Yanga vs Namungo Leo 25/05/2026 Saa Ngapi?
Mchezo wa Yanga vs Namungo leo 25/05/2026 utapigwa majira ya saa 12:30 jioni katika Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam, ikiwa ni moja ya michezo ya muendelezo wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026.
Mchezo huu unawakutanisha Yanga SC, ambao wanahitaji ushindi ili kurejea kwenye nafasi ya juu ya msimamo, dhidi ya Namungo FC ya Lindi, wanaopambana kujiondoa kwenye hatari ya kushuka daraja.
Taarifa Kuhusu Yanga vs Namungo Leo
| Mechi | Yanga SC vs Namungo FC |
| Tarehe | 25/05/2026 |
| Muda | Saa 12:30 jioni |
| Uwanja | KMC Complex |
| Mashindano | Ligi Kuu ya NBC |

Yanga Kusaka Pointi Tatu Muhimu
Yanga wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na hesabu za wazi. Wanahitaji ushindi ili kujiweka vizuri kwenye mbio za nafasi ya juu ya msimamo, hasa baada ya kurejea kwenye njia ya ushindi kwa kuichapa Singida BS mabao 3-0.
Kwa Wananchi, kuangusha pointi kwenye mchezo huu kunaweza kuwa pigo kubwa katika mbio za ubingwa. Hiyo ndiyo sababu mchezo dhidi ya Namungo unabeba uzito mkubwa kwa benchi la ufundi na wachezaji.
Kocha wa muda wa Yanga, Abdihamid Moalin, amesema maandalizi yao yamekwenda vizuri, huku akisisitiza kuwa timu yake imejifunza kutokana na matokeo ya nyuma.
“Kila mmoja anajua kilichotokea kwenye mechi yetu dhidi ya Dodoma Jiji, unazungumzia takwimu, haikuwa timu ambayo imewahi kutufunga (Dodoma), lakini ikafanikiwa kufanya hivyo, tumejifunza, tunaiheshimu Namungo ina kocha mzuri na wachezaji wazuri, tunachotaka ni kuendelea kushinda,” amesema Moalin.
Namungo Wanaingia na Presha ya Msimamo
Namungo nao hawana mchezo mwepesi. Timu hiyo ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 25, na matokeo mabaya yanaweza kuongeza presha zaidi kwenye mapambano ya kujinasua na eneo la hatari.
Kulingana na taarifa zilizopo, Namungo imekosa matokeo ya ushindi kwenye mechi 13 zilizopita, hali inayoufanya mchezo wa leo kuwa na umuhimu mkubwa kwao.
Kocha Mgunda amesema mchezo huu ni muhimu kwa timu yake kutokana na nafasi waliyonayo kwenye msimamo.
“Mechi hii ni muhimu sana kwetu kutokana na nafasi tuliyopo kwenye msimamo lakini hata wapinzani wetu nao ni mechi muhimu kutokana na nafasi waliyonayo, itakuwa mechi yenye ushindani, maandalizi yetu yamekamilika tayari kwa mchezo huo,” amesema Mgunda.
Rekodi ya Yanga Dhidi ya Namungo
Rekodi za mechi za nyuma zinaipa Yanga nguvu zaidi kabla ya mchezo wa leo.
Timu hizi zimekutana mara 12, ambapo Yanga imeshinda michezo saba na kutoka sare tano. Namungo haijawahi kuifunga Yanga kwenye michezo hiyo.
Katika michezo hiyo 12, Yanga imefunga jumla ya mabao 20, huku Namungo ikifunga mabao saba pekee.
Hali ya Wachezaji wa Yanga
Yanga bado inaangalia hali ya kiungo Pacome Zouzoua, ambaye alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Singida BS. Hata hivyo, taarifa zilizopo zinaeleza kuwa majeraha yake hayakuwa makubwa.
Kiungo Allan Okello yupo kwenye kiwango bora na anatarajiwa kuendelea kuwa sehemu muhimu kwenye eneo la ushambuliaji. Mchezaji huyo wa Uganda amefunga mabao tisa na kutoa asisti saba, akiwa amehusika kwenye jumla ya mabao 16.
Mapendekezo ya Mhariri:







Leave a Reply