Kikosi cha Yanga vs Namungo Leo 25/05/2026

Kikosi cha Yanga vs Namungo Leo 25/05/2026

Timu ya Wananchi, Yanga SC, leo itashuka dimbani katika kibarua cha kuzisaka pointi tatu muhimu dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC wenye umuhimu mkubwa kwenye mbio za Yanga SC kutetea taji la ligi. Mchezo huo utapigwa saa 12:30 jioni kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.

Yanga wanaingia kwenye mchezo huu wakihitaji ushindi ili kurejea kwenye nafasi ya juu ya msimamo, huku Namungo FC nao wakiwa na presha ya kusaka matokeo yatakayowasaidia kujinasua na hatari ya kushuka daraja. Kwa maana hiyo, dakika 90 za leo zinabeba uzito mkubwa kwa pande zote mbili.

Taarifa Kuhusu Mchezo wa Yanga Sc vs Namungo Fc Leo

MechiYanga SC vs Namungo FC
Tarehe25/05/2026
MudaSaa 12:30 jioni
UwanjaKMC Complex
MashindanoLigi Kuu ya NBC

Kikosi cha Yanga vs Namungo Leo 25/05/2026

Kikosi cha Yanga Leo Dhidi ya Namungo

Kikosi rasmi cha Yanga dhidi ya Namungo kinatarajiwa kuthibitishwa muda mfupi kabla ya mchezo kuanza, lakini taarifa za maandalizi zinaonyesha Wananchi wataingia kwenye mchezo huu wakiwa na hesabu za kupata pointi tatu muhimu.

Kikosi cha Yanga Leo Dhidi ya Namungo

Yanga wanatoka kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Singida BS, matokeo yaliyowarudisha kwenye njia ya ushindi kabla ya mchezo huu wa nyumbani dhidi ya Namungo.

Katika eneo la ushambuliaji, Allan Okello anaendelea kuwa mmoja wa wachezaji wanaotazamwa zaidi kutokana na mchango wake kwenye mabao. Kiungo huyo wa Uganda amefunga mabao tisa na kutoa asisti saba, akiwa amehusika kwenye jumla ya mabao 16.

Hali ya Pacome Zouzoua Kabla ya Mchezo

Moja ya maeneo yanayofuatiliwa kuelekea mchezo huu ni hali ya kiungo Pacome Zouzoua.

Pacome alipata maumivu kwenye mchezo uliopita dhidi ya Singida BS, na kulikuwa na kusubiri vipimo kujua ukubwa wa jeraha lake. Hata hivyo, taarifa zilizopo zinaeleza kuwa majeraha hayo hayakuwa makubwa.

Hali hiyo inaacha nafasi kwa benchi la ufundi kufanya uamuzi wa mwisho kuhusu ushiriki wake kulingana na utayari wake kabla ya mchezo.

Moalin: Yanga Haitaki Kurudia Makosa

Kocha wa muda wa Yanga, Abdihamid Moalin, amesema maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Namungo yamekwenda vizuri, huku akisisitiza kuwa timu yake imejifunza kutokana na matokeo ya nyuma.

“Kila mmoja anajua kilichotokea kwenye mechi yetu dhidi ya Dodoma Jiji, unazungumzia takwimu, haikuwa timu ambayo imewahi kutufunga (Dodoma), lakini ikafanikiwa kufanya hivyo, tumejifunza, tunaiheshimu Namungo ina kocha mzuri na wachezaji wazuri, tunachotaka ni kuendelea kushinda,” amesema Moalin.

Kauli hiyo inaonyesha kuwa Yanga wanauchukulia mchezo huu kwa tahadhari, licha ya rekodi nzuri waliyonayo dhidi ya Namungo.

Namungo Wanaingia na Presha ya Msimamo

Kwa upande wa Namungo, huu ni mchezo wenye uzito mkubwa. Timu hiyo ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 25, na matokeo mabaya yanaweza kuongeza presha zaidi kwenye mapambano ya kujinasua na eneo la hatari.

Namungo pia imekosa ushindi kwenye mechi 13 zilizopita, jambo linaloufanya mchezo dhidi ya Yanga kuwa mtihani mgumu kwao.

Kocha Mgunda amesema maandalizi yao yamekamilika, huku akisisitiza umuhimu wa mchezo kwa pande zote mbili.

“Mechi hii ni muhimu sana kwetu kutokana na nafasi tuliyopo kwenye msimamo lakini hata wapinzani wetu nao ni mechi muhimu kutokana na nafasi waliyonayo, itakuwa mechi yenye ushindani, maandalizi yetu yamekamilika tayari kwa mchezo huo,” amesema Mgunda.

Rekodi ya Yanga vs Namungo

Yanga wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na rekodi nzuri dhidi ya Namungo.

Timu hizi zimekutana mara 12 kwenye michezo iliyopita. Yanga imeshinda michezo saba na kutoka sare tano, huku Namungo ikiwa haijawahi kupata ushindi dhidi ya Wananchi.

Katika michezo hiyo, Yanga imefunga mabao 20, wakati Namungo imefunga mabao saba.

Takwimu Muhimu Kabla ya Mchezo

  • Yanga ina pointi 57 kwenye ligi.
  • Namungo ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 25.
  • Yanga imeshinda mechi 7 kati ya 12 dhidi ya Namungo.
  • Mechi 5 kati ya Yanga na Namungo zimeisha kwa sare.
  • Namungo haijawahi kuifunga Yanga kwenye michezo hiyo 12.
  • Allan Okello amefunga mabao 9 na kutoa asisti 7.
  • Pacome Zouzoua alipata maumivu dhidi ya Singida BS, lakini taarifa zilizopo zinaeleza hayakuwa makubwa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Mechi za Leo 25/05/2026 Ligi Kuu ya NBC
  2. Simba Yarudi Kileleni Ligi Kuu Bara, Barker Aweka Rekodi ya Mechi 20 Bila Kupoteza
  3. Kikosi cha Taifa Stars Kitakachocheza Mechi Mbili za Kirafiki kwenye Kalenda ya FIFA
  4. Msimamo wa Ligi Kuu ya NBC 2025/2026 Leo 24/05/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo