Mfungaji Bora Ligi Kuu ya NBC 2025/2026 ni Mossi Ndumumwe
Mfungaji Bora Ligi Kuu ya NBC 2025/2026 ni mshambuliaji wa Singida Black Stars, Mossi Ndumumwe, aliyemaliza msimu akiwa na mabao 17 na kuongoza orodha ya wafungaji wa ligi.

Ndumumwe amewazidi wapinzani wake wa karibu baada ya kumaliza juu ya jedwali la wafungaji, huku Feisal Salum wa Azam akifuata nafasi ya pili akiwa na mabao 15. Kiungo wa Young Africans, Allan Okello, ameshika nafasi ya tatu kwa kufunga mabao 14.
Wafungaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC 2025/2026
Jedwali la wafungaji bora wa NBC Premier League msimu wa 2025/2026 limekamilika kama ifuatavyo:
Nafasi | Mchezaji | Klabu | Magoli |
| 1 | Mossi Ndumumwe | Singida BS | 17 |
| 2 | Feisal Salum | Azam | 15 |
| 3 | Allan Okello | Young Africans | 14 |
| 4 | Mathew Tegisi | Pamba Jiji | 11 |
| 5 | Fabrice Wa Ngoy | Namungo | 11 |
| 6 | Pacome Zouzoua | Young Africans | 9 |
| 7 | Mudathir Yahya | Young Africans | 9 |
| 8 | Prince Dube | Young Africans | 9 |
| 9 | Selemani Mwalimu | Simba | 9 |
| 10 | Paul Peter | JKT Tanzania | 9 |
| 11 | Maabad Maulid | Coastal Union | 8 |
| 12 | Iddy Selemani | Azam | 8 |
| 13 | Clatous Chama | Simba | 8 |
| 14 | Saleh Karabaka | JKT Tanzania | 8 |
| 15 | Laurindo Dilson Depu | Young Africans | 8 |
| 16 | William Edgar | Dodoma Jiji | 7 |
| 17 | George Mpole | Tanzania Prisons | 7 |
| 18 | Libasse Gueye | Simba | 7 |
| 19 | Jephte Kitambala | Azam | 7 |
| 20 | Elie Mpanzu | Simba | 7 |
| 21 | Chukwunonye Obasi | Fountain Gate | 6 |
Ndumumwe Aongoza Mbio za Ufungaji
Mossi Ndumumwe ameumaliza msimu akiwa kinara wa mabao kwa kufunga mara 17 na hivyo kutwaa heshima ya kuwa Mfungaji Bora Ligi Kuu ya NBC 2025/2026. Nyuma yake anafuatia Feisal Salum wa Azam mwenye mabao 15, huku Allan Okello wa Young Africans akimaliza nafasi ya tatu kwa mabao 14.
Young Africans Yatoa Wachezaji Wengi Kwenye Orodha
Young Africans ndiyo klabu yenye wachezaji wengi zaidi ndani ya orodha ya wafungaji bora wa msimu huu. Mbali na Allan Okello aliyemaliza na mabao 14, klabu hiyo pia ina Pacome Zouzoua, Mudathir Yahya na Prince Dube waliomaliza na mabao tisa kila mmoja pamoja na Laurindo Dilson Depu aliyefunga mabao nane.
Simba, Azam na Klabu Nyingine Pia Zawakilishwa
Simba imeingiza Selemani Mwalimu, Clatous Chama, Libasse Gueye na Elie Mpanzu kwenye mbio za kuwania kiatu cha dhahabu ambapio nyota hao wote wameshindwa kufikia idaki ya magoli ya Mossi. Azam imewakilishwa na Feisal Salum, Iddy Selemani na Jephte Kitambala, huku JKT Tanzania ikiwa na Paul Peter na Saleh Karabaka.
Pamba Jiji, Namungo, Coastal Union, Dodoma Jiji, Tanzania Prisons na Fountain Gate pia zimekuwa na wachezaji walioingia kwenye orodha ya wafungaji bora wa NBC Premier League msimu wa 2025/2026.
Mapendekezo ya Mhariri:




```







Leave a Reply