Kikosi cha Simba Vs JKT Leo 06/05/2026
Simba itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi leo, Mei 6, 2026, itakapoikaribisha JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam, kuanzia saa 12:15 jioni.
Mchezo huo una umuhimu mkubwa kwa Simba, ambayo inahitaji pointi tatu ili kuendelea kujiimarisha katika nafasi ya pili na kuendelea kuifukuzia nafasi ya kwanza. Kwa upande wa JKT Tanzania, mechi hii ni nafasi ya kujaribu kuvunja rekodi mbaya dhidi ya Simba na kuondoka na matokeo chanya.
Simba inaingia uwanjani ikiwa na pointi 43 baada ya kucheza mechi 20. Katika michezo hiyo, imeshinda 12, imetoka sare saba na kupoteza mchezo mmoja. Pia imefunga mabao 39 na kuruhusu mabao tisa.

JKT Tanzania, ambayo ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 32, imecheza mechi 20, ikishinda nane, kutoka sare nane na kupoteza michezo minne. Timu hiyo imefunga mabao 21 na kuruhusu mabao 20.
Kocha wa Simba, Steve Barker, anaamini timu yake bado ina nafasi ya kuwania ubingwa wa ligi msimu huu licha ya kuwa nyuma ya Yanga kwa pointi tano. Amesema lengo lao katika kila mchezo ni kupata ushindi ili kubaki kwenye nafasi nzuri ya kupambania malengo ya klabu.
“Matarajio ya kila mechi ni kuhakikisha tunashinda ili kujiweka nafasi nzuri ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu, mechi ni ngumu lakini wachezaji wapo tayari kwa kupambania malengo ya klabu,” amesema Barker.
Kwa upande wa JKT Tanzania, kocha Ahmad Ally amesema hawataki kupoteza tena dhidi ya Simba baada ya kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Novemba 8, 2025.
“Haitakuwa mechi rahisi, itakuwa ya mbinu zaidi. Mzunguko wa kwanza tulifungwa lakini matarajio yetu kwa sasa ni kuvuna pointi tatu,” amesema kocha Ally.
Hiki Apa Kikosi cha Simba Vs JKT Leo 06/05/2026
| Namba ya Jezi | Jina la Mchezaji |
| 39 | Kassali |
| 15 | Kapombe (C) |
| 32 | Kibabage |
| 25 | Toure |
| 23 | De Reuck |
| 21 | Kagoma |
| 7 | Gueye |
| 35 | Neo |
| 34 | Mpanzu |
| 10 | Inno |
| 17 | Chama |
Kwenye Benchi: Abel, Duchu, Mligo, Vedastus, Semfuko, Chasambi, Kante, Mwalimu, Morice & Bashiri
Rekodi Za Simba Dhidi Ya JKT Tanzania
Rekodi zinaipa Simba nguvu kubwa kuelekea mchezo huu. Katika mechi saba zilizopita, Simba imeifunga JKT Tanzania mfululizo, jambo linaloweka presha kwa Wanajeshi hao wanaohitaji kubadili historia hiyo.
Kwa ujumla, timu hizo zimekutana mara 11 ndani ya ligi. Simba imeshinda michezo 10, huku JKT Tanzania ikishinda mchezo mmoja. Hakuna sare iliyopatikana katika mechi hizo.
Umuhimu Wa Mchezo Wa Leo
Kwa Simba, ushindi utakuwa hatua muhimu katika kuendelea kujiimarisha nafasi ya pili na kuendeleza presha kwenye mbio za juu ya msimamo. Matokeo yasiyoridhisha yanaweza kuipa nafasi Azam kuishusha, kutegemea na matokeo yake dhidi ya Namungo.
Kwa JKT Tanzania, mchezo huu una maana kubwa zaidi ya pointi tatu. Ni nafasi ya kuonyesha uwezo dhidi ya timu ambayo imekuwa na rekodi nzuri mbele yao katika miaka ya karibuni.
Mchezo wa Simba dhidi ya JKT Tanzania unatarajiwa kuwa wa mbinu na ushindani kutokana na nafasi za timu zote mbili kwenye msimamo, rekodi zao na malengo tofauti kuelekea mwisho wa msimu. Simba inaingia ikiwa na rekodi bora, lakini JKT Tanzania ina nafasi ya kupambana kutafuta matokeo yatakayobadili mwendelezo wa historia baina ya pande hizo mbili.
Mapendekezo ya Mhariri:







Leave a Reply