Kiungo wa Austria Canadi Marcelo Atua Singida Black Stars

Kiungo wa Austria Canadi Marcelo Atua Singida Black Stars

Klabu ya Singida Black Stars imemtambulisha rasmi kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Austria, Canadi Marcelo, kuwa mchezaji wao mpya.

Marcelo mwenye umri wa miaka 28 amejiunga na Singida Black Stars kwa uhamisho huru baada ya mkataba wake na Enosis Neon Paralimni FC ya Cyprus kumalizika Januari 2026.

Kiungo wa Austria Canadi Marcelo Atua Singida Black Stars

Canadi Marcelo ajiunga na Singida Black Stars

Usajili huo unamleta Marcelo katika Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kucheza katika nchi mbalimbali katika safari yake ya soka.

Kiungo huyo amewahi kupitia shule ya vipaji ya Borussia Mönchengladbach ya Ujerumani kabla ya kuendelea na maisha yake ya soka katika klabu nyingine.

Klabu alizowahi kuchezea Canadi Marcelo

Marcelo amewahi kuzichezea SKU Amstetten na SV Ried za Austria. Pia amepita Brisbane Roar ya Australia, FC Hebar ya Bulgaria na Lexington SC ya Marekani.

Kabla ya kujiunga na Singida Black Stars, alikuwa akiichezea Enosis Neon Paralimni FC ya Cyprus. Alikuwa bila klabu tangu Januari 2026 baada ya mkataba wake na timu hiyo kumalizika.

Kutambulishwa kwake kunamfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wapya waliojiunga na Singida Black Stars kuelekea msimu mpya.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Beki wa Nigeria Benjamin Tanimu Atua Singida Black Stars
  2. Singida Black Stars Yakaribia Kukamilisha Usajili wa Ahoua
  3. Wachezaji Wapya Yanga Sc 2026/2027
  4. Wachezaji Wapya wa Simba 2026/2027
  5. Simba Yaipiku Raja Athletic Usajili wa Keletso Makgalwa
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo