Yanga VS Fountain Gate Leo 18/06/2026 Saa Ngapi?

Yanga VS Fountain Gate Leo 18/06/2026 Saa Ngapi?

Yanga itakuwa ugenini leo, Juni 18, 2026, dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha, saa 10:00 jioni.

Yanga VS Fountain Gate Leo 18/06/2026 Saa Ngapi?

Mchezo huo ni sehemu ya mwendelezo wa msako wa pointi tatu kwenye ligi, huku Yanga ikiingia uwanjani ikiwa kileleni mwa msimamo na ikiendelea kupambana kutetea ubingwa wake.

Yanga inaingia kwenye mechi hiyo ikiwa na pointi 63 baada ya kushinda michezo 19, kutoka sare sita na kupoteza mchezo mmoja katika mechi 26 ilizocheza.

Fountain Gate, ambayo itakuwa mwenyeji wa mchezo huo, ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 29. Timu hiyo imeshinda michezo nane, imetoka sare tano na kupoteza michezo 13, pia baada ya kucheza mechi 26.

Katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gate, matokeo yanayoipa kumbukumbu nzuri kabla ya kukutana tena leo Arusha.

Mbali na mchezo huo, mechi nyingine za Ligi Kuu Bara zitapigwa leo saa 10:00 jioni. JKT Tanzania itacheza dhidi ya Tanzania Prisons, huku Pamba Jiji ikiikaribisha Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Mchezo wa Kimkakati kwa Pande Zote

Kocha wa Fountain Gate, Fredy Felix ‘Minziro’, amesema timu yake inatambua ugumu wa mchezo huo, lakini itaingia uwanjani kwa nidhamu kubwa na kwa kuwaheshimu wapinzani wao.

“Malengo yetu ni kuhakikisha tunatoka nafasi zote za hatari kwa maana ya kuondoka kabisa kwenye mechi za Play-Off’, sio rahisi kwa sababu ya gepu dogo la pointi na washindani wetu, hivyo, bado tuna kazi kubwa ya kufanya,” alisema Minziro.

Kwa upande wa Yanga, Kaimu Kocha Mkuu Abdihamid Moallin amesema tofauti ya pointi kati yao na timu zilizo nyuma yao ni sababu inayowafanya waendelee kupambana kutimiza malengo ya msimu.

“Mechi zote zilizobaki kwa sasa ni ngumu kwa sababu ya mahitaji ya kila mmoja wetu, tunatambua tutakutana na mazingira ya aina hiyo, ila tumejipanga kuhakikisha malengo tuliyoweka tangu kuanza kwa msimu huu tunayatimiza,” alisema Moallin.

Umuhimu wa Mechi Hii

Kwa Yanga, mchezo huu una umuhimu mkubwa katika harakati za kutetea taji la Ligi Kuu Bara. Kikosi hicho kinaongoza ligi na kinahitaji kuendelea kukusanya pointi katika mechi zake zilizosalia.

Kwa Fountain Gate, mchezo huu ni sehemu ya mapambano ya kujiondoa kwenye nafasi za hatari na kuepuka presha ya mechi za Play-Off. Kauli ya Minziro inaonyesha kuwa timu hiyo inatambua ukubwa wa kazi iliyo mbele yao.

Yanga na Fountain Gate zinakutana leo katika mchezo unaobeba malengo tofauti kwa kila upande. Yanga inatafuta kuimarisha nafasi yake kileleni, huku Fountain Gate ikihitaji matokeo yatakayoiweka mbali zaidi na eneo la hatari.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Japan Waifundisha Dunia Somo la Usafi Kombe la Dunia
  2. Watatu Waitwa Mezani Namungo Wakati Timu Ikipigania Kubaki Ligi Kuu Bara
  3. Yanga yaitaka Azam FC New Amaan baada ya kukwama mpango wa CCM Kirumba
  4. Ratiba ya NBC Premier League Leo June 14, 2026
  5. Ratiba ya Ligi Kuu ya NBC Leo 13 June 2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo