Viingilio Mechi ya Simba VS Yanga 03/05/2026

Viingilio Mechi ya Simba VS Yanga 03/05/2026

Baada ya pazia la Kariakoo Derby ya fainali ya Mapinduzi Cup kushuka kwa drama ya mikwaju ya penalti iliyoshuhudia Simba ikiibuka na ushindi, macho ya mashabiki sasa yanaelekezwa kwenye pambano jingine kubwa la Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Safari hii, Yanga SC wanarejea uwanjani wakiwa na shauku ya kujibu mapigo, huku Simba wakiwa na dhamira ya kuendeleza ubabe wao. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam, Jumapili ya tarehe 03 Mei 2026, ukiwa ni miongoni mwa mechi zinazotarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi nchini.

Viingilio Mechi ya Simba VS Yanga 03/05/2026

Klabu ya Simba imetangaza rasmi viingilio vya mchezo huo, ikigawa tiketi katika madaraja matatu ili kuruhusu mashabiki wa rika mbalimbali kupata nafasi ya kushuhudia pambano hilo kubwa.

Bei za tiketi ni kama ifuatavyo:

  • Mzunguko – Tsh 15,000
  • VIP B – Tsh 30,000
  • VIP A – Tsh 50,000

Mpangilio huu wa bei umezingatia upatikanaji wa mashabiki wengi zaidi, huku ukilenga kutoa fursa kwa kila shabiki kuhudhuria bila vikwazo vikubwa vya gharama.

Viingilio Mechi ya Simba VS Yanga 03/05/2026

Muda wa Mchezo na Mahali

Kariakoo Derby hii itapigwa kuanzia saa 12:00 jioni katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, ambapo Simba watakuwa wenyeji wakiwakaribisha wapinzani wao wakubwa, Yanga SC.

Kauli Rasmi Kutoka Simba

Akizungumza na waandishi wa habari Mei 1, 2026, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alithibitisha kuanza rasmi kwa mauzo ya tiketi na kutoa wito kwa mashabiki kuchukua hatua mapema.

Alisema:

“Hatujataka kuweka viingilio vya juu sana ili kumpa nafasi kila Mwanasimba kuingia uwanjani. Kwa uwezo wa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, tungeweza kuweka viingilio vikubwa, lakini tumezingatia kuweka viwango rafiki.”

Kauli hiyo inaonyesha wazi dhamira ya klabu kuhakikisha mashabiki wengi wanapata nafasi ya kushuhudia mchezo huo mkubwa bila kubanwa na gharama.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Ligi Kuu Ya NBC Leo 01/05/2026
  2. Matokeo ya Yanga vs Simba Leo 29/04/2026 Fainali Kombe la Mapinduzi
  3. Wafungaji Bora Mapinduzi Cup 2026
  4. Ratiba ya Fainali Mapinduzi Cup 2026
  5. Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Kombe la Muungano 2026
  6. Vilabu Bora Afrika 2026/2027 (CAF Club Ranking)
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo