Kikosi cha Azam FC Dhidi ya Yanga Leo 21/06/2026 Kombe la CRDB

Kikosi cha Azam FC Dhidi ya Yanga Leo 21/06/2026 Kombe la CRDB

Kikosi cha Azam FC vs Yanga leo 21/06/2026 kimewekwa wazi kuelekea mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la CRDB utakaopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, kuanzia saa 9:30 jioni.

Mchezo huu unawakutanisha Azam FC na Yanga katika hatua muhimu ya mashindano hayo, kabla ya timu hizo kukutana tena Juni 24, 2026 kwenye pambano la raundi ya pili ya Ligi Kuu Bara litakalopigwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Hiki Apa Kikosi cha Azam FC Kinachoanza Dhidi ya Yanga

  • 32 Foba
  • 5 Lusajo (C)
  • 12 Msindo
  • 3 Yoro
  • 25 Twalib
  • 23 Himid
  • 52 Kibeku
  • 21 Bin Zayd
  • 19 Ngita J.J
  • 6 Fei Toto
  • 11 Nado

Subs: Manula, Chilambo, Zouzou, Lawi, Songa, Akraminko, Kanoute, Diakite, Zidane, Kitambala.

Azam FC na Yanga Zinarudiana Baada ya Siku 57

Azam FC na Yanga zinakutana leo baada ya siku 57 tangu mara ya mwisho zilipokutana Aprili 25, 2026, katika nusu fainali ya Kombe la Muungano kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Katika mchezo huo, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1. Bao la Azam FC lilifungwa na Feisal Salum ‘Fei Toto’, huku mabao ya Yanga yakifungwa na Prince Dube na Maxi Nzengeli.

Ushindi huo uliipeleka Yanga fainali ya Kombe la Muungano, ambako ilishindwa kutamba baada ya kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Simba, Aprili 29, 2026.

Rekodi ya Yanga Kwenye Kombe la CRDB

Yanga inaingia katika mchezo huu ikiwa na rekodi nzuri kwenye Kombe la CRDB. Timu hiyo ni bingwa wa mashindano hayo kwa misimu minne mfululizo na haijapoteza mchezo wowote wa mashindano hayo tangu Julai 25, 2021.

Mara ya mwisho Yanga kupoteza kwenye michuano hiyo ilikuwa dhidi ya Simba, ilipofungwa bao 1-0 lililofungwa na Taddeo Lwanga dakika ya 80 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Tangu hapo, Yanga imecheza jumla ya mechi 28 za Kombe la CRDB, ikiwa imefunga mabao 84 na kuruhusu mabao 10. Rekodi hiyo ndiyo moja ya changamoto kubwa ambayo Azam FC inakutana nayo leo.

Azam FC pia imekutana na Yanga mara mbili kwenye Kombe la CRDB na kupoteza mechi zote za fainali. Mchezo wa kwanza ulikuwa Juni 12, 2023 kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, ambapo Yanga ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Kennedy Musonda.

Mara nyingine timu hizo zilikutana fainali ya msimu wa 2023-2024, ambapo Yanga ilishinda kwa penalti 6-5 baada ya suluhu ya 0-0 ndani ya dakika 120 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, Juni 2, 2024.

Safari ya Azam FC na Yanga Hadi Nusu Fainali

Timu zote zilianzia hatua ya 64 bora katika Kombe la CRDB msimu wa 2025-2026.

HatuaYangaAzam FC
64 BoraIliifunga Cosmopolitan 2-0Iliifunga Endument FC 1-0
Raundi ya 32Iliifunga Polisi Tanzania 7-1Iliifunga Mbeya Kwanza 1-0
16 BoraIliifunga TMA FC 1-0Iliifunga Fountain Gate 4-0
Robo FainaliIliifunga JKT Tanzania 2-0Iliifunga Mashujaa FC 1-0

Matokeo hayo yamezikutanisha timu hizi kwenye nusu fainali ya Kombe la CRDB, huku kila upande ukiwa na nafasi ya kutafuta tiketi ya kwenda fainali.

Kikosi cha Azam FC Dhidi ya Yanga Leo 21/06/2026 Kombe la CRDB

Kauli za Makocha Kabla ya Mchezo

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Abdihamid Moallin, alisema maandalizi yamekamilika kwa kiwango kikubwa na wachezaji wako katika morali ya juu. Hata hivyo, alikiri ugumu wa mchezo kutokana na aina ya mpinzani na ubora alionao.

“Malenho yetu ni kufanya vizuri katika mechi ya leo bila ya kuangalia siku tatu zijazo tutafanya nini dhidi yao, sio mechi rahisi kwa sababu kila tunapocheza na Azam inatupa ushindani mzuri jambo linalotupa motisha,” alisema Moallin.

Kwa upande wa Azam FC, Kocha Mkuu Florent Ibenge alisema ugumu wa mchezo huo unatokana na mahitaji ya kila timu na malengo yake. Pia alisema ushindi wa mechi sita mfululizo katika mashindano yote unawapa hamasa wachezaji wake kwa ajili ya kupambana.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Yanga VS Fountain Gate Leo 18/06/2026
  2. Yanga VS Fountain Gate Leo 18/06/2026 Saa Ngapi?
  3. Japan Waifundisha Dunia Somo la Usafi Kombe la Dunia
  4. Watatu Waitwa Mezani Namungo Wakati Timu Ikipigania Kubaki Ligi Kuu Bara
  5. Yanga yaitaka Azam FC New Amaan baada ya kukwama mpango wa CCM Kirumba
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo