Matokeo ya Yanga vs Azam Leo 24/06/2026 Ligi Kuu
Yanga SC na Azam FC zinakutana leo, Jumatano Juni 24, 2026, katika mchezo wa Raundi ya 28 ya NBC Premier League msimu wa 2025/2026 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Hapa utapata Matokeo Yanga vs Azam, vikosi vya kuanzia, wachezaji wa akiba, taarifa za kabla ya mechi na updates kadri mchezo utakavyoendelea. Mechi hii inaanza saa 10:00 jioni na ni sehemu ya michezo minane ya Ligi Kuu inayopigwa leo.
Yanga inaingia uwanjani ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 66, huku Simba ikiwa nafasi ya pili na pointi 64. Azam FC ipo na pointi 58 na inaendelea kupambania nafasi nzuri zaidi kabla ya mwisho wa msimu.

Matokeo Yanga vs Azam Live Updates
Taarifa Muhimu za Mchezo
| Mechi | Yanga SC vs Azam FC |
| Mashindano | NBC Premier League 2025/2026 |
| Raundi | Raundi ya 28 |
| Tarehe | 24/06/2026 |
| Muda | Saa 10:00 jioni |
| Uwanja | Amaan, Zanzibar |
| Matangazo | AzamTV |
| Muktadha | Mbio za ubingwa na nafasi za juu za ligi |
Kikosi cha Yanga vs Azam Leo
Hiki apa Kikosi cha Yanga SC kilichotangazwa
- 39 Diarra
- 21 Yao
- 15 Hussein
- 3 Mwamnyeto
- 4 Bacca
- 38 Abuya
- 7 Maxi
- 29 Dube
- 40 Depu
- 20 Okello
- 10 Pacome
Benchi la Yanga: Mshery, Kibwana, Boka, Assink, Nabil, Damaro, Shekhain, Mudathir, Asanal, Edmund.
Kikosi cha Azam FC
- 32 Foba
- 5 Lusajo
- 12 Msindo
- 14 Lawi
- 25 Twalib
- 23 Himid
- 7 Zidane
- 8 Ranoute
- 19 Ngita J.J
- 6 Fei Toto
- 11 Nado
Benchi la Azam: Manula, Chilambo, Zouzou, Fuentes, Ihramu, Bin Zayd, Akaminko, Sangu, Sopu, Kitambala.
Yanga Inahitaji Majibu Baada ya Kipigo cha Kirumba
Mechi hii inakuja takribani saa 70 na dakika 30 baada ya Yanga na Azam kukutana katika Kombe la CRDB, ambako Azam ilishinda mabao 3-2 baada ya dakika 120.
Safari hii, hesabu ni tofauti. Badala ya tiketi ya fainali, kuna pointi tatu muhimu za Ligi Kuu ambazo zinaweza kuathiri moja kwa moja mbio za ubingwa.
Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Abdihamid Moallin, anaingia kwenye mchezo huu akijua kuwa timu yake inahitaji kurejea haraka kwenye ushindani wa ligi. Yanga ipo kileleni, lakini tofauti ya pointi mbili dhidi ya Simba inaifanya mechi hii kuwa na uzito mkubwa.
Mipira ya Juu Ni Eneo la Kwanza kwa Yanga Kufanyia Kazi
Katika mchezo uliopita, Azam iliiumiza Yanga kupitia mipira ya juu. Mabao yote matatu yalitokana na mtindo huo, jambo linalolazimisha benchi la ufundi la Yanga kufanya marekebisho kabla ya mchezo wa leo.
Jean Ngita alionekana kuwa sehemu muhimu ya mpango wa Azam. Ingawa hakufunga, alitumia nguvu zake kwenye mipira ya juu na kuchangia kwenye bao la kwanza baada ya kumtengenezea Himid Mao nafasi ya kufunga kwa kichwa.
Yanga italazimika kuhakikisha mabeki wake wa kati wanapata msaada wa karibu kutoka kwa kiungo wa ulinzi, hasa pale Azam itakapotumia mipira mirefu kuelekea kwa washambuliaji warefu kama Ngita au Kitambala.
Depu na Dube Wanaweza Kuongeza Presha kwa Azam
Moja ya maeneo ambayo Yanga inaweza kuyatumia ni kuongeza idadi ya wachezaji kwenye eneo la ushambuliaji. Katika mchezo uliopita, baada ya Depu kuingia na kucheza karibu na Prince Dube, ulinzi wa Azam ulianza kupata changamoto zaidi.
Twalib Mohamed na Yoro Diaby walikuwa na uhuru zaidi walipokuwa wakikabiliana na mshambuliaji mmoja. Lakini Yanga ilipoongeza mtu mwingine ndani ya eneo la mbele, mabeki wa Azam walilazimika kugawana majukumu.
Hilo linaweza kuwa somo muhimu kwa Moallin katika mchezo wa leo, hasa kama Yanga itahitaji kuanza kwa kasi na kuzuia Azam kujenga utulivu mapema.
Okello Anatakiwa Kupewa Nafasi Zaidi
Allan Okello ni mmoja wa wachezaji wanaoweza kubadilisha mwelekeo wa mchezo. Taarifa za kabla ya mechi zinaonyesha kuwa ana mabao 11 na asisti saba, takwimu zinazomfanya kuwa moja ya silaha muhimu ndani ya kikosi cha Yanga.
Azam ilifanikiwa kumpunguza kwa kumweka chini ya presha ya Himid Mao na Yahya Zayd. Kwa Yanga kupata udhibiti mzuri wa mchezo, Okello anatakiwa kupewa nafasi zaidi kati ya safu za Azam.
Akifanikiwa kupata uhuru huo, anaweza kuwatengenezea nafasi Prince Dube, Depu, Pacome na Max Nzengeli.
Azam Inahitaji Nidhamu Zaidi
Kwa upande wa Azam, ushindi wa Kirumba uliipa timu kujiamini, lakini pia uliweka wazi jambo la kufanyia kazi: nidhamu.
Kadi nyekundu ya Yoro Diaby karibu ibadilishe kabisa mchezo. Hadi dakika ya 69, Azam ilikuwa kwenye nafasi nzuri ya kuumaliza mchezo, lakini ilipobaki na wachezaji 10, ililazimika kutumia nguvu nyingi kulinda matokeo.
Katika mchezo wa ligi, makosa kama hayo yanaweza kuwa gharama kubwa zaidi. Florent Ibenge atahitaji kuona mabeki wake wakicheza kwa utulivu, hasa wanapokutana na washambuliaji wenye kasi kama Prince Dube.
Mapendekezo yaMhariri:
- Ratiba ya Mechi za Leo 24/06/2027 Ligi Kuu ya NBC
- Matokeo ya Azam vs Yanga Leo 21/06/2026 Nusu Fainali Kombe la Shirikisho
- Kikosi cha Yanga vs Azam Leo 21 Juni 2026: Nusu Fainali ya Kombe la CRDB Kirumba
- Kikosi cha Azam FC Dhidi ya Yanga Leo 21/06/2026 Kombe la CRDB
- Msimamo Wa Ligi Kuu NBC Tanzania 2025/2026 Leo June 18
- Japan Waifundisha Dunia Somo la Usafi Kombe la Dunia




```







Leave a Reply