Kikosi Cha Simba Vs APR 03 Agosti 2024 – Simba Day

Kikosi Cha Simba Vs APR 03 Agosti 2024 – Simba Day | Kikosi cha Simba Dhidi ya APR Mechi ya Kirafiki

Klabu ya Simba SC itakutana na APR ya Rwanda katika mchezo wa kirafiki kesho, 03 Agosti, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo kutakuwa na hafla ya kusherekea Simba Day 2024. Huu ni mchezo unaotarajiwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa Simba, kwani ni fursa ya kwanza kuona kikosi kipya kilichosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao.

Kocha wa Simba, Fadlu Davids, ametamba kuwa baada ya wiki sita za maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya, timu yake itakuwa moto wa kuotea mbali. Simba SC imerejea nchini baada ya kuweka kambi ya wiki tatu mjini Ismailia, Misri, ambako walicheza mechi tatu za kujipima nguvu na kushinda zote. Matokeo ya mechi hizo za kirafiki nchini Misri ni ushindi wa 3-0 dhidi ya El-Qanah, na ushindi wa 2-1 mara mbili dhidi ya Telecom Egypt na Al-Adalah FC ya Saudi Arabia.

Kocha Davids amesema usajili wa wachezaji 14 wapya pamoja na wachezaji 14 waliokuwepo umekamilisha kikosi chenye nguvu na nishati. Wachezaji wapya wameonyesha uelewa wa haraka wa mafunzo na mbinu zinazohitajika, jambo ambalo limeongeza ubora wa kikosi.

Kocha Fadlu Davids pia ameweka wazi kuwa maandalizi ya kikosi ni mchanganyiko wa mazoezi ya kimwili na mbinu za kiufundi.

“Mimi ni kocha ambaye siwezi kutofautisha ufiti na mbinu. Hivyo kuanzia siku ya kwanza tulianza kufanyia kazi maandalizi ya kimbinu na jinsi gani tunacheza,” alisema Fadlu.

Kocha huyo anatarajia kuona wachezaji wakiwa na staili ya kiuchezaji inayotakiwa kufikia mwisho wa mapumziko ya FIFA, na kuongeza kuwa kikosi chake kitakuwa na ushirikiano mzuri na mzunguko kamili wa maandalizi ya kimwili na ya kiufundi.

Kikosi Cha Simba Vs APR 03 Agosti 2024 – Simba Day

Hiki apa kikosi cha Simba dhidi ya APR kilichotangazwa

  • Salim
  • Kapombe
  • Hussein (C)
  • Che Malone
  • Chamou
  • Ngoma
  • Mutale
  • Mzamiru
  • Mukwala
  • Ahoua
  • Awesu

Wachezaji wa Ziada; Hussein, Camara, Hamza, Kijili, Duchu, Kazi, Nouma, Omary, Fernandez, Okeejepha, Karabaka, Chasambi, Baluu, Mashaka & Kibu

Hiki apa Kikosi Cha Simba Vs APR 03 Agosti 2024 - Simba Day

Kikosi Cha APR leo Dhidi ya Simba Sc 03 Agosti 2024 – Simba Day

  • Paveh N (30)
  • Niyomugabo C (C) (03)
  • Niyigena C (13)
  • Nshimiyimana Y (28)
  • Byiringiro G (18)
  • Mugisha G (11)
  • Taddeo L (14)
  • Dauda Y (25)
  • Ruboneka B (27)
  • Lamine B (14)
  • Victor M (29)

Wachezaji wa Akiba; Ishimwe P, Kategaya E, Ndayishimiye D, Niyibizi R, Dushimimana O, Mugiraneza F, Lamptey R, Alioum S, Tuyisenge A, Godwin, Chidiebere & Mamadou Sy

Kikosi Cha APR leo Dhidi ya Simba Sc 03 Agosti 2024 - Simba Day

Kikosi Cha Simba Vs APR 03 Agosti 2024 - Simba Day

Simba Day 2024

Simba Day ni tamasha maalum kwa klabu ya Simba kutambulisha kikosi cha msimu mpya pamoja na benchi la ufundi. Tamasha hili litanguliwa na burudani mbalimbali ikiwemo muziki, na kisha kufuatiwa na mechi ya kirafiki dhidi ya APR ya Rwanda. Kocha Davids amesema kuwa mchezo huu una malengo mawili: kuangalia maendeleo ya kiufundi ya kikosi na kufurahisha mashabiki wa Simba.

Mara baada ya tamasha la Simba Day, kikosi cha Simba kitarejea kambini kujiandaa na mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC, utakaofanyika Agosti 8 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Timu ya Taifa U20 Kitakachoingia Kambini Agosti 5, 2024
  2. Kikosi Cha Simba Vs Al Adalah FC Leo (29/07/2024)- Mechi ya Kirafiki
  3. Kikosi Cha Yanga Vs Kaizer Chiefs 28 July 2024 – Toyota Cup
  4. Kikosi cha Simba Vs Telecom Egypt leo 28/07/2024 – Mechi ya Kirafiki
  5. Kikosi cha Yanga Vs TS Galaxy 24 July 2024- Mechi Ya Kirafiki
  6. Kikosi cha Simba Vs El-Qanah Egypt Mechi Ya Kirafiki (22 July 2024)
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo