Nafasi Mpya za Kazi Almashauri ya Wilaya ya Kibiti (Mwisho wa Maombi 28 Julai, 2024)

Nafasi Mpya za Kazi Almashauri ya Wilaya ya Kibiti (Mwisho 28 Julai, 2024)

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, amepokea kibali cha Ajira Mpya kutoka kwa Katibu Mkuu OR – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024. Hivyo anapenda kuwatangazia Watanzania wote wenye sifa kutuma maombi kwa kada nne (04) kama zilivyoanishwa kwa kuzingatia sifa tajwa: –

Nafasi Mpya za Kazi Almashauri ya Wilaya ya Kibiti (Mwisho wa Maombi 28 Julai, 2024)

Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja La II (“Office Management  Secretary II”) Nafasi 03

Sifa Za Mwombaji.

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne (Form IV) au cha Sita (Form VI), wenye stashahada  (Diploma) ya Uhazili au cheti cha (NTA Level 6) ya uhazili. Aidha wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata program za kompyuta za ofisi kama vile; Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

Msaidizi Wa Kumbukumbu Daraja La II (“Records Management  Assistant” II) Nafasi 03.

Sifa Za Mwombaji.

Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha nne (IV) au sita (VI), wenye Stashahada au NTA level

6 katika fani ya Utunzaji Kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali

mwenye ujuzi wa kutumia kompyuta.

Dereva Daraja La II – Nafasi 5

Sifa Za Mwombaji

Kuajiriwa mwenye Cheti cha Kidato cha Nne (IV) na Leseni ya Daraja C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha VETA au NIT AU chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

Mtendaji Wa Kijiji Daraja La III (“Village Executive”) Nafasi 4

Sifa Za Mwombaji.

Kuajiriwa mwenye Cheti cha Kidato cha Nne (IV) na Leseni ya Daraja C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha VETA au NIT AU chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

Masharti Ya Jumla Kwa Waombaji

  1. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45
  2. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya ulevu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  3. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae (CV) yenye Anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya barua pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  4. Provisional/ testimonial/ statement of Result na hati za matokeo za kidato cha Nne na Sita (Form IV and Form Six results slip) HAVITAKUBALIWA.
  5. Waombaji waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
  6. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  7. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingia katika Kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  8. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma, wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/O1/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  9. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kidato cha nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Postgraduate/Deree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, Computer Certificate, Vyeti vya Kitaaluma (Proffesional Certificate from Respective Boards).
  10. Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  11. Uwasilishaji wa taarifa na Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria
  12. Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza. Makao makuu ya Halmashauri, Mtaa wa Lumiozi/Barabara ya Bomani, S. L. P 33 Kibiti/Pwani, Simu: +255023-2010926, Nukushi: +255023-2010927, Baruapepe: [email protected] ,[email protected], Tovuti; www.kibitidc.go.tz

Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 28 Julai, 2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –

  • Mkurugenzi Mtendaji,
  • Halmashauri ya Wilaya,
  • S.L.P 33,

Jinsi ya Kutuma Maombi

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo:- https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Yatangaza Nafasi za Kazi (Mwisho 25/07/2024)
  2. Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Mbogwe (Mwisho Wa Maombi 26 Julai 2024)
  3. Ajira Mpya Shinyanga: Halmashauri ya Manispaa Yatangaza Nafasi mbalimbali – Mwisho wa Kutuma Maombi ni 25 Julai, 2024
  4. Halmashauri ya Mji Handeni Yatangaza Nafasi Mpya za Kazi (Mwisho Julai 27)
  5. Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi: Mwisho wa Maombi Julai 21, 2024
  6. Mwisho wa Kutuma Maombi Ajira Mpya za Afya Zilizotangazwa July 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo