Kikosi cha Yanga vs Gaborone United Leo Septemba 12, 2026

Kikosi cha Yanga vs Gaborone United Leo Septemba 12, 2026

Yanga leo Jumamosi, Septemba 12, 2026 itaikaribisha Gaborone United ya Botswana katika mchezo wa marudiano wa raundi ya kwanza ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Mchezo wa Yanga vs Gaborone United utaanza saa 1:00 usiku (19:00), huku macho ya mashabiki yakielekezwa pia kwenye kikosi ambacho kocha Manqoba Mngqithi atakitumia katika pambano hilo muhimu.

Kikosi rasmi cha kwanza cha Yanga kinatarajiwa kutangazwa muda mchache kabla ya mchezo kuanza majira ya saa 1:00 usiku. Hata hivyo, timu ya wananchi Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na wachezaji kadhaa ambao tayari wamekuwa sehemu muhimu ya hesabu dhidi ya Gaborone United.

Kikosi cha Yanga vs Gaborone United Leo Septemba 12, 2026

Kikosi cha Yanga vs Gaborone United leo

Kocha Manqoba Mngqithi ana kibarua kigumu cha kuchagua kikosi kitakachoweza kuipa Yanga matokeo ya kuivusha kwenda hatua inayofuata baada ya mchezo wao wa kwanza kuisha kwa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa Botswana Septemba 5, 2026.

Katika mchezo huo, Yanga ililazimika kusubiri hadi dakika za mwisho kupata bao la kusawazisha kupitia mshambuliaji Selemani Mwalimu, aliyemalizia pasi ya Mudathir Yahya.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuingia kwenye mchezo wa leo ikiwa inahitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kuendelea mbele bila kutegemea hesabu nyingine.

Taarifa za Yanga vs Gaborone United leo

  • Mchezo: Yanga vs Gaborone United
  • Mashindano: Ligi ya Mabingwa Afrika
  • Tarehe: Jumamosi, Septemba 12, 2026
  • Muda: Saa 1:00 usiku (19:00)
  • Uwanja: Azam Complex, Chamazi
  • Matokeo ya first leg: Gaborone United 1-1 Yanga

Selemani Mwalimu kwenye hesabu za mchezo

Moja ya majina yanayovutia zaidi kuelekea mchezo wa leo ni Selemani Mwalimu.

Mshambuliaji huyo mpya ndiye aliyefunga bao la kusawazisha katika mchezo wa kwanza Botswana, bao ambalo limeifanya Yanga kurejea Dar es Salaam ikiwa na matokeo ya 1-1.

Yanga pia imeamua kuutumia mchezo wa leo kama siku maalumu ya kumpokea rasmi Selemani mbele ya mashabiki wake baada ya kutokuwapo wakati wa Tamasha la Yanga Day.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe alisema:

“Wanayanga wampokee kijana wao na yeye sasa ajisikie yuko nyumbani.”

Mchango wake katika mchezo wa kwanza unamweka miongoni mwa wachezaji watakaotazamwa kwa karibu dhidi ya Gaborone United.

Shalulile, Maxi na Aziz Ki walivyoweka Gaborone macho

Hata kabla ya mchezo wa kwanza, kocha wa Gaborone United Sean Connor alitaja baadhi ya maeneo ya Yanga ambayo yalikuwa yakimpa tahadhari.

Connor alimzungumzia mshambuliaji Peter Shalulile kama moja ya silaha muhimu katika safu ya ushambuliaji ya Yanga.

Kocha huyo pia aliwataja Maxi Nzengeli na Aziz Ki katika eneo la kiungo, akieleza kuwa Yanga ina wachezaji wenye uwezo wa kuleta madhara iwapo watapewa uhuru wa kucheza.

“Unapotakiwa kushindana na timu ya namna hiyo lazima uwe na mpango wa kuwafanya wasicheze kwa uhuru wao,” alisema Connor.

Kauli hiyo inaonyesha aina ya wachezaji ambao Gaborone United imekuwa ikiwaangalia kwa karibu katika maandalizi ya michezo yake dhidi ya Yanga.

Manqoba anahitaji kikosi cha kushambulia

Mngqithi tayari ameonyesha kwamba falsafa yake dhidi ya Gaborone United si kukaa nyuma na kulinda matokeo.

Kabla ya mchezo wa kwanza, kocha huyo alisema:

“Hatuidharau Gaborone hata kidogo, tunakwenda kuikabili na tahadhari kubwa. Kitu ninachoweza kuhakikisha ni hatutacheza kwa lengo la kuzuia, tutakwenda kushambulia.”

Kauli hiyo inaongeza uwezekano wa Yanga kuingia kwenye mchezo wa leo ikiwa na kikosi chenye uwezo mkubwa wa kushambulia, hasa kutokana na umuhimu wa kupata bao mapema.

Ali Kamwe pia ameonya kuhusu uwezo wa Gaborone United kwenye mipira ya kutenga.

“Ni mchezo mgumu kwa sababu ubora wa Gaborone upo kwenye maeneo hatari kwenye mpira.”

Kwa Yanga, kupata bao mapema kunaweza kuwa muhimu katika kupunguza presha na kuwalazimisha wageni kutoka katika mfumo wao wa kujilinda.

Mudathir Yahya naye anaingia kwenye hesabu

Mudathir Yahya alikuwa na mchango muhimu katika bao la Yanga kwenye mchezo wa kwanza baada ya kutoa pasi iliyomaliziwa na Selemani Mwalimu.

Hilo linaifanya safu ya kiungo kuwa moja ya maeneo ambayo yataangaliwa kwa karibu wakati Mngqithi atakapofanya uchaguzi wake wa kikosi cha kwanza.

Gaborone United ilionyesha katika mchezo wa kwanza uwezo wa kujilinda na kuifanya Yanga kutafuta nafasi kwa muda mrefu, hivyo ubunifu wa viungo unaweza kuwa muhimu zaidi katika mchezo wa leo.

Gaborone United si ya kubezwa

Licha ya Yanga kuwa nyumbani, viongozi na benchi la ufundi wameendelea kusisitiza kuwa Gaborone United haiwezi kubezwa.

Kamwe amesema wapinzani hao wana uwezo mkubwa kwenye mipira ya kutenga na wanaweza kutumia nafasi yoyote watakayopewa.

Tahadhari hiyo inamaanisha Yanga haitahitaji tu kikosi chenye uwezo wa kutengeneza mabao, bali pia wachezaji wenye nidhamu wakati timu inapopoteza mpira na katika mipira iliyokufa.

Gaborone United pia iliionyesha Yanga ugumu wake katika mchezo wa kwanza kwa kupata bao la kuongoza kabla ya Selemani kusawazisha katika dakika za nyongeza.

Kikosi rasmi cha Yanga dhidi ya Gaborone United

Kikosi rasmi cha Yanga dhidi ya Gaborone United

Soma Pia: 

  1. Yanga Vs Gaborone United Leo 12/09/2026 Saa Ngapi?
  2. Msimamo Wa Ligi Kuu NBC Tanzania 2026/2027
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo