Ratiba ya Klabu Bingwa Afrika 2026/2027 CAF Hatua ya Awali
Ratiba ya Klabu Bingwa Afrika 2026/2027 CAF Hatua ya Awali imetangazwa rasmi baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kufanya droo ya raundi za awali za Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu wa 2026/2027. Mashindano ya mwaka huu yanashirikisha jumla ya vilabu 61 vinavyowania ubingwa wa Afrika.
CAF imeweka mfumo maalum wa droo kwa kuzingatia viwango vya vilabu, ukaribu wa kijiografia na historia ya ushiriki katika mashindano ya kimataifa ili kupunguza gharama za safari na kuongeza ushindani.

Mfumo wa Droo ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2026/2027
Kwa mujibu wa CAF, jumla ya vilabu 61 vinashiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2026/2027.
Vilabu vitatu vilivyoongoza kwenye viwango vya CAF vimepewa nafasi ya kuanzia moja kwa moja katika raundi ya pili ya mchujo.
Vilabu hivyo ni:
- Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)
- Esperance Sportive (Tunisia)
- Renaissance Berkane (Morocco)
Vilabu hivi vitaanza moja kwa moja hatua ya pili ya mchujo (Round of 32) na vitacheza mechi ya marudiano nyumbani.
Ratiba ya Hatua ya Awali ya Klabu Bingwa Afrika 2026/2027
Raundi ya kwanza ya mchujo itahusisha mechi 29 za nyumbani na ugenini.
Ratiba kamili ya hatua ya awali ni kama ifuatavyo:
- Wiliete (Angola) vs Foresters FC (Seychelles)
- Scotland FC (Zimbabwe) vs Nsingizini Hotspurs (Eswatini)
- Uniao do Songo (Msumbiji) vs Atletico Petroleos (Angola)
- Mangasport (Gabon) vs African Stars (Namibia)
- La Cure Waves (Mauritius) vs Orlando Pirates (Afrika Kusini)
- 15 de Agosto (Angola) vs Fomboni FC (Comoros)
- Mighty Wanderers (Malawi) vs Simba SC (Tanzania)
- CFFA (Madagascar) vs Lioli (Lesotho)
- Gaborone United (Botswana) vs Young Africans (Tanzania)
- Al-Sweihli (Libya) vs KVZ (Zanzibar)
- Aigle du Congo (Congo) vs APR (Rwanda)
- AS Port (Djibouti) vs Zamalek (Misri)
- Al-Merrikh Bentiu (Sudan Kusini) vs Hegan (Somalia)
- Gor Mahia (Kenya) vs Pyramids (Misri)
- Ailgons FC (Comoros) vs Sidama Bunna (Ethiopia)
- Aigle Noir (Burundi) vs Al-Hilal (Sudan)
- Star Sport (Gambia) vs Medina United (Gambia)
- Maghreb Fez (Morocco) vs Rahimo (Burkina Faso)
- ASKO Kara (Togo) vs ASEC Mimosas (Ivory Coast)
- FC Canchungo (Guinea-Bissau) vs Teungueth (Senegal)
- Colombe Sportive (Cameroon) vs Stade Malien (Mali)
- Rangers International (Nigeria) vs AS Sobamap (Benin)
- ASN Nigelec (Niger) vs MC Alger (Algeria)
- San Pedro (Ivory Coast) vs Rivers United (Nigeria)
- Vipers (Uganda) vs Nouadhibou (Mauritania)
- JS Saoura (Algeria) vs Horoya (Guinea)
- Al-Merrikh (Sudan) vs Power Dynamos (Zambia)
- Medeama (Ghana) vs Mazembe (DR Congo)
- Club Africain (Tunisia) vs Djoliba (Mali)
Ratiba ya Raundi ya Pili ya Mchujo
Washindi wa raundi ya kwanza watakutana katika hatua ya pili, huku baadhi yao wakicheza dhidi ya vilabu vilivyopewa nafasi ya kuanzia moja kwa moja.
