Kikosi cha Azam FC Dhidi ya Yanga Leo 21/06/2026 Kombe la CRDB
Kikosi cha Azam FC vs Yanga leo 21/06/2026 kimewekwa wazi kuelekea mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la CRDB utakaopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, kuanzia saa 9:30 jioni.
Mchezo huu unawakutanisha Azam FC na Yanga katika hatua muhimu ya mashindano hayo, kabla ya timu hizo kukutana tena Juni 24, 2026 kwenye pambano la raundi ya pili ya Ligi Kuu Bara litakalopigwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Hiki Apa Kikosi cha Azam FC Kinachoanza Dhidi ya Yanga
- 32 Foba
- 5 Lusajo (C)
- 12 Msindo
- 3 Yoro
- 25 Twalib
- 23 Himid
- 52 Kibeku
- 21 Bin Zayd
- 19 Ngita J.J
- 6 Fei Toto
- 11 Nado
Subs: Manula, Chilambo, Zouzou, Lawi, Songa, Akraminko, Kanoute, Diakite, Zidane, Kitambala.
Azam FC na Yanga Zinarudiana Baada ya Siku 57
Azam FC na Yanga zinakutana leo baada ya siku 57 tangu mara ya mwisho zilipokutana Aprili 25, 2026, katika nusu fainali ya Kombe la Muungano kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Katika mchezo huo, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1. Bao la Azam FC lilifungwa na Feisal Salum ‘Fei Toto’, huku mabao ya Yanga yakifungwa na Prince Dube na Maxi Nzengeli.
Ushindi huo uliipeleka Yanga fainali ya Kombe la Muungano, ambako ilishindwa kutamba baada ya kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Simba, Aprili 29, 2026.
Rekodi ya Yanga Kwenye Kombe la CRDB
Yanga inaingia katika mchezo huu ikiwa na rekodi nzuri kwenye Kombe la CRDB. Timu hiyo ni bingwa wa mashindano hayo kwa misimu minne mfululizo na haijapoteza mchezo wowote wa mashindano hayo tangu Julai 25, 2021.
Mara ya mwisho Yanga kupoteza kwenye michuano hiyo ilikuwa dhidi ya Simba, ilipofungwa bao 1-0 lililofungwa na Taddeo Lwanga dakika ya 80 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Tangu hapo, Yanga imecheza jumla ya mechi 28 za Kombe la CRDB, ikiwa imefunga mabao 84 na kuruhusu mabao 10. Rekodi hiyo ndiyo moja ya changamoto kubwa ambayo Azam FC inakutana nayo leo.
Azam FC pia imekutana na Yanga mara mbili kwenye Kombe la CRDB na kupoteza mechi zote za fainali. Mchezo wa kwanza ulikuwa Juni 12, 2023 kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, ambapo Yanga ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Kennedy Musonda.
Mara nyingine timu hizo zilikutana fainali ya msimu wa 2023-2024, ambapo Yanga ilishinda kwa penalti 6-5 baada ya suluhu ya 0-0 ndani ya dakika 120 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, Juni 2, 2024.
Safari ya Azam FC na Yanga Hadi Nusu Fainali
Timu zote zilianzia hatua ya 64 bora katika Kombe la CRDB msimu wa 2025-2026.
| Hatua | Yanga | Azam FC |
| 64 Bora | Iliifunga Cosmopolitan 2-0 | Iliifunga Endument FC 1-0 |
| Raundi ya 32 | Iliifunga Polisi Tanzania 7-1 | Iliifunga Mbeya Kwanza 1-0 |
| 16 Bora | Iliifunga TMA FC 1-0 | Iliifunga Fountain Gate 4-0 |
| Robo Fainali | Iliifunga JKT Tanzania 2-0 | Iliifunga Mashujaa FC 1-0 |
Matokeo hayo yamezikutanisha timu hizi kwenye nusu fainali ya Kombe la CRDB, huku kila upande ukiwa na nafasi ya kutafuta tiketi ya kwenda fainali.

Kauli za Makocha Kabla ya Mchezo
Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Abdihamid Moallin, alisema maandalizi yamekamilika kwa kiwango kikubwa na wachezaji wako katika morali ya juu. Hata hivyo, alikiri ugumu wa mchezo kutokana na aina ya mpinzani na ubora alionao.
“Malenho yetu ni kufanya vizuri katika mechi ya leo bila ya kuangalia siku tatu zijazo tutafanya nini dhidi yao, sio mechi rahisi kwa sababu kila tunapocheza na Azam inatupa ushindani mzuri jambo linalotupa motisha,” alisema Moallin.
Kwa upande wa Azam FC, Kocha Mkuu Florent Ibenge alisema ugumu wa mchezo huo unatokana na mahitaji ya kila timu na malengo yake. Pia alisema ushindi wa mechi sita mfululizo katika mashindano yote unawapa hamasa wachezaji wake kwa ajili ya kupambana.
Mapendekezo ya Mhariri:




```





Leave a Reply