TFF Yatangaza Adhabu ya Kupoka Pointi Tano kwa Timu Zitakazokwepa Vyumba vya Kubadilishia Nguo

TFF Yatangaza Adhabu ya Kupoka Pointi Tano kwa Timu Zitakazokwepa Vyumba vya Kubadilishia Nguo

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, amesema kanuni imerekebishwa ili timu ipokwe pointi tano iwapo itatumia vyumba tofauti na vya kubadilishia nguo vya uwanjani bila sababu za msingi.

Karia amesema TFF imenunua vifaa mbalimbali vitakavyotumika kuchunguza malalamiko yanayotolewa na timu kuhusu vyumba vya kubadilishia nguo.

TFF Yatangaza Adhabu ya Kupoka Pointi Tano kwa Timu Zitakazokwepa Vyumba vya Kubadilishia Nguo

“Kumekuwa na malalamiko mengi ya timu kuhusu vyumba vya kubadilishia nguo, sasa vifaa hivyo tulivyonunua tutavitumia kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa madai mbalimbali ambayo yamekuwa yakisemwa,” amesema Karia.

Ameeleza kuwa uchunguzi ukibaini vyumba vya uwanjani havikuwa na tatizo, timu iliyotumia vyumba vingine itapokwa pointi tano hata kama itakuwa imeshinda mchezo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Yanga kutozwa Sh100 milioni kwa kutumia eneo linalofahamika kama “Jumba Jeupe” katika mechi dhidi ya JKT Tanzania na Simba. Eneo hilo lipo Mbweni, Dar es Salaam.

Karia alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari za michezo katika ofisi za TFF zilizopo Karume, Dar es Salaam.

Soma Pia:

  1. Nyuma ya Usajili wa Nathaniel Chilambo Simba, Kapombe Atajwa
  2. Matokeo ya Simba vs Mogadishu City Leo 25/07/2026
  3. Wachezaji Wapya wa Simba 2026/2027
  4. Cv ya Keletso Makgalwa Winga Mpya Simba Sc 2026/2027
  5. Cv ya Ibrahim Doumbia Mshambuliaji Mpya wa Simba Sc 2026/2027
  6. Ratiba Yanga Ligi Kuu ya NBC 2026/2027 Tanzania
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo