Matokeo ya Mashujaa VS Yanga Sc Leo 13/06/2026
Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Mashujaa FC na Yanga SC unapigwa leo Juni 13, 2026 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, kuanzia saa 10:15 jioni.
Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa kileleni mwa msimamo kwa pointi 60, huku Mashujaa FC ikiwa nafasi ya 11 na pointi 27. Kwa Yanga, huu ni mchezo wa kuendeleza kasi yake katika mbio za kileleni; kwa Mashujaa, ni nafasi ya kutafuta matokeo chanya mbele ya mabingwa watetezi.
Matokeo ya Mashujaa vs Yanga SC Live
Matokeo na matukio ya mchezo wa Mashujaa FC dhidi ya Yanga SC yanapatikana kupitia live updates hapa:

Kikosi cha Yanga SC Dhidi ya Mashujaa FC
Yanga SC inaanza mchezo wa leo ikiwa na Diarra langoni, huku safu ya wachezaji wa ndani ikijumuisha Yao, Boka, Mwamnyeto na Bacca. Mwamnyeto ndiye nahodha wa kikosi cha kuanza.
| Namba | Mchezaji |
|---|---|
| 39 | Diarra |
| 21 | Yao |
| 23 | Boka |
| 3 | Mwamnyeto |
| 4 | Bacca |
| 38 | Abuya |
| 7 | Maxi |
| 27 | Mudathir |
| 29 | Dube |
| 20 | Okello |
| 10 | Pacome |
Benchi la Yanga SC: Masalanga, Hussein, Assink, Asanal, Damaro, Farid, Edmund, Nabil, SureBoy na Depu.
Mashujaa FC vs Yanga SC: Taarifa za Kabla ya Mchezo
Mchezo huu unaikutanisha Mashujaa FC na Yanga katika mazingira tofauti kwenye msimamo. Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 60 baada ya kucheza mechi 25, ikishinda 18, kutoka sare sita na kupoteza moja.
Mashujaa FC ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 27. Katika mechi 25 za msimu huu, imeshinda tano, kutoka sare 12 na kupoteza nane.
Yanga ina kumbukumbu nzuri dhidi ya Mashujaa FC kwenye mchezo wa raundi ya kwanza. Timu hizo zilipokutana Januari 19, 2026 kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Yanga ilishinda mabao 6-0.
Mabao ya mchezo huo yalifungwa na Mohamed Damaro, Duke Abuya, Prince Dube, Pacome Zouzoua, Mudathir Yahya na Laurindo Dilson Maria ‘Depu’.
Rekodi ya Mashujaa FC Dhidi ya Yanga
Mashujaa FC bado haijaifunga Yanga tangu ilipopanda Ligi Kuu Bara msimu wa 2023-2024. Timu hizo zimekutana mara tano, na Yanga imeshinda michezo yote.
Katika michezo hiyo mitano, Mashujaa imeruhusu mabao 17 na kufunga mabao matatu. Rekodi hiyo inaongeza uzito wa mchezo wa leo, hasa kwa upande wa wenyeji wanaohitaji kubadili mwenendo huo wakiwa nyumbani Kigoma.
Mwenendo wa Karibuni
Mashujaa FC inaingia kwenye mchezo huu ikiwa haijashinda mechi nne mfululizo za Ligi Kuu Bara. Katika kipindi hicho, imepoteza mechi mbili na kutoka sare mbili.
Ushindi wa mwisho wa Mashujaa ulikuwa Mei 4, 2026, ilipoifunga TRA United bao 1-0 ikiwa nyumbani.
Kwa upande wa Yanga, kikosi cha Kocha Abdihamid Moalin kinaingia kwenye mchezo huu kikihitaji kuendelea kuimarisha nafasi yake ya kwanza kwenye msimamo.
Mapendekezo ya Mhariri:
- PSG Mabingwa Tena UEFA Champions League Baada ya Ushindi wa Penalti Dhidi ya Arsenal
- Liverpool Yaachana na Arne Slot, Iraola Apewa Nafasi Kubwa Kumrithi
- Ratiba Ligi Kuu Bara 2026 Yawagawa Wadau Baada ya Msimu Kusogezwa Hadi Juni 30
- Ratiba ya Kombe la Dunia 2026: Mechi Zote, Tarehe, Viwanja na Makundi
- Yanga Yaiingilia Azam Dili la Winga Mkongo Henoc Molia




```







Leave a Reply