Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2026
Baraza la Mitihani la Tanzania, National Examinations Council of Tanzania, limetangaza rasmi ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Sekondari ya Juu (ACSEE) kwa mwaka 2026. Ratiba hii inaonesha kwa kina tarehe, muda na masomo yote yatakayofanyiwa mtihani kwa watahiniwa wa Kidato cha Sita kote Tanzania.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mitihani imepangwa kuanza mapema mwezi Mei 2026 na kuendelea hadi mwishoni mwa mwezi huo, ikihusisha vipindi vya asubuhi na alasiri pamoja na mitihani ya vitendo kwa baadhi ya masomo.
Muhtasari wa Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2026
- Siku ya Kuanza kwa Mitihani: Jumatatu, 04 Mei 2026
- Kumalizika: Jumatatu, 25 Mei 2026
Vipindi vya Mtihani
Ratiba inaonesha kuwa mitihani itafanyika katika vipindi viwili vikuu:
- Kipindi cha Asubuhi (A.M): Saa 2:00 – 5:00 asubuhi (8:00 – 11:00)
- Kipindi cha Mchana (P.M): Saa 8:00 – 11:00 jioni (2:00 – 5:00)
Aidha, baadhi ya mitihani ya vitendo imepangwa kufanyika kwa muda maalum tofauti, hasa kuanzia saa 4:00 asubuhi (10:00) hadi saa 7:20 mchana (1:20), kulingana na somo husika.

Mwanzo wa Mitihani: Msisitizo kwa Masomo ya Msingi
Siku ya kwanza ya mitihani, watahiniwa wataanza na somo la General Studies katika kipindi cha asubuhi, somo ambalo ni la lazima kwa watahiniwa wote wa ACSEE. Katika kipindi cha mchana siku hiyo hiyo, masomo kadhaa yataanza ikiwa ni pamoja na History 1, Biology 1, Chinese Language 1 pamoja na Accountancy 1, yakifungua rasmi mfululizo wa mitihani ya kitaaluma.
Siku zinazofuata zinaonesha msongamano wa masomo ya msingi na ya mchepuo kama vile Physics, Chemistry, Economics, Geography pamoja na lugha mbalimbali, zikionesha upana wa tathmini kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita.
Wiki ya Pili: Mchanganyiko wa Nadharia na Vitendo
Kuanzia tarehe 11 Mei 2026, ratiba inaonesha kua wanafunzi watakua wakifanya mitihani ya vitendo kwa wingi. Masomo kama Biology, Chemistry, Physics, pamoja na Fine Art na Computer Science, yatafanyiwa tathmini ya vitendo ili kupima uelewa wa wanafunzi katika matumizi halisi ya maarifa yao.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mitihani ya vitendo imepangwa kwa makundi tofauti (3A, 3B, 3C), hatua inayolenga kurahisisha usimamizi wa watahiniwa wengi katika vituo mbalimbali vya mtihani.
Awamu ya mwisho ya mitihani itaendelea hadi tarehe 25 Mei 2026, ambapo somo la Chemistry 3C (Practical) litahitimisha rasmi mchakato mzima wa mitihani ya ACSEE kwa mwaka huo.
Mpangilio huu unaonyesha jinsi tathmini ya mwisho ya Kidato cha Sita inavyolenga kutoa fursa sawa kwa wanafunzi wote, huku ikizingatia aina mbalimbali za masomo na mbinu za upimaji.
Maelekezo Muhimu kwa Watahiniwa
Katika ratiba hiyo, NECTA imesisitiza mambo kadhaa muhimu:
- Watahiniwa wanapaswa kufuata kwa makini maelekezo yote yaliyopo kwenye Notice to Candidates.
- Endapo kutatokea tofauti yoyote kati ya ratiba na karatasi ya mtihani, taarifa iliyo kwenye karatasi ya mtihani ndiyo itakayotumika.
- Mitihani itaendelea kama ilivyopangwa hata kama itaangukia siku ya sikukuu ya umma.
Mapendekezo ya Mhariri:








Leave a Reply