Simba vs TRA United Leo 17/05/2026 Saa Ngapi?
Wekundu wa Msimbazi Simba leo watakuwa dimbani kuisaka tiketi ya kufuzu nusu fainali ya Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup, ambapo watachuana vikali dhidi ya wabishi TRA United katika mtanange utakaotimua vumbi katika viunga vya dimba la KMC jijini Dar es Salaam.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa na mvuto mkubwa kutokana na historia ya timu hizi msimu huu, baada ya kukutana mara mbili kwenye ligi. Katika michezo hiyo, Simba ilishinda mara moja, huku mchezo wao wa mwisho uliopigwa ugenini mjini Arusha ukimalizika kwa sare ya bila kufungana.
Taarifa Muhimu za Mechi
| Kipengele | Maelezo |
| Mchezo | Simba SC vs TRA United |
| Mashindano | Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup |
| Hatua | Robo fainali |
| Uwanja | KMC, Dar es Salaam |
| Muda | Saa 12:30 jioni |
| Tarehe | 17/05/2026 |

Simba inaingia kwenye mchezo huu ikikumbuka ushindi wake wa mabao 3-0 dhidi ya TRA United mara ya mwisho ilipoikaribisha timu hiyo katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo. Hata hivyo, mazingira ya mchezo wa leo yanaonekana kuwa tofauti kwa sababu ni mechi ya mtoano, ambapo mshindi ataendelea na safari ya nusu fainali.
Kwa upande wa TRA United, macho ya wengi yanaelekezwa kwa winga Ramadhan Salum Chobwedo, ambaye anatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya changamoto kwa safu ya ulinzi ya Simba. Vita yake dhidi ya beki wa kushoto Nickson Kibabage inaweza kuwa moja ya maeneo yatakayobeba uzito mkubwa kwenye mchezo huu.
Mapambano ya Chobwedo na Kibabage
Mara ya mwisho Chobwedo na Kibabage walipokutana, kulikuwa na vita kubwa uwanjani. Chobwedo alimpa wakati mgumu Kibabage katika baadhi ya nyakati, ingawa pia kulikuwa na vipindi ambavyo beki huyo wa Simba alimzuia winga huyo kuleta madhara zaidi.
Hilo linafanya pambano lao la leo kupewa uzito mkubwa, hasa kwa sababu TRA United inaweza kutumia kasi na ubunifu wa Chobwedo kutengeneza nafasi, wakati Simba itahitaji nidhamu kubwa ya ulinzi ili kudhibiti mashambulizi kutoka pembeni.
Umuhimu wa Mchezo kwa Simba
Simba inahitaji ushindi ili kufuzu nusu fainali ya Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup. Kwa Wekundu wa Msimbazi, ushindi katika hatua hii utakuwa muhimu katika kuendeleza matumaini ya kutinga fainali na kuwania ubingwa wa michuano hiyo.
Klabu hiyo ina rekodi ya kubeba Kombe la Shirikisho mara nne, huku taji lake la mwisho likiwa msimu wa 2020-2021 ilipoifunga Yanga bao 1-0. Tangu wakati huo, Simba haijafanikiwa kulibeba tena taji hilo kwa misimu minne.
Mchezo wa leo kati ya Simba na TRA United unatarajiwa kuwa kipimo muhimu kwa pande zote mbili. Simba inatafuta tiketi ya nusu fainali, wakati TRA United itaingia uwanjani ikihitaji kuendeleza ushindani wake dhidi ya moja ya timu kubwa nchini.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Timu Zilizofuzu Nusu Fainali CRDB Federation Cup 2026
- Matokeo ya JKT Tanzania VS Yanga Leo 16/05/2026
- Matokeo ya Coastal Union vs Singida Bs Leo 16/05/2026
- Azam TV Kuonesha Mechi Zote 104 za Kombe la Dunia 2026 Mbashara
- Matokeo ya Simba Queens vs Yanga Princess Leo 15/05/2026






Leave a Reply