Matokeo ya Yanga vs Namungo leo 25/05/2026
Kikosi cha Yanga leo kitashuka dimbani kuzisaka pointi tatu muhimu dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC unaopigwa leo, Mei 25, 2026 kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.
Mchezo huu una umuhimu mkubwa kwa Yanga SC ambao wanahitaji ushindi ili kuendelea kujiweka vizuri kwenye mbio za kutetea ubingwa wa ligi. Kwa upande wa Namungo FC, dakika 90 za leo ni muhimu katika harakati za kujinasua na presha ya nafasi za chini kwenye msimamo.
Matokeo ya Yanga vs Namungo Leo Live
Hapa chini unaweza kufuatilia matokeo ya Yanga vs Namungo leo 25/05/2026 kupitia live updates za mchezo huu wa Ligi Kuu ya NBC.
Taarifa za Mchezo Yanga Vs Namungo Fc
| Mechi | Yanga SC vs Namungo FC |
| Tarehe | 25/05/2026 |
| Muda | Saa 12:30 jioni |
| Uwanja | KMC Complex |
| Mashindano | Ligi Kuu ya NBC |
Kikosi cha Yanga vs Namungo Leo
Yanga SC imeanza na Diarra langoni, akilindwa na safu ya ulinzi yenye Yao, Mwenda, Mwamnyeto na Bacca.
Eneo la kati lina Damaro, Maxi, Abuya na Mudathir, huku safu ya mbele ikiwa na Dube na Okello.
Kikosi cha Yanga Kinachoanza
| Namba | Mchezaji |
|---|---|
| 39 | Diarra |
| 21 | Yao |
| 33 | Mwenda |
| 3 | Mwamnyeto |
| 4 | Bacca |
| 25 | Damaro |
| 7 | Maxi |
| 38 | Abuya |
| 29 | Dube |
| 27 | Mudathir |
| 20 | Okello |
Benchi la Yanga: Masalanga, Kibwana, Assink, Abdulnasir, Kouma, Sheikhan, Edmund, SureBoy, Ally, Depu.
Yanga Kusaka Ushindi Muhimu KMC Complex
Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na pointi 57 kwenye ligi. Wananchi wanahitaji ushindi ili kurejea kwenye nafasi ya juu ya msimamo na kuendelea kubaki kwenye mbio za ubingwa.
Timu hiyo inatoka kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Singida BS, matokeo yaliyowarudisha kwenye njia ya ushindi kabla ya kukutana na Namungo.
Kocha wa muda wa Yanga, Abdihamid Moalin, alisema maandalizi ya mchezo huu yamekwenda vizuri na timu yake imejifunza kutokana na makosa ya nyuma.
“Kila mmoja anajua kilichotokea kwenye mechi yetu dhidi ya Dodoma Jiji, unazungumzia takwimu, haikuwa timu ambayo imewahi kutufunga (Dodoma), lakini ikafanikiwa kufanya hivyo, tumejifunza, tunaiheshimu Namungo ina kocha mzuri na wachezaji wazuri, tunachotaka ni kuendelea kushinda,” amesema Moalin.
Namungo Wanaingia na Presha ya Msimamo
Namungo FC ipo nafasi ya 12 kwenye msimamo ikiwa na pointi 25. Mchezo dhidi ya Yanga ni muhimu kwao kwa sababu matokeo mabaya yanaweza kuongeza presha kwenye vita ya kujinasua na eneo la hatari.
Namungo pia imekosa ushindi kwenye mechi 13 zilizopita, hali inayoufanya mchezo huu kuwa mtihani mkubwa kwa timu hiyo ya Lindi.
Kocha Mgunda alisema maandalizi yao yamekamilika na mchezo huu una umuhimu mkubwa kwa pande zote mbili.
“Mechi hii ni muhimu sana kwetu kutokana na nafasi tuliyopo kwenye msimamo lakini hata wapinzani wetu nao ni mechi muhimu kutokana na nafasi waliyonayo, itakuwa mechi yenye ushindani, maandalizi yetu yamekamilika tayari kwa mchezo huo,” amesema Mgunda.
Rekodi ya Yanga Dhidi ya Namungo
Yanga ina rekodi nzuri mbele ya Namungo. Timu hizi zimekutana mara 12, ambapo Yanga imeshinda michezo saba na kutoka sare tano.
Namungo haijawahi kuifunga Yanga kwenye michezo hiyo 12. Katika rekodi hiyo, Yanga imefunga mabao 20, huku Namungo ikifunga mabao saba.
Wachezaji wa Kuangalia
Kwa Yanga, Allan Okello ni mmoja wa wachezaji wanaotazamwa zaidi kutokana na kiwango chake cha sasa. Kiungo huyo wa Uganda amefunga mabao tisa na kutoa asisti saba, akiwa amehusika kwenye jumla ya mabao 16.
Pacome Zouzoua alikuwa kwenye uangalizi baada ya kupata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Singida BS, ingawa taarifa zilizopo zinaeleza kuwa majeraha yake hayakuwa makubwa.
Takwimu Muhimu Kabla ya Mchezo
- Yanga vs Namungo inapigwa saa 12:30 jioni.
- Uwanja ni KMC Complex, Dar es Salaam.
- Yanga ina pointi 57 kwenye ligi.
- Namungo ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 25.
- Yanga imeshinda mechi 7 kati ya 12 dhidi ya Namungo.
- Mechi 5 kati ya Yanga na Namungo zimeisha kwa sare.
- Namungo haijawahi kuifunga Yanga kwenye michezo hiyo 12.
- Allan Okello ana mabao 9 na asisti 7 kwenye ligi.
Mapendekezo ya Mhariri:







Leave a Reply