Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2026

Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2026

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, limetangaza rasmi Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2026 kwa watahiniwa wa Mtihani wa Cheti cha Juu cha Elimu ya Sekondari (ACSEE).

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mitihani imepangwa kuanza tarehe 04 Mei 2026 na itahitimishwa tarehe 25 Mei 2026, ikihusisha mitihani ya nadharia pamoja na mitihani ya vitendo (practical).

Ratiba hii ni nyaraka muhimu kwa wanafunzi, walimu na wasimamizi wa mitihani, kwani inaeleza kwa kina siku, muda na masomo yote yatakayofanyiwa mtihani katika vipindi vya asubuhi na alasiri.

Muhtasari wa Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2026

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na NECTA, mitihani itafanyika kwa vipindi viwili vikuu:

  • Kipindi cha Asubuhi (A.M.): Kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi 5:00 asubuhi kwa masomo mengi ya nadharia, na saa 4:00 asubuhi hadi 7:20 mchana au saa 4:00 asubuhi hadi 9:00 mchana kwa baadhi ya mitihani ya vitendo.
  • Kipindi cha Alasiri (P.M.): Kuanzia saa 8:00 mchana hadi 11:00 jioni.

Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2026 – Masomo ya Nadharia

Jumatatu – 04/05/2026

KipindiSomo
AsubuhiGeneral Studies
AlasiriHistory 1, Chinese Language 1, Biology 1, Accountancy 1

Jumanne – 05/05/2026

KipindiSomo
AsubuhiKiswahili 1, Physics 1, Agriculture 1, Commerce 1, Food and Human Nutrition 1
AlasiriGeography 1, Physical Education 1, French Language 1, Education

Jumatano – 06/05/2026

KipindiSomo
AsubuhiKiswahili 2, Basic Applied Mathematics, Advanced Mathematics 1
AlasiriEnglish Language 1, Chemistry 1, Economics 1

Alhamisi – 07/05/2026

KipindiSomo
AsubuhiGeography 2, Agriculture 2, Accountancy 2, Food and Human Nutrition 2
AlasiriFine Art 1, Chinese Language 2, Physics 2, Economics 2

Ijumaa – 08/05/2026

KipindiSomo
AsubuhiHistory 2, Biology 2
AlasiriEnglish Language 2, Chemistry 2, Commerce 2

Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2026 – Masomo ya Practical

Jumatatu – 11/05/2026

KipindiSomo
AsubuhiFrench Language 2, Agriculture 3 (Practical), Advanced Mathematics 2, Food and Human Nutrition 3 (Practical)
AlasiriDivinity 1, Islamic Knowledge 1

Jumanne – 12/05/2026

KipindiSomo
AsubuhiFine Art 2 (Practical), Biology 3A (Practical)
AlasiriComputer Science 1, Information and Computer Studies

Jumatano – 13/05/2026

KipindiSomo
AsubuhiChemistry 3A (Practical)
AlasiriArabic Language 1

Alhamisi – 14/05/2026

KipindiSomo
AsubuhiPhysics 3A (Practical)
AlasiriDivinity 2, Islamic Knowledge 2

Ijumaa – 15/05/2026

KipindiSomo
AsubuhiComputer Science 2 (Practical)
AlasiriArabic Language 2

Ratiba ya Practical – Makundi B na C

Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo