Matokeo ya Yanga VS Fountain Gate Leo 18/06/2026: Updates za Ligi Kuu Bara
Yanga inacheza dhidi ya Fountain Gate leo, Juni 18, 2026, katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, kuanzia saa 10:00 jioni.
Fuatilia matokeo ya Yanga SC dhidi ya Fountain Gate leo kupitia ukurasa huu, ambapo taarifa za mchezo zitawekwa mubashara kadri pambano hilo la Ligi Kuu Bara litakavyoendelea Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi 63 baada ya kucheza mechi 26. Mabingwa hao watetezi wameshinda mechi 19, kutoka sare sita na kupoteza mchezo mmoja.
Fountain Gate, ambayo ni mwenyeji wa mchezo huu, ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 29 baada ya kucheza mechi 26. Timu hiyo imeshinda mechi nane, kutoka sare tano na kupoteza michezo 13.
Katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizi msimu huu, Yanga iliifunga Fountain Gate mabao 2-0.

Kikosi cha Yanga Dhidi ya Fountain Gate
Yanga imeanza na Diarra langoni, huku wachezaji wengine waliotajwa kwenye kikosi cha leo wakiwa Yao, Hussein, Mwamnyeto, Bacca, Abuya, Maxi, Mudathir, Depu, Okello na Pacome.
Wachezaji waliopo benchi ni Masalanga, Assink, Boka, Andabwile, Asanal, Damaro, Farid, Edmund, Nabil na Dube.
Muktadha wa Mchezo
Kocha wa Fountain Gate, Fredy Felix ‘Minziro’, amesema malengo ya timu yake ni kujiondoa kwenye nafasi za hatari na kuepuka kabisa presha ya michezo ya Play-Off.
“Malengo yetu ni kuhakikisha tunatoka nafasi zote za hatari kwa maana ya kuondoka kabisa kwenye mechi za Play-Off’, sio rahisi kwa sababu ya gepu dogo la pointi na washindani wetu, hivyo, bado tuna kazi kubwa ya kufanya,” alisema Minziro.
Kwa upande wa Yanga, Kaimu Kocha Mkuu Abdihamid Moallin amesema mechi zilizobaki ni ngumu kutokana na mahitaji ya kila timu, lakini kikosi chake kimejipanga kutimiza malengo ya msimu.
“Mechi zote zilizobaki kwa sasa ni ngumu kwa sababu ya mahitaji ya kila mmoja wetu, tunatambua tutakutana na mazingira ya aina hiyo, ila tumejipanga kuhakikisha malengo tuliyoweka tangu kuanza kwa msimu huu tunayatimiza,” alisema Moallin.
Umuhimu wa Matokeo ya Leo
Kwa Yanga, mchezo huu ni sehemu ya kampeni ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara. Kwa Fountain Gate, mchezo huu una umuhimu katika juhudi za kujiondoa kwenye nafasi za hatari.
Matokeo ya mchezo huu yataendelea kuonekana mubashara kupitia sehemu ya live updates, huku Yanga na Fountain Gate zikipambana katika mchezo muhimu wa Ligi Kuu Bara jijini Arusha.
Mapendekezo ya Mhariri:




```





Leave a Reply