Wafungaji Bora Kombe la Dunia 2026 (Vinara Wa Magoli Kombe la Dunia)

Wafungaji Bora Kombe la Dunia 2026 (Vinara Wa Magoli Kombe la Dunia)

Orodha ya Wafungaji Bora Kombe la Dunia 2026 sasa ina vinara watatu baada ya Erling Haaland kufikisha magoli nane na kuwafikia Lionel Messi na Kylian Mbappé katika mbio za Golden Boot.

Haaland alifunga mara mbili katika mchezo wa hatua ya 16 bora kati ya Norway na Brazil, na kuifanya vita ya kiatu cha dhahabu kuwa wazi zaidi. Messi, Mbappé na Haaland sasa wana magoli manane kila mmoja, huku Mbappé akiwa na faida kwa assists zake mbili.

Wafungaji Bora Kombe la Dunia 2026 (Vinara Wa Magoli Kombe la Dunia)

Wafungaji Bora Kombe la Dunia 2026: Vinara wana magoli 8

Erling Haaland amejiunga rasmi na Messi na Mbappé kileleni mwa orodha ya wafungaji Kombe la Dunia 2026 baada ya kufunga magoli mawili dhidi ya Brazil.

Mshambuliaji huyo wa Norway alifunga mara mbili katika kipindi cha pili na kufikisha jumla ya magoli nane kwenye mashindano. Magoli hayo yameifanya nafasi ya kwanza katika mbio za Golden Boot Kombe la Dunia 2026 kugawanywa na wachezaji watatu.

Kabla ya Haaland kufikisha idadi hiyo, Mbappé alikuwa amemfikia Messi kwa kufunga penalti dhidi ya Paraguay na kusajili goli lake la nane.

Messi alikuwa amechukua uongozi peke yake baada ya kufunga dhidi ya Cape Verde, lakini Mbappé akamfikia wakati hatua za mtoano zikianza. Sasa Haaland ameongeza ushindani baada ya mabao yake mawili dhidi ya Brazil.

Orodha ya wafungaji bora Kombe la Dunia 2026

Hii ndiyo orodha kamili ya vinara wa magoli Kombe la Dunia 2026 kulingana na takwimu zilizopo:

PlayerCountryGoalsAssists
Erling HaalandNorway80
Kylian MbappéFrance82
Lionel MessiArgentina80
Harry KaneEngland50
Ousmane DembéléFrance42
Mikel OyarzabalSpain41
Vinícius JúniorBrazil41
Ismaïla SarrSenegal41
Deniz UndavGermany32
Johan ManzambiSwitzerland31
Julián QuiñonesMexico31
Cody GakpoNetherlands31
Brian BrobbeyNetherlands30
Folarin BalogunUnited States30
Matheus CunhaBrazil30
Elijah JustNew Zealand30
Jonathan DavidCanada30
Cristiano RonaldoPortugal30
Ismael SaibariMorocco30
Kai HavertzGermany30

Nani anaongoza mbio za Golden Boot Kombe la Dunia 2026?

Kwa idadi ya magoli, Haaland, Messi na Mbappé wako sawa baada ya kila mmoja kufikisha magoli manane.

Hata hivyo, Kylian Mbappé ndiye mwenye faida kwa sasa katika kigezo cha kwanza cha FIFA cha kuvunja sare, kutokana na kuwa na assists mbili. Messi na Haaland hawajasajili assist hadi sasa.

Hivyo, endapo mashindano yangemalizika katika hali hiyo, Mbappé ndiye angepewa Golden Boot.

Mbio bado ziko wazi kwa sababu mashindano yanaendelea kuelekea hatua ya robo fainali na bado kuna mechi za kuchezwa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Kombe la Dunia Leo 01/07/2026
  2. Timu Zilizofuzu 16 Bora Kombe la Dunia 2026
  3. Timu za Afrika Zilizofuzu Hatua ya 32 Bora Kombe la Dunia 2026
  4. Ratiba ya Hatua ya 32 Bora Kombe la Dunia 2026
  5. Ratiba ya Mechi za Hatua ya 32 Bora Kombe la Dunia 2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo