Kikosi cha Yanga vs Azam Leo 21 Juni 2026: Nusu Fainali ya Kombe la CRDB Kirumba
Yanga na Azam FC zinakutana leo Jumapili, Juni 21, 2026, katika nusu fainali ya pili ya Kombe la CRDB kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Mechi hiyo inatarajiwa kuanza saa 9:30 jioni.
Mchezo huu ni muhimu kwa sababu unaamua timu itakayokwenda fainali, huku ukizikutanisha timu mbili zenye ushindani mkubwa katika soka la Tanzania. Kwa mashabiki, Kikosi cha Yanga vs Azam kinatoa picha ya namna Yanga ilivyojipanga kuikabili Azam katika mchezo huu wa mtoano.

Kikosi cha Yanga dhidi ya Azam leo
Hiki ndicho kikosi cha Yanga kilichotangazwa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Azam FC leo.
| Namba | Mchezaji |
|---|---|
| 39 | Diarra |
| 12 | Kirwana |
| 23 | Boka |
| 4 | Bacca |
| 3 | Mwamnyeto |
| 38 | Abuya |
| 7 | Maxi |
| 27 | Mudathir |
| 29 | Dube |
| 20 | Okello |
| 10 | Pacome |
Wachezaji wa akiba wa Yanga: Mshery, Assink, Hussein, Asanal, Aziz, Sheikhan, Damaro, Nabii, Edmund & Depu
Rekodi ya Yanga kwenye Kombe la CRDB
Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na rekodi bora kwenye Kombe la CRDB. Timu hiyo ni bingwa wa mashindano hayo kwa misimu minne mfululizo.
Mara ya mwisho Yanga kupoteza mchezo wa Kombe la CRDB ilikuwa Julai 25, 2021, ilipofungwa bao 1-0 na Simba kwenye fainali iliyopigwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma. Bao hilo lilifungwa na Taddeo Lwanga dakika ya 80.
Tangu hapo, Yanga haijapoteza mchezo wowote wa mashindano hayo hadi leo, ikiwa imetimiza siku 1792, sawa na miaka mitano, miezi 10 na siku 27 bila kupoteza kwenye Kombe la CRDB.
Katika kipindi hicho, Yanga imecheza jumla ya mechi 28 za Kombe la CRDB, imefunga mabao 84 na kuruhusu mabao 10.
Historia ya Yanga na Azam kwenye Kombe la CRDB
Azam FC imekutana na Yanga mara mbili kwenye Kombe la CRDB, na kupoteza mechi zote mbili za fainali.
Mara ya kwanza ilikuwa Juni 12, 2023, kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, ambapo Yanga ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Kennedy Musonda.
Mara ya pili ilikuwa fainali ya msimu wa 2023-2024, iliyopigwa Juni 2, 2024, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Timu hizo zilitoka suluhu ya 0-0 ndani ya dakika 120, kabla ya Yanga kushinda kwa penalti 6-5.
Kukutana tena baada ya siku 57
Yanga na Azam zinakutana leo ikiwa ni siku 57 tangu zilipokutana mara ya mwisho Aprili 25, 2026, katika nusu fainali ya Kombe la Muungano kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Katika mchezo huo, Yanga ilishinda mabao 2-1. Bao la Azam lilifungwa na Feisal Salum ‘Fei Toto’, huku mabao ya Yanga yakifungwa na Prince Dube na Maxi Nzengeli.
Ushindi huo uliipeleka Yanga fainali ya Kombe la Muungano, ambako baadaye ilifungwa bao 1-0 na Simba, Aprili 29, 2026.
Safari ya Yanga na Azam hadi nusu fainali
Yanga na Azam FC zilianzia hatua ya 64 bora katika michuano ya CRDB msimu wa 2025-2026.
Yanga ilianza kwa kuifunga Cosmopolitan mabao 2-0, huku Azam FC ikiifunga Endument FC ya Kilimanjaro bao 1-0.
Katika raundi ya 32, Yanga iliifunga Polisi Tanzania mabao 7-1. Azam FC iliifunga Mbeya Kwanza bao 1-0.
Hatua ya 16 bora, Yanga iliifunga TMA FC bao 1-0, wakati Azam FC iliifunga Fountain Gate mabao 4-0.
Robo fainali, Yanga iliifunga JKT Tanzania mabao 2-0, huku Azam FC ikiiondoa Mashujaa FC kwa ushindi wa bao 1-0.
Kauli za makocha kabla ya mchezo
Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Abdihamid Moallin, alisema maandalizi yamekamilika kwa kiwango kikubwa na wachezaji wako katika morali ya juu. Hata hivyo, alikiri kuwa wanakwenda kukutana na mpinzani mgumu.
“Malenho yetu ni kufanya vizuri katika mechi ya leo bila ya kuangalia siku tatu zijazo tutafanya nini dhidi yao, sio mechi rahisi kwa sababu kila tunapocheza na Azam inatupa ushindani mzuri jambo linalotupa motisha,” alisema Moallin.
Kwa upande wa Azam FC, Kocha Mkuu Florent Ibenge alisema ugumu wa mchezo unatokana na mahitaji na malengo ya kila timu. Pia, ushindi wa mechi sita mfululizo katika mashindano yote unatajwa kuwapa wachezaji wake hamasa kuelekea mchezo huu.
Mapendekezo ya Mhariri:




```





Leave a Reply