Ratiba ya raundi ya pili ni:
- Mshindi wa Wiliete vs Foresters FC atacheza dhidi ya Mamelodi Sundowns
- Mshindi wa Scotland FC vs Nsingizini Hotspurs atacheza dhidi ya mshindi wa Uniao do Songo vs Atletico Petroleos
- Mshindi wa Mangasport vs African Stars atacheza dhidi ya mshindi wa La Cure Waves vs Orlando Pirates
- Mshindi wa 15 de Agosto vs Fomboni FC atacheza dhidi ya mshindi wa Mighty Wanderers vs Simba SC
- Mshindi wa CFFA vs Lioli atacheza dhidi ya mshindi wa Gaborone United vs Young Africans
- Mshindi wa Al-Sweihli vs KVZ atacheza dhidi ya Esperance Sportive
- Mshindi wa Aigle du Congo vs APR atacheza dhidi ya mshindi wa AS Port vs Zamalek
- Mshindi wa Al-Merrikh Bentiu vs Hegan atacheza dhidi ya mshindi wa Gor Mahia vs Pyramids
- Mshindi wa Ailgons FC vs Sidama Bunna atacheza dhidi ya mshindi wa Aigle Noir vs Al-Hilal
- Mshindi wa Star Sport vs Medina United atacheza dhidi ya Renaissance Berkane
- Mshindi wa Maghreb Fez vs Rahimo atacheza dhidi ya mshindi wa ASKO Kara vs ASEC Mimosas
- Mshindi wa FC Canchungo vs Teungueth atacheza dhidi ya mshindi wa Colombe Sportive vs Stade Malien
- Mshindi wa Rangers International vs AS Sobamap atacheza dhidi ya mshindi wa ASN Nigelec vs MC Alger
- Mshindi wa San Pedro vs Rivers United atacheza dhidi ya mshindi wa Vipers vs Nouadhibou
- Mshindi wa JS Saoura vs Horoya atacheza dhidi ya mshindi wa Al-Merrikh vs Power Dynamos
- Mshindi wa Medeama vs Mazembe atacheza dhidi ya mshindi wa Club Africain vs Djoliba
Simba SC na Young Africans Waanza Safari ya Afrika
Wawakilishi wa Tanzania, Simba SC na Young Africans (Yanga), wataanza kampeni zao katika hatua ya kwanza ya mchujo.
- Simba SC itacheza dhidi ya Mighty Wanderers ya Malawi.
- Young Africans itamenyana na Gaborone United ya Botswana.
Iwapo Simba itafuzu, itakutana na mshindi wa mechi kati ya 15 de Agosto ya Angola na Fomboni FC ya Comoros.
Kwa upande wa Young Africans, ikipepeta hatua ya kwanza itakutana na mshindi wa pambano kati ya CFFA ya Madagascar na Lioli ya Lesotho.
Mfumo wa Droo Ulivyopangwa
CAF iligawa vilabu katika makundi mbalimbali kulingana na viwango vyao na matokeo yao katika mashindano ya Afrika.
Baadhi ya vilabu vilivyokuwa kwenye kundi la timu zilizopewa ubora wa juu ni:
- Zamalek (Misri)
- Pyramids (Misri)
- Petro Atletico (Angola)
- Orlando Pirates (Afrika Kusini)
- Simba SC (Tanzania)
- Young Africans (Tanzania)
- Al-Hilal (Sudan)
- ASEC Mimosas (Ivory Coast)
- Stade Malien (Mali)
- MC Alger (Algeria)
CAF pia ilipanga droo kwa kuzingatia ukaribu wa kijiografia ili kupunguza safari ndefu kwa vilabu vinavyoshiriki.
Aidha, timu mbili kutoka nchi moja hazikuruhusiwa kukutana katika hatua hizi za awali za mashindano.
Ratiba ya Mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika 2026/2027
Raundi ya Kwanza ya Mchujo
- Mechi za kwanza: 4–6 Septemba 2026
- Marudiano: 11–13 Septemba 2026
Raundi ya Pili ya Mchujo
- Mechi za kwanza: 16–18 Oktoba 2026
- Marudiano: 23–25 Oktoba 2026
Hatua ya Makundi
- Mzunguko wa 1: 27–29 Novemba 2026
- Mzunguko wa 2: 4–6 Desemba 2026
- Mzunguko wa 3: 18–20 Desemba 2026
- Mzunguko wa 4: 8–10 Januari 2027
- Mzunguko wa 5: 15–17 Januari 2027
- Mzunguko wa 6: 22–24 Januari 2027
Robo Fainali
- Mechi za kwanza: 26–28 Februari 2027
- Marudiano: 5–7 Machi 2027
Nusu Fainali
- Mechi za kwanza: 9–11 Aprili 2027
- Marudiano: 16–18 Aprili 2027
Fainali
Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2026/2027 itachezwa katika kipindi cha 9 Mei hadi 31 Mei 2027. CAF bado haijatangaza tarehe rasmi za mechi za fainali.
Hitimisho
Ratiba ya Klabu Bingwa Afrika 2026/2027 imeweka wazi njia ya vilabu 61 kuelekea kwenye ubingwa wa Afrika. Wakati vigogo kama Mamelodi Sundowns, Esperance Sportive na Renaissance Berkane wakianza moja kwa moja raundi ya pili, vilabu vingine vitaanza safari yao kupitia hatua ya kwanza ya mchujo. Kwa Tanzania, macho yote yataelekezwa kwa Simba SC na Young Africans watakaoanza kampeni zao mwezi Septemba 2026 wakisaka nafasi ya kufuzu hatua inayofuata ya mashindano.
Mpaendekezo ya Mhariri:




```







Leave a Reply