Vituo vya Usaili Ajira Serikalini Aprili 2026 – Orodha Kamili Kutoka Sekretarieti ya Ajira

Vituo vya Usaili Ajira Serikalini Aprili 2026 – Orodha Kamili Kutoka Sekretarieti ya Ajira

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetangaza rasmi vituo vya usaili wa mahojiano kwa waombaji wa ajira serikalini vinavyotarajiwa kutumika mwezi Aprili 2026. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia mikoa waliyopangiwa kufanya usaili huo kama ilivyoainishwa kwenye tangazo rasmi.

Taarifa hii inaweka wazi mgawanyo wa vituo vya usaili kwa kila mkoa, hatua ambayo inalenga kuhakikisha wasailiwa wanapata mwongozo sahihi wa mahali pa kufanyia mahojiano yao. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kila msailiwa anatakiwa kufika katika kituo kilichopangwa kulingana na mkoa wake.

Ifuatayo ni orodha kamili ya vituo vya usaili ajira serikalini Aprili 2026 kama ilivyotolewa rasmi:

Vituo vya Usaili Ajira Serikalini Aprili 2026 - Orodha Kamili Kutoka Sekretarieti ya Ajira

Orodha ya Vituo vya Usaili Ajira Serikalini Aprili 2026

Na.MkoaKituo cha Usaili
1ArushaChuo cha Uhasibu Arusha (IAA)
2Dar es SalaamOfisi ya Mkurugenzi, Manispaa ya Kigamboni
3DodomaOfisi za Sekretarieti ya Ajira – Tambukareli
4GeitaShule ya Sekondari ya Wasichana Nyankumbu
5IringaChuo cha Ualimu Kleruu
6KageraShule ya Sekondari ya Ihungo
7KataviShule ya Sekondari ya Wasichana Mpanda
8KigomaShule ya Sekondari ya Kigoma
9KilimanjaroChuo cha Ushirika Moshi (MoCU)
10LindiShule ya Sekondari ya Wama-Sharaf
11ManyaraChuo cha Uhasibu Arusha (IAA) – Manyara Kampasi ya Zamani
12MaraChuo cha Maendeleo ya Jamii – Buhare
13MbeyaChuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)
14MorogoroChuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) – Dkt Samia Complex
15MtwaraChuo cha Sayansi na Teknolojia – Kampasi ya Mtwara
16MwanzaShule ya Sekondari ya Alliance
17NjombeShule ya Sekondari ya Njombe
18PwaniWIPAHS – Kibaha
19RukwaChuo cha VETA Rukwa – Kata ya Momoka Kashayi
20RuvumaChuo cha Ualimu Songea
21SimiyuShule ya Sekondari ya Simiyu
22ShinyangaChuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM)
23SingidaShule ya Sekondari ya Mwenge
24SongweShule ya Sekondari ya Vwawa
25TaboraChuo cha Uhazili – TPSC
26TangaShule ya Sekondari Galanos
27PembaOfisi za Vyuo vya Amali – Vitongoji Chakechake Pemba
28UngujaJengo la Katiba na Sheria – Mazizini, Ghorofa ya Tatu

Taarifa hii imetolewa tarehe 08 Aprili 2026 na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Lynn Chawala, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchakato wa usaili kwa waombaji wa ajira katika utumishi wa umma.

Wasailiwa wote wanahimizwa kufika katika vituo walivyopangiwa kwa kuzingatia mikoa yao ili kuhakikisha mchakato wa usaili unakwenda kwa utaratibu uliopangwa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Tano 2026/2027
  2. Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Tano 2026
  3. Majina ya Waliochaguliwa Vyuo Vya Kati 2026/2027 | Selection Vyuo Vya Kati
  4. Ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi 2026
  5. Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga Vyuo Vya VETA Januari 2026 Awamu ya Pili
  6. Viwango Vya Mishahara ya Walimu 2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo