Timu Zilizofuzu Nusu Fainali CRDB Federation Cup 2026

Timu Zilizofuzu Nusu Fainali CRDB Federation Cup 2026

Hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB Federation Cup msimu wa 2026 imeanza kutimua vumbi leo, ambapo mashabiki wa soka wameshuhudia michezo miwili ya ushindani iliyoanza kutoa sura ya hatua inayofuata ya michuano hiyo.

Michezo hiyo imepigwa katika viwanja vya Meja Isamuhyo, Mbweni na Mkakwani, Tanga, huku kila timu ikisaka nafasi ya kuendelea kubaki kwenye mbio za kutinga hatua ya nusu fainali.

Hizi Apa Timu Zilizotanguilia Hatua ya Nusu Fainali

Timu zilizotangulia kufuzu hatua ya nusu fainali ya CRDB Federation Cup 2026 ni Yanga na Coastal Union.

Yanga imekata tiketi hiyo baada ya kuifunga JKT Tanzania mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Meja Isamuhyo, Mbweni. Coastal Union nayo imefuzu baada ya kuiondoa Singida BS kwa mikwaju ya penalti 4-2 Uwanja wa Mkakwani, Tanga, baada ya dakika 90 kumalizika kwa suluhu.

Yanga iliingia kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania ikiwa imetoka kupoteza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji kwa mabao 3-2. Huo ulikuwa mchezo wake wa kwanza baada ya kupoteza kwa mara ya kwanza kwenye ligi msimu huu.

Licha ya mchezo huo kutajwa kuwa mgumu kutokana na historia ya Yanga kutopata ushindi kwenye uwanja huo, kikosi cha Jangwani kilionyesha ubora na kutawala vipindi vyote viwili.

Kwenye kikosi kilichoanza, beki na nahodha Bakari Mwamnyeto hakuwamo hata kwenye benchi, huku nafasi yake ikichukuliwa na Frank Assinki, ambaye alionyesha kiwango kizuri.

JKT Tanzania ilijikuta nyuma dakika ya 33 baada ya beki Hassan Wahabi kujifunga wakati akijaribu kuokoa krosi ya Chadrack Boka. Dakika sita baadaye, Mudathir Yahaya alifunga bao la pili kwa Yanga baada ya kuiwahi pasi ya Pacome Zouzoua na kumalizia kirahisi mbele ya kipa Ramadhan Chalamanda.

Mabao hayo yaliifanya Yanga kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa 2-0. Kipindi cha pili, Yanga iliendelea kutengeneza nafasi kupitia kwa Dube, Okello na Boka, lakini ikakosa umakini kwenye matumizi ya nafasi hizo hadi mchezo kumalizika kwa ushindi huo.

Hii ni mara ya pili Yanga kuiondoa JKT Tanzania kwenye michuano hiyo, baada ya msimu uliopita kuifunga pia mabao 2-0 katika hatua ya nusu fainali.

Timu Zilizofuzu Nusu Fainali CRDB Federation Cup 2026

Matukio Muhimu ya Robo Fainali

Katika mchezo wa mapema, Coastal Union ilifanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kuifunga Singida BS kwa penalti 4-2. Mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Mkakwani, Tanga, ulimalizika kwa suluhu ndani ya dakika 90 kabla ya kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti.

Kwa matokeo hayo, Coastal Union sasa inasubiri mshindi kati ya Simba na TRA, mchezo unaotarajiwa kupigwa Uwanja wa KMC Complex. Yanga nayo inasubiri mshindi kati ya Mashujaa na Azam.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya JKT Tanzania VS Yanga Leo 16/05/2026
  2. Matokeo ya Coastal Union vs Singida Bs Leo 16/05/2026
  3. Azam TV Kuonesha Mechi Zote 104 za Kombe la Dunia 2026 Mbashara
  4. Msimamo wa Ligi Kuu Wanawake Tanzania (TWPL) 2025/2026
  5. Robo fainali CRDB Bank Federation Cup 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo