Vilabu Bora Afrika 2025 (CAF Club Ranking 2025)

Vilabu Bora Afrika 2025 (CAF Club Ranking 2025) | Rank za CAF 2025

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limetangaza rasmi orodha ya vilabu bora barani Afrika kwa mwaka 2025, ikionesha mwelekeo wa nguvu za soka la vilabu katika bara hili. Orodha hii, inayojulikana kama CAF Club Ranking 2025, hutolewa kila mwaka kwa kuzingatia mafanikio ya vilabu katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) na yae ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) katika misimu ya hivi karibuni.

Kwa mwaka huu, matokeo haya yametolewa muda mfupi kabla ya droo za awamu za awali za michuano ya TotalEnergies CAF Champions League na TotalEnergies CAF Confederation Cup msimu wa 2025/26, droo ambazo zitafanyika jijini Dar es Salaam. Viwango hivi hutumika kupanga vikapu vya droo, hivyo nafasi ya klabu katika orodha hii ni muhimu kwa mpangilio wa mechi na uwezekano wa kufuzu hatua za juu.

Al Ahly FC kutoka Misri imeendelea kushikilia nafasi ya kwanza kwa alama 78, ikithibitisha ubabe wake barani Afrika baada ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika mara nne katika misimu sita iliyopita. Nafasi ya pili inashikiliwa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini (62 pointi), ambayo imejijengea sifa kama nguvu kubwa Kusini mwa Afrika.

Espérance Sportive de Tunis ya Tunisia imeibuka ya tatu kwa alama 57, ikidumisha utawala wa vilabu vya Kaskazini mwa Afrika katika mashindano ya CAF. RS Berkane ya Morocco (52 pointi), mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita, wamefuatia katika nafasi ya nne, huku nafasi ya tano ikishikiliwa na Simba SC ya Tanzania (48 pointi), ambayo imekuwa klabu bora zaidi kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki.

Orodha ya Vilabu Bora Afrika 2025 (CAF Club Ranking 2025) | Rank za CAF 2025

RankJina la Klabu
1Al Ahly FC
2Mamelodi Sundowns
3Espérance Sportive de Tunis
4RS Berkane
5Simba SC
6Pyramids FC
7Zamalek SC
8Wydad AC
9USM Alger
10CR Belouizdad
11Al Hilal SC
12Young Africans
13ASEC Mimosas
14TP Mazembe
15Orlando Pirates
16Raja CA
17Atletico Petroleos
18AS FAR
19MC Alger
20GD Sagrada Esperança
21CS Constantine
22Stellenbosch FC
23Al Masry SC
24Rivers United FC
25JS Kabylie
26Dreams FC
27Stade Malien
28Horoya AC
29Future FC
30Etoile SS
31Marumo Gallants FC
32E.S. Setif
33FC Nouadhibou
34Abu Salim SC
35Enyimba FC
36ASC Jaraaf
37Coton Sport FC de Garoua
38CS Sfaxien
39Jwaneng Galaxy FC
40US Monastirienne
41Al Merrikh SC
42Al Ahli Tripoli
43CD Lunda-Sul
44FC Bravos do Maquis
45Stade d’Abidjan
46Djoliba AC de Bamako
47AS Maniema Union
48CSMD Diables Noirs
49AS Vita Club
50Kaizer Chiefs FC
51Medeama SC
52Al Hilal Benghazi
53Sekhukhune United FC
54Club Africain
55Al Ittihad
56AmaZulu FC
57FC St Eloi Lupopo
58AS Real de Bamako
59ASKO de Kara
60Vipers SC
61Orapa United
62Associação Black Bulls
63A.P.C. de Lobito
64S.O.A.R.
65SuperSport United FC
66JS Saoura
67AS Otohô
68DC Motema Pembe
69Al Akhder
70Royal Leopards FC
71US Gendarmerie Nationale
72Zanaco FC
73Teungueth FC
74Nkana FC
75Salitas FC
76Ahli Benghazi
77Namungo FC
78Napsa Stars FC

Vilabu Bora Afrika 2025 (CAF Club Ranking 2025)

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Mshahara wa Celestin Ecua Yanga 2025/2026
  2. Msimamo Kundi la Tanzania CHAN 2024
  3. Mohamed Hussein Shabalala Ajiunga na Yanga SC Baada ya Miaka 11 Simba
  4. Ratiba ya CHAN 2025 Mechi za Makundi
  5. Orodha ya Wachezaji Wazawa Yanga Sc 2025/2026
  6. CV Ya Mohamed Doumbia Kiungo Mpya wa Yanga 2025/2026
  7. Cv ya Mohammed Bajaber Kiungo Mshambuliaji Mpya Simba Sc 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo