Matokeo ya Simba VS Yanga Leo 03 May 2026
Dar es Salaam, Tanzania — Wekundu wa Msimbazi Simba Sc leo wanakutana na Yanga Sc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC ambao umekua ukisubiriwa baada ya vita ya waasimu hawa wawili kumalizwa katika dakika za jioni kabisa katika fainali ya kombe la Mapinduzi ambapo Simba iliibuka kidedea baada ya ushindi mwembamba wa goili 1-0 lililopatikana dakika ya 123 kupitia mkwaju wa penati.
Mchezo huu wa leo unatoa nafasi kwa Simba kuwaziba midomo washindani wao ambao wanaona wamebahatishwa kufungwa katika mchezo wa fainali ya mapinduzi au Yanga kudhihirisha kuwa ni kweli waliahatishwa.
Katika muktadha huo, Matokeo ya Simba VS Yanga Leo 03 May 2026 yana nafasi ya kuathiri msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025–2026, huku timu zote zikihitaji matokeo chanya.
Fuatilia Hapa Matokeo ya Simba VS Yanga Leo 03 May 2026
| SIMBA SC | 2-1 | YANGA SC |
- 🏆 #nbcpremierleague
- Simba SC🆚 Yanga Sc
- 🗓️ 03 May 2026
- 🏟️ Isamuhyo
- ⏱️ 18:00 Jioni
Simba na Yanga katika ushindani wa moja kwa moja
Mchezo huo utachezwa leo Jumapili, Mei 3, 2026, katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo jijini Dar es Salaam, ukiwa ni raundi ya pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Hii ni mara ya nne kwa Simba Sports Club na Young Africans Sports Club kukutana msimu huu, kila timu ikiwa imeshinda mara moja na nyingine kumalizika kwa sare.
Yanga inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 47, huku Simba ikiwa na pointi 42. Hivyo, Matokeo ya Simba VS Yanga Leo 03 May 2026 yanaweza kubadili tofauti ya pointi kati ya timu hizo.
Simba inaingia kwenye mchezo huo ikiwa mwenyeji na ikihitaji ushindi ili kupunguza pengo hilo. Sare au kupoteza kutaiweka Yanga katika nafasi nzuri zaidi ya kuendelea kuongoza ligi.
Kwa upande wa kikosi, Simba inaendelea kufuatilia hali ya winga Anicet Oura aliyepata majeraha ya misuli ya paja katika fainali ya Kombe la Muungano, huku beki Ismael Toure akitajwa kuwa tayari kucheza.
Yanga na rekodi ya kutopoteza ligi
Young Africans SC iliendelea na maandalizi yake Zanzibar kabla ya kurejea Dar es Salaam. Katika mchezo huu itawakosa Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kutokana na majeraha pamoja na Mudathir Yahya anayekosa kutokana na adhabu.
Chadrack Boka anatarajiwa kuanza upande wa kushoto huku Duke Abuya akitarajiwa kuanza katika eneo la kiungo wa kati.
Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa haijapoteza mechi yoyote ya Ligi Kuu tangu Novemba 7, 2024, ikiwa imecheza mechi 39 bila kupoteza. Rekodi za mwezi Mei zinaonyesha imekuwa na matokeo mazuri dhidi ya Simba, ikiwa imeshinda mechi tatu kati ya saba zilizochezwa mwezi huo tangu mwaka 1965.
Kwa upande wa mechi za Jumapili, Simba inaongoza kwa ushindi tisa dhidi ya saba za Yanga katika jumla ya mechi 37 zilizochezwa siku hiyo.
Mapendekezo ya Mhariri:







Leave a Reply