PSG Mabingwa Tena UEFA Champions League Baada ya Ushindi wa Penalti Dhidi ya Arsenal

PSG Mabingwa Tena UEFA Champions League Baada ya Ushindi wa Penalti Dhidi ya Arsenal

PSG mabingwa UEFA Champions League tena baada ya kuifunga Arsenal 4-3 kwa mikwaju ya penalti, kufuatia sare ya 1-1 katika fainali iliyochezwa Budapest.

Ushindi huo umeifanya Paris Saint-Germain kutetea taji lake la Ulaya kwa msimu wa pili mfululizo, huku penalti zikibeba hatima ya mchezo baada ya dakika 120 kushindwa kutoa mshindi.

PSG Mabingwa Tena UEFA Champions League Baada ya Ushindi wa Penalti Dhidi ya Arsenal

Arsenal Walianza Vizuri Kupitia Havertz

Arsenal ilianza mchezo kwa nguvu na kupata bao la mapema kupitia Kai Havertz dakika ya sita. Bao hilo liliipa Arsenal uongozi wa 1-0, huku safu yao ya ulinzi ikiendelea kuizuia PSG kwa muda mrefu.

PSG walimiliki mpira kwa kiasi kikubwa katika mchezo huo, lakini walikutana na ukuta mgumu wa Arsenal ambao ulifanya kazi kubwa kuwalinda dhidi ya mashambulizi mengi.

Kwa takwimu zilizopo, PSG walimiliki mpira kwa asilimia 75 dhidi ya 25 za Arsenal ndani ya dakika 120. Pia walipiga mashuti 21, huku Arsenal wakipiga mashuti 7.

Dembele Aisawazishia PSG kwa Penalti

PSG walipata nafasi ya kurudi mchezoni dakika ya 60 baada ya tukio lililomhusisha Cristhian Mosquera. Ousmane Dembele alichukua jukumu la kupiga penalti na kufunga bao la kusawazisha.

Bao hilo liliifanya fainali irudi kwenye usawa wa 1-1, na licha ya timu zote kuendelea kutafuta bao la ushindi, mchezo uliendelea hadi muda wa nyongeza.

Arsenal walikuwa na dai kubwa la penalti katika muda wa nyongeza, lakini halikukubaliwa. Baada ya hapo, fainali ikaenda kwenye mikwaju ya penalti.

PSG Waamua Mchezo kwa Penalti

Katika mikwaju ya penalti, PSG walikuwa na umakini zaidi na kuweza kuibuka na ushinda 4-3. Lucas Beraldo alifunga penalti ya maamuzi kwa upande wa PSG, kabla ya Gabriel Magalhaes kupiga juu penalti muhimu ya Arsenal.

Matokeo baada ya dakika 120PSG 1-1 Arsenal
Mshindi kwa penaltiPSG
Mikwaju ya penaltiPSG 4-3 Arsenal
Bao la ArsenalKai Havertz
Bao la PSGOusmane Dembele
Penalti ya maamuziLucas Beraldo
Penalti iliyokosaGabriel Magalhaes

Ushindi huo umeifanya PSG kubeba taji la UEFA Champions League kwa mara ya pili mfululizo. Pia ni taji lao la pili la Ulaya katika historia ya klabu.

Kwa PSG, huu ni mwisho mzuri wa msimu wa 2025/2026 baada ya pia kushinda Ligue 1. Ingawa hawakufanikiwa kutwaa treble kwa mara ya pili, wamemaliza msimu wakiwa na mataji mawili makubwa.

Kwa Arsenal, ilikuwa fainali iliyowapa nafasi kubwa baada ya kuongoza mapema, lakini mwisho wa mchezo uliamuliwa na penalti. Gabriel alikosa mkwaju muhimu, na PSG wakahitimisha usiku wao kwa ushindi mwingine wa Ulaya.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Kombe la Dunia 2026: Mechi Zote, Tarehe, Viwanja na Makundi
  2. Vitu vya Kwenda Navyo JKT Mujibu Wa Sheria 2026
  3. Yanga Yaiingilia Azam Dili la Winga Mkongo Henoc Molia
  4. Timu Za Afrika Zilizofuzu Kombe la Dunia 2026 na Nafasi Zao Kwenye Michuano
  5. Kundi la Tanzania Kufuzu AFCON 2027
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo