Kikosi cha Yanga Vs Simba Leo 03 May 2026
Dabi ya Kariakoo inapigwa leo Jumapili katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo jijini Dar es Salaam, ambapo Simba itakuwa mwenyeji wa Yanga. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na nafasi ya timu hizi katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Taarifa za Mchezo
- ๐ย #nbcpremierleague
- ๐ Simba SC
- ๐๏ธ 03 May 2026
- ๐๏ธ Isamuhyo
- โฑ๏ธ 18:00 Jioni
Wakati mashabiki wakisubiri kuanoa Kikosi cha Yanga Vs Simba Leo 03 May 2026 ambacho kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 11 jioni dakika kadhaa kabla ya mtanange kuanza, tayari presha ya mchezo imeongezeka kutokana na umuhimu wake katika msimamo wa ligi. Yanga inaongoza kwa pointi 47, huku Simba ikiwa nafasi ya pili na pointi 42, hali inayofanya ushindi kuwa muhimu kwa kila upande.
Hii ni mara ya nne kwa timu hizi kukutana msimu huu. Kila timu imeshinda mchezo mmoja, huku mwingine ukiisha kwa sare. Katika mechi ya mwisho, Simba ilishinda bao 1-0 katika fainali ya Kombe la Muungano, matokeo yanayoipa timu hiyo maandalizi mazuri kuelekea mchezo wa leo.
Hiki Apa Kikosi cha Yanga Vs Simba Leo 03 May 2026
- 39 Diarra
- 33 Mwenda
- 23 Boka
- 3 Mwamnyeto (C)
- 4 Bacca
- 25 Damaro
- 7 Maxi
- 38 Abuya
- 29 Dube
- 20 Okello
- 10 Pacome
Kwenye Benchi: Mshery, Abubakar, Yao, Assinki, Abdulnassir, Andabwile, Sureboy, Mwanengo, Sheikhan, Depu
Kwa upande wa Simba, maandalizi yamekamilika huku baadhi ya wachezaji waliocheza fainali wakirejeshwa mapema Dar es Salaam kwa ajili ya mapumziko. Hata hivyo, kuna ufuatiliaji wa hali za kiafya kwa baadhi ya wachezaji, akiwemo Anicet Oura aliyepata tatizo la misuli ya paja pamoja na beki Ismael Toure ambaye alimaliza mchezo uliopita akiwa na maumivu, lakini anatajwa kuwa tayari kucheza.
Yanga imefanya maandalizi yake Zanzibar kabla ya kurejea Dar es Salaam. Kikosi hicho kitawakosa Mohammed Hussein โTshabalalaโ kutokana na majeraha na Mudathir Yahya anayekitumikia adhabu ya kufungiwa. Chadrack Boka anatarajiwa kuendelea kucheza upande wa kushoto, huku Duke Abuya akitarajiwa kuanza katika safu ya kiungo.
Katika eneo la kiufundi, makocha wa timu zote mbili wametambua ushindani uliopo katika mchezo huu. Simba inalenga kutumia uwanja wa nyumbani kupata matokeo chanya, wakati Yanga inalenga kuendeleza mwenendo wake wa kutopoteza mechi za ligi msimu huu.
Katika Kikosi cha Yanga Vs Simba Leo 03 May 2026, kiungo mshambuliaji Allan Okello anatajwa kuwa mchezaji muhimu kwa upande wa Yanga. Ameonyesha kiwango kizuri katika mechi za hivi karibuni, hasa katika ubunifu wa mashambulizi na utoaji wa pasi za mwisho, akiwa na asisti sita katika mechi 13 za ligi.
Okello hupendelea kucheza kati ya mistari ya viungo na mabeki, jambo linalolazimisha wapinzani kufanya maamuzi ya haraka. Pia ana uwezo wa kupiga mashuti ya mbali na kufanya maamuzi kwa haraka, hali inayoweza kuathiri mpangilio wa safu ya ulinzi ya Simba.
Kwa upande wa Simba, mbinu za kumdhibiti Okello zinatarajiwa kujumuisha ulinzi wa karibu na kuzuia mawasiliano kati yake na washambuliaji wa Yanga. Hata hivyo, hatua hiyo inaweza kufungua nafasi kwa viungo wengine wa Yanga kama Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli.
Mapendekezo ya Mhariri:







Leave a Reply