Matokeo ya Yanga vs Simba Leo 12/08/2026 Ngao ya Jamii
Wekundu wa Msimbazi Simba SC na Yanga SC leo watafungua rasmi pazia la msimu wa 2026/2027 watakapo chuana vikali katika fainali ya Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.
Dabi hiyo ya Kariakoo inawakutanisha watani hao wa jadi katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku kila timu ikiwa na lengo la kuanza msimu mpya kwa kutwaa taji.
Yanga inaingia kwenye mchezo ikiwa na lengo la kuendelea kushikilia Ngao ya Jamii, wakati Simba ikisaka kulirejesha taji hilo baada ya misimu miwili bila kulibeba.
Mchezo huo utaanza saa 2:30 usiku, huku vikosi vya kwanza vya timu zote mbili tayari vikiwa vimetangazwa.
Matokeo ya Yanga vs Simba Leo 12/08/2026
| Yanga Sc | 1-0 | Simba Sc |
Mchezo huo unatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa soka kutokana na ushindani wa muda mrefu kati ya Yanga na Simba pamoja na uwepo wa wachezaji wapya katika timu zote mbili.

Kikosi cha Simba vs Yanga Leo
Kocha wa Simba, Steve Barker, amefanya maamuzi yake na kuanza na Mamadou Kassali langoni.
Safu ya ulinzi ina David Kameta Duchu, Nickson Kibabage, Ismael Toure na Rushine De Reuck.
Katikati ya uwanja wameanza Yusuf Kagoma, Lebase Gueye na Ibrahim Jabaar, huku safu ya mbele ikiwa na Ibrahim Doumbia, Clatous Chama na Anicet Oura.
Starting XI ya Simba
- 39 Mamadou Kassali
- 15 David Kameta Duchu
- 3 Nickson Kibabage
- 25 Ismael Toure
- 23 Rushine De Reuck
- 21 Yusuf Kagoma
- 7 Lebase Gueye
- 8 Ibrahim Jabaar
- 29 Ibrahim Doumbia
- 17 Clatous Chama
- 20 Anicet Oura
Wachezaji wa Simba walio kwenye benchi ni Abel, Chilambo, Mligo, Vedastus, Semfuko, Msimu, Inno, Mpanzu, Morice na Keletso.
Kikosi cha Yanga vs Simba Leo
Yanga, chini ya kocha Manqoba Mngqithi, imeanza na Diarra langoni.
Katika ulinzi wameanza Yao, Boka, Bakari Mwamnyeto ambaye ni nahodha, pamoja na Bacca.
Eneo la kiungo lina Duke Abuya, Kangwanda na Mudathir, huku safu ya mbele ikiwa na Peter Shalulile, Maxi Nzengeli na Houssein Zakouani.
Starting XI ya Yanga
- 39 Diarra
- 21 Yao
- 23 Boka
- 36 Bakari Mwamnyeto (Nahodha)
- 4 Bacca
- 38 Duke Abuya
- 22 Kangwanda
- 27 Mudathir
13 Peter Shalulile - 7 Maxi Nzengeli
- 11 Houssein Zakouani
Benchi la Yanga lina Mshery, Husseini, Kazimoto, Mahsen, Mussa, Abdulnassir, SureBoy, Edmund, Okello na Toure.
Shalulile Aanza Dabi ya Kariakoo
Mshambuliaji Peter Shalulile ni miongoni mwa wachezaji wanaovuta perhatian kubwa katika mchezo huu baada ya kupewa nafasi ya kuanza kwa Yanga.
Shalulile ametua Yanga akitokea Mamelodi Sundowns na leo atakuwa akikabiliwa na Simba katika dabi yake ya kwanza ya Kariakoo.
Kwa upande wa Simba, Clatous Chama ana uzoefu mkubwa wa michezo hii akiwa amecheza dabi 21 rasmi za Kariakoo na kufunga mabao manne.
Chama na Doumbia Kwenye Safu ya Simba
Barker ameamua kumtumia Ibrahim Doumbia kuanzia mwanzo pamoja na Chama na Oura.
Doumbia anaweza kuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika kutengeneza presha kwa safu ya ulinzi ya Yanga, wakati Chama akitarajiwa kutumia uzoefu wake katika kutengeneza nafasi.
Simba pia ina wachezaji kama Mpanzu na Keletso kwenye benchi ambao wanaweza kutumika kuongeza nguvu wakati mchezo ukiendelea.
Soma Pia:
- Kikosi cha Yanga vs Simba Leo 12/08/2026 Ngao ya Jamii
- Kikosi cha Simba vs Yanga Leo 12/08/2026
- Yanga vs Simba Leo 12/08/2026 Saa Ngapi?
- Rayon Sports Yaifunga Gor Mahia 2-1 na Kutwaa Ubingwa wa CECAFA Kagame 2026
- Ratiba ya Klabu Bingwa Afrika 2026/2027 CAF Hatua ya Awali
- Ratiba ya Kombe la Shirikisho 2026/2027 Hatua ya Awali




```





Leave a Reply