Matokeo Ya Yanga vs Dodoma Jiji Leo 13/052026

Matokeo Ya Yanga vs Dodoma Jiji Leo 13/052026

Yanga SC leo inaingia uwanjani ugenini kuvaana na Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu Bara wenye umuhimu mkubwa kwa pande zote mbili.

Mabingwa hao watetezi wanatafuta ushindi ili kujiweka salama kwenye mbio za kuusaka ubingwa, huku Dodoma Jiji ikihitaji pointi tatu ili kupanda kutoka nafasi ya nane hadi ya saba.

Yanga inaongozwa na kocha wa muda Abdihamid Moalin, ambaye anakuwa kwenye mchezo wake wa pili wa ligi akiwa na jukumu la kuendeleza mwendo wa ushindi kwenye Uwanja wa Airtel, Singida.

Dodoma Jiji inacheza mchezo huu ikiwa na pointi 29. Ushindi unaweza kuifanya ifikishe pointi 32 na kupanda nafasi moja kwenye msimamo.

Kwa upande wa Yanga, kikosi kilichotangazwa kinaanza na Djigui Diarra langoni, huku safu ya ulinzi ikiwa na Yao, Duka, Mwamnyeto na Bacca. Eneo la kiungo lina Abuya, Maxi na Mudathir, wakati safu ya ushambuliaji imeundwa na Prince Dube, Allan Okello na Pacome.

Wachezaji wa akiba ni Masalanga, Abubakar, Kibwana, Assink, Hussein, Abdulnasir, Damaro, Sheikhan, Buba na Depu.

Yanga inakutana na Dodoma ikiwa na rekodi nzuri katika mechi 11 walizokutana kwenye ligi, ambapo Dodoma haijapata hata sare dhidi ya mabingwa hao watetezi.

Katika mechi tano za mwisho, Yanga imeangusha pointi mbili pekee baada ya kutoka sare ugenini dhidi ya Simba, kabla ya kushinda michezo minne iliyofuata.

Habari nyingine muhimu kwa Yanga ni kurejea kwa kiungo Mudathir Yahaya, aliyemaliza adhabu ya kusimamishwa mechi tatu na kamati ya usimamizi wa ligi. Beki wa kushoto Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ pia amerejea baada ya kuumia akiwa Zanzibar kwenye mechi za Kombe la Muungano.

Matokeo Ya Yanga vs Dodoma Jiji Leo 13/052026

Kikosi cha Yanga na Hesabu za Mchezo

Kocha Abdihamid Moalin amesema mchezo huo hautakuwa rahisi, akisisitiza kuwa Dodoma imekuwa ikitoa ushindani kila inapokutana na Yanga.

“Utakumbuka kwenye mchezo wa kwanza tukiwa nyumbani walianza kutufunga lakini tulikuwa imara tukasawazisha na kushinda, Dodoma ni timu nzuri hutakiwi kwenda kukutanan nayo ukiona kama itakuwa mechi rahisi,” amesema Moalin.

Moalin ameongeza kuwa Yanga inahitaji kucheza kwa ubora mkubwa kwa kuwa kipindi hiki si salama kuangusha pointi.

“Tunataka kucheza kwa ubora mkubwa, wakati kama huu sio salama sana kuangusha pointi, hatutaki kitu kama hicho kitokee, tumesafiri na wachezaji wote muhimu na wako sawasawa, tupo tayari kwa mchezo.”

Dodoma Jiji italazimika kuwa makini na Prince Dube, ambaye ndiye kinara wa mabao ndani ya kikosi cha Yanga akiwa na mabao tisa. Allan Okello pia ni mchezaji muhimu kwa mabingwa hao, akiwa kinara wa pasi za mwisho kikosini hapo kwa pasi saba.

Kwa upande wa Dodoma, mshambuliaji William Edgar ndiye mchezaji anayebeba matumaini makubwa kwenye safu ya ushambuliaji. Edgar ana mabao sita na ndiye aliyemtungua kipa Djigui Diarra katika mchezo wa mwisho uliowakutanisha na Yanga, ambao mabingwa hao walishinda 3-1.

Fuatilia Hapa Matokeo Ya Yanga vs Dodoma Jiji Leo 13/052026 Live

Umuhimu wa Mchezo kwa Pande Zote

Mchezo huu una uzito mkubwa kwa Yanga kutokana na hesabu za kuendelea kukimbiza taji la tano mfululizo. Timu hiyo inahitaji ushindi ili kubaki imara katika mbio za ubingwa.

Dodoma nayo inaingia kwenye mchezo huu ikihitaji kuboresha nafasi yake kwenye msimamo. Changamoto kubwa kwa wenyeji hao ni safu ya ulinzi, baada ya kuruhusu mabao 21 huku wakifunga 19.

Kocha wa Dodoma, Amani Josiah, amesema wanatambua ugumu wa mchezo lakini wanataka kutumia makosa ya Yanga kutafuta pointi.

“Tunakwenda kwenye mchezo mgumu, mara ya mwisho tulipokutana kwao, tuliwabana vizuri lakini baadaye tulipopata bao kina makosa tulitafanya yakatugharimu na kupoteza mchezo, Yanga ni wazuri wana wachezaji wenye uzoefu lakini haina maana kwamba haifanyi makosa, tutakwenda kutumia makosa yao,” amesema Josiah.

Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na kikosi chenye majina muhimu katika kila eneo, huku Dodoma ikihitaji nidhamu kubwa ya ulinzi na ufanisi mbele ya lango ili kubadili historia yake dhidi ya mabingwa hao watetezi.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo wa EPL Leo 10/05/2026 Ligi Kuu ya Uingereza
  2. Msimamo wa Ligi Kuu Ya NBC 10 Mei 2026 Baada ya Mechi za Leo
  3. Matokeo ya Simba VS Tanzania Prisons Leo 10/05/2026
  4. Kikosi cha Simba VS Tanzania Prisons Leo 10/05/2026
  5. Washindi wa Tuzo Za BMT 2026
  6. Rekodi Nne za Azam FC Zavunjwa na TRA United Baada ya Kipigo cha 4-1
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo