Karia: Tuzo za TFF 2025/2026 Kutolewa Desemba au Januari

Karia: Tuzo za TFF 2025/2026 Kutolewa Desemba au Januari

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, amesema Tuzo za TFF za msimu wa 2025/2026 zinatarajiwa kutolewa Desemba 2026 au Januari 2027.

Karia amesema maandalizi ya tuzo hizo tayari yameanza, huku TFF ikishirikiana na wadhamini mbalimbali kuhakikisha hafla hiyo inafanyika.

Tuzo za TFF 2025/2026 Kutolewa Desemba au Januari

Maandalizi ya Tuzo za TFF Yaanza

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Karia amesema shirikisho limeanza mchakato wa kuandaa tuzo hizo baada ya tuzo za msimu wa 2024/2025 kutofanyika kutokana na changamoto mbalimbali.

“Msimu wa 2024/2025, tuzo hazijafanyika kwa sababu ya changamoto mbalimbali ambazo nimezizungumzia mara kwa mara,” amesema Karia.

Kutofanyika kwa tuzo za msimu uliopita kuliwafanya wadau na mashabiki wa soka kuendelea kusubiri taarifa kuhusu lini wachezaji na wadau waliofanya vizuri watatambuliwa.

Baadhi ya Washindi Hujulikana Mapema

Karia amesema baadhi ya vipengele, kama vile mfungaji bora na kipa bora, huwa rahisi kupata washindi kwa sababu hutegemea takwimu na vigezo vinavyoonekana moja kwa moja.

Hata hivyo, vipengele vingine vinahitaji mchakato mpana zaidi kabla ya washindi kutangazwa.

“Kwa wengine kunahitaji mchakato unaohitaji muda,” amesema Karia.

Ameongeza kuwa FIFA na CAF pia zina taratibu zao za kutoa tuzo, hivyo mashabiki wanapaswa kuelewa kuwa uteuzi wa baadhi ya washindi hauwezi kukamilishwa mara moja.

TFF sasa inalenga kukamilisha maandalizi kwa kushirikiana na wadhamini ili tuzo za msimu wa 2025/2026 zitolewe kati ya Desemba 2026 na Januari 2027.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Namba Sita Mpya Yanga Huyu Hapa, Ni Fred Duval Ngoma
  2. Simba na Singida Black Stars Zaaga CECAFA Kagame Cup
  3. TFF Yatangaza Adhabu ya Kupoka Pointi Tano kwa Timu Zitakazokwepa Vyumba vya Kubadilishia Nguo
  4. Fabrice Ngoy Aingia Kwenye Rada za Geita Gold Baada ya Kuachana na Namungo
  5. Nyuma ya Usajili wa Nathaniel Chilambo Simba, Kapombe Atajwa
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo