Kikosi cha Yanga Princess vs Simba Queens Leo 15/05/2026

Kikosi cha Yanga Princess vs Simba Queens Leo 15/05/2026

Yanga Princess na Simba Queens zinakutana leo katika mchezo mkubwa wa Ligi ya Wanawake Tanzania utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, kuanzia saa 11 jioni.

Dabi hii inakuja ikiwa na uzito mkubwa kwenye mbio za ubingwa, huku Simba Queens ikiwa kileleni mwa msimamo na Yanga Princess ikishika nafasi ya pili. Tofauti ya pointi nne kati ya timu hizo mbili inaifanya mechi ya leo kuwa moja ya michezo muhimu zaidi katika mzunguko wa 16 wa ligi.

Simba Queens inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na pointi 43 baada ya kucheza mechi 15. Timu hiyo imeshinda mechi 14 na kutoka sare moja, ikiwa bado haijapoteza mchezo msimu huu.

Yanga Princess ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 39 baada ya idadi hiyo hiyo ya michezo. Ushindi kwa Yanga Princess leo utaifanya ifikishe pointi 42 na kupunguza tofauti dhidi ya Simba Queens hadi pointi moja.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, Yanga Princess ikiwa mwenyeji ilipoteza kwa mabao 2-0. Mabao ya Simba Queens yalifungwa na Jentrix Shikangwa na Aisha Mnunka.

Kikosi cha Yanga Princess vs Simba Queens Leo 15/05/2026

Kikosi cha Yanga Princess vs Simba Queens Leo 15/05/2026

Kikosi cha Yanga Princess kitakachoanza dhidi ya Simba Queens leo kinatarajiwa kutangazwa na benchi la ufundi muda mchache kabla ya mchezo kuanza saa 11 jioni katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Mashabiki wanatarajia kuona Yanga Princess ikiingia uwanjani kwa tahadhari kubwa, ikijua kuwa mchezo huu una maana kubwa kwenye mbio za ubingwa na nafasi yake katika msimamo wa ligi.

Kwa upande wa Simba Queens, kikosi kitakachoanza pia kitasubiriwa kwa hamu kutokana na rekodi nzuri ya timu hiyo msimu huu. Simba Queens haijapoteza mchezo katika mechi 15 ilizocheza, na imekuwa na safu imara ya ulinzi baada ya kuruhusu mabao mawili pekee.

Hiki Apa Kikosi cha Yanga Princess vs Simba Queens

  • Akarekor
  • Jeannine
  • Aregash
  • Wincate
  • Akudo
  • Precious
  • Agness
  • Igwe ©
  • Mabanza
  • A. Djafari
  • Nabbosa

Subs: Ester, Angela, Silvia, My Naco, Akoth, Diana, Y. Samuel, Zubeda, Kisisa.

Yanga Princess Yahitaji Ushindi Kupunguza Pengo

Yanga Princess inaingia kwenye dabi hii ikifahamu kuwa matokeo ya leo yanaweza kubadilisha mwelekeo wa mbio za ubingwa. Ikiibuka na ushindi, itafikisha pointi 42 na kuiacha Simba Queens ikiwa mbele kwa pointi moja pekee.

Hata hivyo, kupoteza kwa Yanga Princess kunaweza kuipa Simba Queens nafasi kubwa zaidi ya kujiimarisha kileleni. Pia kuna presha kutoka kwa JKT Queens, iliyo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 38, pointi moja nyuma ya Yanga Princess.

Kwa maana hiyo, Yanga Princess inahitaji matokeo mazuri si tu kupunguza pengo dhidi ya Simba Queens, bali pia kulinda nafasi yake ya pili kwenye msimamo.

Rekodi ya Simba Queens Dhidi ya Yanga Princess

Tangu mwaka 2019, Simba Queens na Yanga Princess zimekutana mara 18 kwenye mashindano mbalimbali, ikiwemo Ngao ya Jamii. Katika michezo hiyo, Simba Queens imeshinda mara 12, Yanga Princess mara tatu, huku mechi tatu zikimalizika kwa sare.

Kwenye ligi, timu hizo zimekutana mara 14. Simba Queens imeshinda mara 10, sare mbili na kupoteza mara mbili. Yanga Princess imeshinda mara mbili, imetoka sare mbili na kupoteza mara mbili.

Takwimu hizo zinaipa Simba Queens nguvu ya kisaikolojia kabla ya mchezo, lakini dabi ya aina hii mara nyingi huamuliwa na nidhamu, mbinu, ari na uwezo wa kutumia nafasi zinazopatikana.

Vita ya Makocha na Safu za Ushambuliaji

Mchezo huu pia unatazamwa kama pambano la kiufundi kati ya Edna Lema wa Yanga Princess na Mussa Hassan ‘Mgosi’ wa Simba Queens.

Edna Lema hataiongoza Yanga Princess akiwa benchi kutokana na adhabu ya kadi nyekundu aliyopata katika mechi iliyopita. Hata hivyo, maandalizi yake, falsafa yake na maelekezo yake yataendelea kuwa sehemu muhimu ya mpango wa Yanga Princess.

Katika safu ya ushambuliaji, Yanga Princess inamtegemea Jeannine Mukandayisenga, ambaye ndiye kinara wa mabao akiwa na 19. Kwa upande wa Simba Queens, Jentrix Shikangwa ni mchezaji muhimu kwenye eneo la ushambuliaji akiwa na mabao 12.

Yanga Princess imefunga mabao 44, idadi inayoonyesha uwezo wake wa kushambulia. Hata hivyo, timu hiyo imeruhusu mabao 13, wakati Simba Queens imeruhusu mabao mawili pekee katika mechi 15.

Kauli za Wachezaji Kabla ya Mchezo

Mshambuliaji wa Simba Queens, Aisha Mnunka, amesema mchezo huo ni mkubwa na kila upande umejiandaa kwa namna yake.

“Ni mechi kubwa kila mmoja amejiandaa kwa namna yake sisi tumejiandaa vizuri kwa ajili ya pointi tatu laakni siwezi kumzungumzia zaidi mpinzani yote kwa yote itaenda kujulikana nani mshindi na itaenda kutupa tasiwira nzuri,” alisema Mnunka.

Kwa upande wa Yanga Princess, kiungo Agnes Pallangyo amesema dabi haiamuliwi na mbinu pekee, bali pia kujitoa kwa wachezaji.

“Naamini kila mchezaji ana morali na anatamani kushinda mechi kwa sababu ni mechi ya maamuzi, mbinu pekee hazitoshi kwa sababu muda mwingine inaweza kukubalia au kukataa ikikataa jitihada zetu zitaamua.”

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo wa Ligi Kuu Wanawake Tanzania (TWPL) 2025/2026
  2. Robo fainali CRDB Bank Federation Cup 2025/2026
  3. Simba Queens VS Yanga Princess Leo 15/05/2026 Saa Ngapi?
  4. Kikosi cha Azam vs Pamba Jiji Leo 14/05/2026
  5. Msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Baada ya Mechi za Leo Mei 14, 2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo