Matokeo ya Simba vs TRA United Leo 17/05/2026

Matokeo ya Simba vs TRA United Leo 17/05/2026

Wekundu wa Msimbazi Simba leo watakuwa dimbani kuisaka tiketi ya kufuzu nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB Federation Cup, ambapo watachuana vikali dhidi ya wabishi TRA United katika mtanange utakaotimua vumbi katika dimba la KMC jijini Dar es Salaam.

Mchezo huu unasubiriwa kwa hamu kubwa, huku mashabiki wakifuatilia kwa karibu matokeo ya Simba vs TRA United leo 17/05/2026, kutokana na umuhimu wake katika mbio za kufuzu hatua ya nusu fainali.

Simba inaingia kwenye mchezo huu ikijua inahitaji ushindi ili kusonga mbele kwenye michuano ambayo imeikosa kwa misimu minne. Wekundu wa Msimbazi wana rekodi ya kubeba taji hili mara nne, huku mara ya mwisho wakitwaa ubingwa msimu wa 2020/2021 baada ya kuifunga Yanga bao 1-0.

Timu hizi tayari zimekutana mara mbili msimu huu katika ligi. Simba ilishinda mchezo mmoja, huku mechi ya mwisho baina yao ikimalizika kwa sare tasa ugenini mjini Arusha.

Mara ya mwisho Simba ilipoikaribisha TRA United katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, iliondoka na ushindi wa mabao 3-0. Hata hivyo, mchezo wa leo unaweza kuwa na presha tofauti kwa kuwa ni wa mtoano.

Macho ya wengi yatakuwa kwa winga wa TRA United, Ramadhan Salum Chobwedo, ambaye anatarajiwa kuwa na vita kali dhidi ya beki wa kushoto wa Simba, Nickson Kibabage. Mara ya mwisho wawili hao kukutana, Chobwedo alionyesha ubora wake katika baadhi ya nyakati, ingawa pia alikumbana na upinzani mkubwa kutoka kwa Kibabage.

Matokeo ya Simba vs TRA United Leo 17/05/2026

Kikosi cha Simba dhidi ya TRA United

Simba imemtaja Kassa langoni, huku safu ya ulinzi ikiwa na Duchu, Kibabage, Toure C na De Reuck.

Eneo la kiungo lina Kagoma, Gueye, Kante, Mpanzu na Chama, wakati Oura akianza kwenye safu ya ushambuliaji.

Kikosi cha Simba:
39 Kassa, 15 Duchu, 32 Kibabage, 25 Toure C, 23 De Reuck, 21 Kagoma, 7 Gueye, 8 Kante, 34 Mpanzu, 17 Chama, 20 Oura.

Kwenye Benchi: Abel, Chasambi, Miiro, Vedastus, Nazi, Semfuko, Mwalimu, Morice, Inno, Bashiri.

Kikosi cha TRA United dhidi ya Simba

TRA United imeanza na Noel langoni, huku safu ya ulinzi ikiwa na Isaack, Nouma, Kombo C na Christopher.

Katika eneo la mbele, timu hiyo itawategemea wachezaji kama Chobwedo, Mapaka, Ally na Enock kuisumbua safu ya ulinzi ya Simba.

Kikosi cha TRA United:
1 Noel GK, 36 Isaack, 45 Nouma, 5 Kombo C, 4 Christopher, 14 Jamaly, 11 Chobwedo, 30 Mbaa, 16 Mapaka, 21 Ally, 46 Enock.

Kwenye Benchi: 39 Fikirini, 36 Omary, 8 Kapama, 40 Nkane, 6 Mugoya, 27 Ouchi, 10 Chilunda, 28 Chewe, 22 Azarus, 23 Mussa.

Fuatilia Hapa Matokeo ya Simba vs TRA United Leo 17/05/2026

Simba Sc2-0TRA United
  • SIMBA SC 🆚 TRA United
  • 🏆 CRDB Bank Federation Cup (#CRDBBFC)
  • 🏟 Uwanja wa KMC Complex – Dar es Salaam.
  • 📆 17.05.2026
  • 🕓 12:30 Jioni

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Timu Zilizofuzu Nusu Fainali CRDB Federation Cup 2026
  2. Matokeo ya JKT Tanzania VS Yanga Leo 16/05/2026
  3. Matokeo ya Coastal Union vs Singida Bs Leo 16/05/2026
  4. Azam TV Kuonesha Mechi Zote 104 za Kombe la Dunia 2026 Mbashara
  5. Matokeo ya Simba Queens vs Yanga Princess Leo 15/05/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo