Idadi ya Makombe ya UEFA Real Madrid

Idadi ya Makombe ya UEFA Real Madrid | Jumla ya Makombe ya Klabu Bingwa Ulaya ya Real Madrid

Real Madrid, wababe wa soka kutoka Hispania, imeendeleza utawala wake katika soka la Ulaya kwa kutwaa kombe la 15 la Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) baada ya kuifunga Borussia Dortmund kwenye fainali ya kusisimua iliyofanyika Uwanja wa Wembley June 01 2024.

Ushindi huu ni wa sita kwa Real Madrid ndani ya miaka kumi iliyopita, na unathibitisha zaidi nafasi yao kama timu yenye mafanikio makubwa katika historia ya mashindano haya ya kifahari. Timu hiyo ya Hispania ilionyesha ubabe wao uwanjani kwa mchezo wa kusisimua na ushindi wa kishindo. Los Blancos, kama wanavyojulikana, walikuwa na mfululizo wa ushindi katika mashindano haya, wakishinda kila mchezo tangu hatua ya makundi. Ubora wao uwanjani na uzoefu katika mechi kubwa uliwapa faida kubwa dhidi ya Borussia Dortmund.

Idadi ya Makombe ya UEFA Real Madrid

Idadi ya Makombe ya UEFA Real Madrid

Real Madrid imekuwa na utawala mkubwa katika soka ya Ulaya, hasa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Wameshiriki katika fainali 18, wakishinda 15 na kupoteza tatu pekee. Idadi hii ya mataji ni mara mbili ya AC Milan, timu iliyopo nafasi ya pili kwa mataji mengi.

Hii apa Orodha ya Misimu ambayo Real Madrid ameshinda UEFA

SnSEASONWINNER
152023-24Real Madrid
142021-22Real Madrid
132017-18Real Madrid
122016-17Real Madrid
112015-16Real Madrid
102013-14Real Madrid
92001-02Real Madrid
81999-2000Real Madrid
71997-98Real Madrid
61965-66Real Madrid
51959-60Real Madrid
41958-59Real Madrid
31957-58Real Madrid
21956-57Real Madrid
11955-56Real Madrid

Mapendekezo Ya Mhariri:

  1. Viingilio vya Fainali ya Kombe la Shirikisho CRDB 2024: Bei na Maeneo ya Kununua Tiketi Yatangazwa!
  2. Ley Matampi Golikipa mwenye Clean Sheet Nyingi Ligi Kuu NBC 2023/2024
  3. Timu za Tanzania Zilizofuzu Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
  4. Timu Zilizofuzu Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
  5. Muonekano wa Kombe La CRDB Federation Cup 2023/2024
  6. Harry Kane Ndio Mshindi wa Kiatu cha Dhahabu Ulaya 2023-2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo