Yanga Yatwaa Ubingwa wa Tano Mfululizo NBC Premier League 2025/26

Yanga Yatwaa Ubingwa wa Tano Mfululizo NBC Premier League 2025/26

Yanga bingwa NBC Premier League 2025/26 baada ya kuifunga JKT Tanzania mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Meja Janerali Isamuhyo. Ushindi huo umeifanya Yanga kufikisha pointi 75 na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya tano mfululizo. Kwa jumla, Wananchi wamefikia ubingwa wao wa 32 wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara.

Yanga Yatwaa Ubingwa wa Tano Mfululizo NBC Premier League 2025/26

Yanga Yaichapa JKT Tanzania Kwa Mabao 3-0

Katika mchezo huo, Yanga ilianza kupata bao la kwanza dakika ya 8 kupitia Dube, kabla ya Maxi kuongeza la pili dakika ya 51.

Depu alihitimisha ushindi huo dakika ya 66, akiipa Yanga matokeo ya 3-0 dhidi ya Maafande wa JKT Tanzania.

FT: JKT Tanzania 0-3 Yanga SC

⚽ 08’ Dube
⚽ 51’ Maxi
⚽ 66’ Depu

Yanga Yamaliza Kileleni Kwa Pointi 75

Yanga SC imehitimisha msimu ikiwa juu ya timu zote zinazoshiriki NBC Premier League, ikifikisha pointi 75 baada ya mechi 30 za msimu wa 2025/26. Simba SC imemaliza nafasi ya pili ikiwa na pointi 73, alama mbili nyuma ya Yanga. Azam FC imeshika nafasi ya tatu kwa pointi 62, huku Singida Black Stars ikikamilisha nafasi nne za juu ikiwa na pointi 50.

NafasiTimuPointi
1Yanga SC75
2Simba SC73
3Azam FC62
4Singida Black Stars50

Ubingwa wa Tano Mfululizo Kwa Wananchi

Kutwaa taji la msimu wa 2025/26 kunaifanya Yanga kuendelea kuandika rekodi yake ya kutawala Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa imetetea ubingwa huo kwa msimu wa tano mfululizo.

Kwa matokeo hayo, Yanga imefunga msimu ikiwa bingwa wa NBC Premier League 2025/26 na kuongeza idadi ya mataji yake ya Ligi Kuu Tanzania Bara hadi 32.

Mosi Ndumumwe Aibuka Mfungaji Bora

Mshambuliaji wa Singida Black Stars, Mosi Ndumumwe, ameibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/26.

Ndumumwe amemaliza msimu akiwa na jumla ya mabao 17, baada ya kufunga hat-trick katika kipigo cha 4-3 dhidi ya Fountain Gate FC.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Yanga vs JKT Tanzania Leo 30/06/2026
  2. JKT Tanzania vs Yanga Leo 30/06/2026 Saa Ngapi?
  3. Ratiba ya Ligi Kuu NBC Leo Juni 30, 2026: Yanga, Simba Kuamua Ubingwa Raundi ya Mwisho
  4. Simba Yatoa Tamko Kuhusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Kuchezwa Pemba
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo