Kikosi cha Yanga vs JKT Tanzania Leo 30/06/2026

Kikosi cha Yanga vs JKT Tanzania Leo 30/06/2026

Kikosi cha Yanga leo kitashuka dimbani katika kibarua cha kuhakikisha kinatetea ubingwa wake wa Ligi Kuu ya NBC, ambapo kitachuana uso kwa uso na JKT Tanzania katika mchezo unaotarajiwa kuwa na mvuto mkubwa.

Mchezo huu utatimua vumbi leo Jumanne, Juni 30, 2026, majira ya saa 10:00 jioni katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.

Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa kileleni mwa msimamo baada ya kukusanya pointi 72 katika mechi 29. Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 70, hivyo matokeo ya leo yana maana kubwa katika mbio za ubingwa.

Kikosi cha Yanga vs JKT Tanzania Leo 30/06/2026

Kikosi cha Yanga Kiko Tayari

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Abdihamid Moallin, amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo huo muhimu dhidi ya JKT Tanzania.

Moallin amesema wachezaji wote wako fiti na wana morali ya juu kuelekea mchezo wa mwisho wa msimu. Amesisitiza kuwa Yanga inatambua ubora wa JKT Tanzania na italazimika kucheza kwa umakini mkubwa ili kupata matokeo inayoyahitaji.

“JKT ni timu nzuri yenye kocha bora na iliyopangwa vizuri. Tunafahamu uwezo wao, hivyo tunapaswa kucheza kwa kiwango cha juu na kuwa makini hasa upande wa ulinzi. Lengo letu ni kushinda mchezo na kusherehekea ubingwa baada ya hapo,” amesema Moallin.

Kauli hiyo inaonyesha kuwa Yanga haitarajii mchezo mwepesi, licha ya kuwa kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa.

Hiki Apa Kikosi cha Yanga Kilichotangazwa

  • DIARRA
  • YAO
  • HUSSEIN
  • ASSINKI
  • BACCA
  • ABUYA ©
  • MAXI
  • DUBE
  • DEPU
  • OKELLO
  • PACOME

Benchi: Mshery, Kibwana, Boka, Abubakar Aziz, Damaro, SureBoy, Abdulnassir, Mudathir, Edmund.

Kikosi Rasmi cha Yanga Kimewekwa Wazi?

Kikosi rasmi cha kuanzia cha Yanga dhidi ya JKT Tanzania kinatarajiwa kutangazwa mjira ya saa 9 alasiri muda mchache kabla ya mechi kuanza. Benchi la ufundi la Yanga limeweka wazi kuwa wachezaji wake wako katika hali nzuri kiafya na wapo tayari kwa mchezo. Hilo linaifanya timu hiyo kuwa na nafasi ya kupanga kikosi chenye ushindani kulingana na mpango wa mwalimu.

Kwa kawaida, kikosi rasmi cha kuanzia hutangazwa karibu na muda wa mchezo. Mashabiki wa Yanga watasubiri kuona majina yatakayopewa nafasi ya kuanza katika mchezo huu wa saa 10:00 jioni.

Wachezaji wa Yanga Wanaotajwa Kabla ya Mechi

Miongoni mwa wachezaji wa Yanga wanaotajwa kuelekea mchezo huu ni Allan Okello na Emmanuel Mwanengo.

Okello anaingia kwenye raundi ya mwisho akiwa kwenye mbio za kuwania tuzo ya mfungaji bora. Ana mabao 14, akiwa nyuma ya Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Azam FC mwenye mabao 15.

Kwa Okello, mchezo dhidi ya JKT Tanzania una maana mbili: kuisaidia Yanga katika mbio za ubingwa na kuendelea kupambana kwenye orodha ya wafungaji bora.

Mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Mwanengo, amesema mchezo huu ndio unaoamua hatima ya ubingwa kwa timu yao.

“Hata ushindi wa bao moja unatosha kutupa ubingwa. Tunaamini mbele ya mashabiki wetu tutafanya vizuri na kumaliza kazi,” amesema Mwanengo.

JKT Tanzania Nayo Haijaingia Kinyonge

JKT Tanzania inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na lengo la kumaliza msimu kwa matokeo mazuri. Kocha wa timu hiyo, Ahmad Ally, amesema maandalizi ya kikosi chake yanaendelea vizuri licha ya safari ndefu kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam.

Ally amesema wachezaji wake wako katika hali nzuri kiafya, isipokuwa Edson Katanga ambaye atakosekana kutokana na adhabu ya kadi.

“Mchezo utakuwa mgumu kwa sababu kila timu ina malengo yake. Sisi tupo hapa kwa ajili ya kutimiza malengo ya JKT, si kuangalia timu nyingine zinafanya nini. Tutacheza kwa nidhamu ya kimkakati na kuhakikisha tunafanya kila tuwezalo kupata matokeo mazuri,” amesema Ally.

Nyota wa JKT Tanzania, Nassor Maulid, amesema morali ndani ya kikosi ipo juu na wachezaji wamejipanga kufuata maelekezo ya benchi la ufundi.

“Sisi tuna malengo yetu kama ambavyo wapinzani wetu wana malengo yao. Tutapambana kuhakikisha tunamaliza msimu kwa matokeo mazuri,” amesema Maulid.

Hesabu za Ubingwa Zikoje?

Yanga inaongoza msimamo ikiwa na pointi 72 baada ya mechi 29, huku Simba ikiwa nafasi ya pili na pointi 70. Tofauti ya pointi mbili inaifanya Yanga kuwa kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa.

Ushindi dhidi ya JKT Tanzania utaifanya Yanga kutwaa ubingwa wa tano mfululizo. Sare pia inaweza kuitosha kulingana na matokeo ya Simba dhidi ya KMC.

Kwa upande wa Simba, hesabu ni kushinda mchezo wake dhidi ya KMC katika Uwanja wa KMC Complex, kisha kusubiri matokeo ya JKT Tanzania vs Yanga SC.

Taarifa Muhimu za Mechi

KipengeleTaarifa
MechiJKT Tanzania vs Yanga SC
TareheJumanne, Juni 30, 2026
MudaSaa 10:00 jioni
UwanjaMeja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam
MashindanoLigi Kuu ya NBC
YangaPointi 72 baada ya mechi 29
SimbaPointi 70 baada ya mechi 29

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Simba Yatoa Tamko Kuhusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Kuchezwa Pemba
  2. KMKM Bingwa Tena FA Zanzibar Baada ya Kuifunga Chipukizi Fainali ya Pemba
  3. Matokeo ya Simba vs Singida Black Stars Leo 27 Juni 2026
  4. Azam FC Yakaribia Kukamilisha Usajili wa Nyota Wawili Kutoka DR Congo
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo