Matokeo ya Simba SC vs Dodoma Jiji Leo 24/05/2026
Simba SC inashuka uwanjani leo Jumapili, Mei 24, 2026, kuikaribisha Dodoma Jiji katika mchezo muhimu wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kupigwa Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 12:15 jioni.
Mchezo huu una uzito mkubwa kwa Simba, ambayo inaendelea kupambana katika mbio za kileleni mwa msimamo wa NBC Premier League 2025/2026. Wekundu hao wanaingia kwenye mechi hii wakiwa nafasi ya pili na pointi 55 baada ya michezo 24, nyuma ya Young Africans yenye pointi 57.
Kwa upande wa Dodoma Jiji, mchezo huu ni nafasi nyingine ya kuimarisha nafasi yake kwenye msimamo. Timu hiyo ipo nafasi ya nane ikiwa na pointi 33, sawa na Pamba Jiji ambayo pia ina pointi 33.
Matokeo ya Simba SC vs Dodoma Jiji Leo Live
Fuatilia matokeo ya Simba SC vs Dodoma Jiji leo kupitia live score hapa chini. Updates za mchezo zitaonekana kadri mchezo utakavyoendelea.
Muhtasari wa Mechi
| Mechi | Simba SC vs Dodoma Jiji |
| Tarehe | 24/05/2026 |
| Mashindano | NBC Premier League 2025/2026 |
| Uwanja | KMC Complex, Dar es Salaam |
| Muda | Saa 12:15 jioni |
| Simba SC | Nafasi ya 2, pointi 55 |
| Dodoma Jiji | Nafasi ya 8, pointi 33 |
Simba Inahitaji Matokeo ya Ushindi
Kwa Simba, matokeo ya leo yana maana kubwa kwenye mbio za ubingwa. Ushindi dhidi ya Dodoma Jiji utaipeleka timu hiyo hadi pointi 58 na kuirudisha juu ya msimamo wa ligi.
Simba ilishuka nafasi ya pili baada ya Yanga kurejea kileleni ikiwa na pointi 57. Hivyo, mchezo huu unaipa Simba nafasi ya kurejesha presha kwa wapinzani wake wakubwa kwenye vita ya ubingwa.
Kama Simba itashindwa kushinda, itasalia nafasi ya pili, hali ambayo inaweza kuwa nafuu kwa Yanga kwenye msimamo.
Dodoma Jiji Inatafuta Pointi Muhimu
Dodoma Jiji inaingia kwenye mchezo huu ikiwa nafasi ya nane na pointi 33. Timu hiyo inahitaji matokeo mazuri ili kujiweka kwenye nafasi bora zaidi kwenye msimamo.
Angalau pointi moja inaweza kuisaidia Dodoma Jiji kuishusha Pamba Jiji, ambayo nayo ina pointi 33. Hii inaifanya mechi hii kuwa muhimu kwa pande zote mbili, licha ya Simba kuingia ikiwa na presha kubwa zaidi ya mbio za kileleni.
Rekodi ya Simba SC Dhidi ya Dodoma Jiji
Takwimu za makutano ya timu hizi zinaonyesha Simba imekuwa na rekodi bora dhidi ya Dodoma Jiji. Katika mechi 11 ambazo timu hizo zimekutana, Simba imeshinda 10 na kutoka sare moja.
Katika michezo hiyo, Simba imefunga mabao 22, huku Dodoma Jiji ikifunga mabao mawili pekee.
Hata hivyo, Dodoma Jiji iliwapa Simba wakati mgumu kwenye mchezo wa Februari 25, 2026, baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana. Simba ilitengeneza nafasi nyingi kwenye mchezo huo, lakini haikuweza kupata bao.
Wachezaji wa Kuangaliwa Leo
Clatous Chama anaingia kwenye mchezo huu akiwa mmoja wa wachezaji muhimu zaidi kwa Simba. Kiungo huyo amekuwa kwenye kiwango bora, akibeba tuzo tano mfululizo za mchezaji bora wa mechi.
Chama amefunga mabao manane na kutoa asisti sita, akihusika kwenye jumla ya mabao 14. Katika mchezo wa mwisho dhidi ya Coastal Union, alitengeneza mabao yote mawili ya Simba kwenye ushindi wa 2-1.
Eneo la ushambuliaji pia litakuwa na macho mengi. Kocha Steve Barker amekuwa akimtumia Elie Mpanzu kama mshambuliaji kinara, huku Seleman Mwalimu akiachwa nje katika baadhi ya chaguo la kuanza.
Kwa Dodoma Jiji, Edgar William ndiye kinara wa mabao wa timu hiyo akiwa na mabao saba. Mshambuliaji huyo tayari ameifunga Yanga msimu huu kwenye mchezo uliopigwa KMC Complex, ambapo Dodoma Jiji ilifungwa 3-1.
Kauli za Makocha Kabla ya Mchezo
Kocha msaidizi wa Simba, Suleiman Matola, amesema mchezo dhidi ya Dodoma Jiji hautakuwa rahisi, hasa kutokana na namna timu hiyo ilivyowapa upinzani kwenye mchezo uliopita.
“Haitakuwa mechi rahisi, ukiangalia matokeo ya mechi iliyopita tulipokutana nao walitupa wakati mgumu pamoja na upinzani mkubwa lakini pamoja na ugumu na ubora wao, tumejipanga kuhakikisha tunapata pointi tatu katika mchezo wa kesho (leo).”
Kwa upande wa Dodoma Jiji, kocha Amani Josiah amesema timu yake imejiandaa vizuri na inatambua kuwa presha kubwa ipo kwa Simba kutokana na malengo yao kwenye ligi.
“Tumejiandaa vizuri kwenda kukutana na Simba, tutaingia tukiwa kama timu ya pili lakini mchezo utakuwa wa presha kubwa kwa Simba, tunawaheshimu ni timu nzuri lakini watahitaji matokeo kutokana na malengo yao lakini na sisi tunataka matokeo kujiweka sehemu nzuri zaidi.”
Mwenendo wa Simba na Dodoma Jiji Kabla ya Mechi
Simba imekuwa na mwenendo mzuri kwenye mechi zake tano za mwisho. Timu hiyo imeshinda michezo minne dhidi ya Coastal Union, Mashujaa, Tanzania Prisons na JKT Tanzania, huku ikipata sare moja dhidi ya Yanga.
Dodoma Jiji nayo haijaingia kwenye mchezo huu ikiwa dhaifu. Katika mechi tano za mwisho, imeshinda mbili dhidi ya Yanga na Mtibwa Sugar, na kutoka sare tatu.
Ushindi wa Dodoma Jiji dhidi ya Yanga kwa mabao 3-2 unaongeza tahadhari kwa Simba, hasa kwa kuwa timu hiyo imeonyesha inaweza kupata matokeo dhidi ya timu zinazowania nafasi za juu.
Ratiba Nyingine za Ligi Leo
Mbali na Simba SC dhidi ya Dodoma Jiji, kuna michezo mingine ya Ligi Kuu Bara inayochezwa leo.
Saa 10:00 jioni, TRA United itaikaribisha Fountain Gate kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha. TRA United ina pointi 37 na inahitaji ushindi ili kupanda hadi nafasi ya nne kwa kufikisha pointi 40.
Fountain Gate ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 26, na ushindi unaweza kuisaidia kupanda hadi nafasi ya tisa.
Kocha wa Fountain Gate, Fred Felix Minziro, alisema:
“Tumejiandaa Vizuri na mchezo na vijana wapo tayari kwa kupambana, siyo mechi rahisi lakini hakuna kuingia kinyonge, tunazihitaji alama tatu kesho (leo).”
Mchezo mwingine wa saa 10:00 jioni ni Mtibwa Sugar dhidi ya JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Saa 2:30 usiku, Coastal Union itacheza dhidi ya Mashujaa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Unaweza Kusoma Pia








Leave a Reply