Kikosi cha Simba Vs El-Qanah Egypt Mechi Ya Kirafiki (22 July 2024)

Kikosi cha Simba Vs El-Qanah Egypt Mechi Ya Kirafiki (22 July 2024)

Wekundu wa Msimbazi, Simba Sports Club, itaanza msimu wake wa michezo ya kirafiki kwa kucheza dhidi ya El-Qanah kutoka Misri. Mechi hii itatimua vumbi tarehe 22 Julai 2024 katika Uwanja wa Old Suez Canal. Lengo kuu la mechi hii ni kuwapa nafasi wachezaji wapya wa Simba kuonyesha uwezo wao, pamoja na kocha mpya, Fadlu Davids, kuonyesha mbinu zake za mchezo.

Mechi hii ya kirafiki ina malengo kadhaa muhimu kwa Simba SC kuelekea msimu wa 2024/2025. Miongoni mwa malengo muhimu ya mchezo huu wa kirafiki dhidi ya El-Qanah Egypt ni pamoja na;

1. Kuwapa Nafasi Wachezaji Wapya: Simba imesajili wachezaji wapya katika dirisha hili la usajili. Mechi hii itawapa fursa ya kuonyesha vipaji vyao na kujenga muunganiko mzuri na wachezaji wa zamani.

2. Mtihani wa Mbinu za Kocha Mpya: Fadlu Davids, kocha mpya wa Simba, atakuwa na nafasi ya kujaribu mbinu zake za mchezo kabla ya mechi muhimu dhidi ya Yanga SC katika ngao ya jamii. Hii itasaidia kutambua maeneo yanayohitaji kuboreshwa.

Mechi hii inatarajiwa kuwa ya kusisimua na yenye ushindani mkubwa. Kwa mashabiki wa Simba SC na wapenzi wa soka kwa ujumla, huu ni mtanange usiofaa kukosa. Endelea kufuatilia habari na taarifa zaidi kuhusu mchezo huu kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.

Kikosi cha Simba Vs El-Qanah Egypt Mechi Ya Kirafiki (22 July 2024)

Kikosi kinachoanza Leo dhidi ya El-Qanah: Ally Salim (1) Shomari Kapombe (12) Mohamed Hussein (15) Karaboue Chamou (2) Che malone (20) Mzamiru Yassin (19) Yusuph Kagoma (21) Edwin Balua (16) Joshua Mutale (7) Jean Charles Ahoua (10) Freddy Michael (18).

Hapa chini tumekuletea orodha ya wachezaji wanaotarajiwa kuunda kikosi cha Simba SC dhidi ya El-Qanah Egypt

MAGOLIKIPA

  • Ayoub Lakred ๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ฆ
  • Ally Salim ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
  • Hussein Abeli ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

MABEKI

  • Che Fondoh Malone ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฒ
  • Abdulrazack Hamza ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
  • Hussein Kazi ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
  • Chamou Karaboue ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฎ
  • Shomari Kapombe ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
  • Valentin Nouma ๐Ÿ‡ง๐Ÿ‡ซ
  • Mohammed Hussein ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
  • Israel Mwenda ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

VIUNGO WAKABAJI

  • Augustine Okejepha ๐Ÿ‡ณ๐Ÿ‡ฌ
  • Yusuph Kagoma ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
  • Fabrice Ngoma ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฉ
  • Mzamiru Yassin ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
  • Debora Mavambo ๐Ÿ‡ฌ๐Ÿ‡ฆ

VIUNGO WASHAMBULIAJI

  • Jean Charles Ahoua ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฎ
  • Kibu Denis Prosper ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
  • Omary Omary ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
  • Joshua Mutale ๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡ฒ
  • Edwin Balua ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
  • Ladack Chasambi ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
  • Salehe Karabaka ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

WASHAMBULIAJI

  • Freddy Michael Kouablan ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฎ
  • Valentino Mashaka ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
  • Steven Dese Mukwala ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ฌ

Kikosi cha Simba Vs El-Qanah Egypt Mechi Ya Kirafiki (22 July 2024)

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. APR Yatangulia Fainali Cecafa Dar Port Kagame Cup 2024
  2. Matokeo ya Yanga vs FC Augsburg Leo 20 Julai 2024: Yaliyojiri Uwanjani
  3. Kikosi Cha Yanga Vs FC Augsburg Mpumalanga Cup 20/July/2024
  4. Matokeo Azam FC vs US Yacoub El Mansour Leo (20/07/2024) | Mechi ya Kirafiki
  5. Awesu na Onana Watua Misri Kujiunga na Kambi ya Mazoezi ya Simba
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo