Rayon Sports Yaifunga Gor Mahia 2-1 na Kutwaa Ubingwa wa CECAFA Kagame 2026

Rayon Sports Yaifunga Gor Mahia 2-1 na Kutwaa Ubingwa wa CECAFA Kagame 2026

RAYON Sports ya Rwanda imetwaa ubingwa wa Kombe la CECAFA Kagame 2026 baada ya kuifunga Gor Mahia ya Kenya mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa kwa dakika 120 kwenye Uwanja wa Amahoro nchini Rwanda.

Ushindi huo umeifanya Rayon Sports kutwaa ubingwa wake wa pili wa CECAFA Kagame Cup, ikiwa ni miaka 28 tangu ilipotwaa taji hilo kwa mara ya kwanza mwaka 1998.

Katika fainali hiyo iliyochezwa Ijumaa, Agosti 7, 2026, Rayon Sports ilianza mchezo kwa kasi mbele ya maelfu ya mashabiki waliofurika Uwanja wa Amahoro, huku wenyeji wakitawala umiliki wa mpira na kusaka bao la mapema.

Rayon Sports Yaifunga Gor Mahia 2-1 na Kutwaa Ubingwa wa CECAFA Kagame 2026

Junior Kameni Aifungia Rayon Sports Bao la Kwanza

Presha ya Rayon Sports ilizaa matunda ndani ya dakika 30 za kwanza za mchezo baada ya Junior Kameni kufunga bao la kuongoza kufuatia piga nikupige.

Baada ya kupata bao hilo, Gor Mahia ilijaribu kujibu kupitia mashambulizi ya kushtukiza, lakini safu ya ulinzi ya Rayon Sports ilisimama imara na kuhakikisha timu hiyo inaenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza huku Rayon Sports ikionekana kubadili mbinu na kucheza kwa tahadhari zaidi katika kulinda uongozi wake.

Shariff Musa Aisawazishia Gor Mahia

Gor Mahia iliongeza kasi katika kipindi cha pili na juhudi zake zikazaa matunda katika dakika ya 54.

Shariff Musa aliifungia Gor Mahia bao la kusawazisha na kufanya matokeo kuwa 1-1, hali iliyorejesha matumaini ya timu hiyo kutwaa ubingwa.

Bao hilo lilibadilisha sura ya mchezo, huku Rayon Sports ikianza kushambulia tena baada ya awali kucheza kwa tahadhari zaidi. Timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu katika kutafuta bao la ushindi.

Hata hivyo, dakika 90 za muda wa kawaida zilimalizika kwa sare ya 1-1, hivyo timu hizo kulazimika kucheza dakika 30 za nyongeza ili kumpata bingwa.

Muhoza Daniel Aipa Rayon Sports Ushindi

Katika dakika ya 98 ya muda wa nyongeza, Muhoza Daniel aliibuka shujaa wa Rayon Sports baada ya kufunga bao la pili na kuiweka timu yake mbele kwa mabao 2-1.

Gor Mahia ilifanya kila juhudi kusaka bao la kusawazisha katika dakika zilizobaki, lakini safu ya ulinzi ya Rayon Sports iliendelea kuwa imara hadi filimbi ya mwisho ilipopulizwa.

Matokeo hayo yaliifanya Rayon Sports kushinda fainali kwa mabao 2-1 baada ya dakika 120 na kutwaa ubingwa wa CECAFA Kagame 2026.

Rayon Sports Yarejea Kileleni Baada ya Miaka 28

Ubingwa huo ni wa pili kwa Rayon Sports katika historia ya mashindano ya CECAFA Kagame.

Mara ya kwanza timu hiyo ilitwaa ubingwa huo ilikuwa mwaka 1998, ilipoifunga Mlandege FC ya Zanzibar mabao 2-1 huko Zanzibar.

Baada ya miaka 28, Rayon Sports imefanikiwa kurejea kileleni na kuongeza taji la pili la mashindano hayo katika historia yake.

Kwa upande wa Gor Mahia, timu hiyo imeshindwa kuongeza idadi ya mataji yake matatu ya CECAFA Kagame iliyowahi kutwaa mwaka 1980, 1981 na 1985. Gor Mahia ilitwaa ubingwa huo kwa mara ya mwisho mwaka 1985 jijini Khartoum nchini Sudan.

Zawadi ya Ubingwa wa CECAFA Kagame 2026

Baada ya kutwaa ubingwa, Rayon Sports imeondoka na kitita cha dola 30,000, sawa na Sh79.5 milioni, kama mabingwa wa CECAFA Kagame 2026.

Gor Mahia, ambayo imemaliza katika nafasi ya pili, imejinyakulia dola 20,000, sawa na Sh53 milioni.

Kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Gor Mahia, Rayon Sports imeandika ukurasa mwingine katika historia yake ya CECAFA Kagame Cup na kutwaa taji hilo kwa mara ya pili baada ya kusubiri miaka 28.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Klabu Bingwa Afrika 2026/2027 CAF Hatua ya Awali
  2. Ratiba ya Kombe la Shirikisho 2026/2027 Hatua ya Awali
  3. Picha za Wachezaji wa Simba Wapya 2026/2027
  4. Kikosi cha Geita Gold 2026/2027
  5. Jezi Mpya za Simba 2026/2027
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo