizo zitategemea matokeo ya mchezo wa Simba ambao unapigwa kwa wakati mmoja.

Kikosi cha Yanga vs JKT Tanzania Leo

Yanga imeanza na kikosi chenye mchanganyiko wa uzoefu, nguvu na ubunifu, huku Aziz Ki Abouya akiwa nahodha wa timu katika mchezo huu muhimu.

Kikosi cha kuanza cha Yanga:

  • Diarra
  • Yao
  • Hussein
  • Assinki
  • Bacca
  • Abuya ©
  • Maxi
  • Dube
  • Depu
  • Okello
  • Pacome

Wachezaji wa akiba: Mshery, Kibwana, Boka, Abubakar Aziz, Damaro, SureBoy, Abdulnassir, Mudathir, Edmund.

Uwepo wa Diarra langoni, Yao na Hussein kwenye eneo la ulinzi, pamoja na Pacome, Okello, Depu na Dube katika maeneo ya mbele, unaonyesha namna Yanga ilivyoingia kwenye mchezo huu ikiwa na nia ya kushambulia na kutafuta matokeo mapema.

Dakika 90 za Kuamua Bingwa

Msimu wa 2025/2026 umefika mwisho baada ya miezi tisa ya ushindani mkubwa. Raundi hii ya mwisho inapigwa kwa mfumo wa mechi zote nane kuanza kwa wakati mmoja, jambo linaloongeza presha kwa timu zinazowania ubingwa, zile zinazopambana kubaki ligi kuu na zile zinazotafuta nafasi bora kwenye msimamo.

Kwa Yanga, hesabu ni nyepesi lakini zenye presha kubwa: kushinda dhidi ya JKT Tanzania na kutangaza ubingwa wa tano mfululizo. Kwa Simba, mchezo dhidi ya KMC ni wa lazima kushinda, kisha kusubiri taarifa kutoka Mbweni.

Hii ndiyo sababu mashabiki wa soka nchini watakuwa wakifuatilia matukio ya viwanja viwili kwa wakati mmoja: Mbweni ambako Yanga inacheza na JKT Tanzania, na KMC Complex ambako Simba inacheza dhidi ya KMC.

JKT Tanzania Yaingia Bila Presha Kubwa

JKT Tanzania inaingia kwenye mchezo huu ikiwa haina presha ya ubingwa, lakini hiyo haimaanishi kuwa itakuwa mpinzani mwepesi. Timu hiyo imeonyesha ushindani mkubwa msimu huu na inaweza kuwa kikwazo kwa Yanga ikiwa itacheza kwa nidhamu na umakini.

Kocha wa JKT Tanzania, Ahmad Ally, alisema maandalizi ya timu yake yamekuwa mazuri licha ya safari ndefu kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam. Alisisitiza kuwa JKT Tanzania haitacheza kwa kuangalia mahitaji ya wapinzani, bali malengo yake kama timu.

“Mchezo utakuwa mgumu kwa sababu kila timu ina malengo yake,” alisema Ally.

Kauli hiyo inaonyesha kuwa JKT Tanzania imepanga kumaliza msimu kwa heshima, licha ya kucheza dhidi ya timu inayowania ubingwa.

Yanga Yataka Kumaliza Kazi Mbweni

Kwa upande wa Yanga, Kaimu Kocha Mkuu Abdihamid Moallin alisema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo huu muhimu. Alieleza kuwa wanaiheshimu JKT Tanzania kutokana na ubora wake, lakini lengo kubwa la Yanga ni kushinda na kusherehekea ubingwa.

“Lengo letu ni kushinda mchezo na kusherehekea ubingwa baada ya hapo,” alisema Moallin.

Mshambuliaji Emmanuel Mwanengo naye alieleza kuwa wachezaji wanafahamu uzito wa mchezo huo na wanahitaji hata ushindi mwembamba ili kutimiza lengo lao.

“Hata ushindi wa bao moja unatosha kutupa ubingwa,” alisema Mwanengo.

NBC Yaandaa Sherehe Mbili za Ubingwa

Wadhamini wakuu wa Ligi Kuu Bara, Benki ya NBC, wameandaa mazingira ya kuhakikisha bingwa anakabidhiwa kombe siku hiyo hiyo. Kwa kuwa Yanga na Simba zote bado zina nafasi ya kutwaa ubingwa, maandalizi yamefanyika kwenye pande mbili.

NBC imesema kutakuwa na sherehe mbili zenye viwango sawa, huku helikopta ikitarajiwa kutumika kusafirisha kombe kwenda kwenye uwanja ambao bingwa atapatikana.

Hatua hiyo imeongeza hamasa ya mchezo wa mwisho, kwani mashabiki wa Dar es Salaam watakuwa wakisubiri kuona kombe litaelekea Mbweni au KMC Complex baada ya dakika 90 kumalizika.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Yanga vs JKT Tanzania Leo 30/06/2026
  2. JKT Tanzania vs Yanga Leo 30/06/2026 Saa Ngapi?
  3. Ratiba ya Ligi Kuu NBC Leo Juni 30, 2026: Yanga, Simba Kuamua Ubingwa Raundi ya Mwisho
  4. Simba Yatoa Tamko Kuhusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Kuchezwa Pemba
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo