Kikosi cha Azam vs Pamba Jiji Leo 14/05/2026

Kikosi cha Azam vs Pamba Jiji Leo 14/05/2026

Azam itakuwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam leo kuikaribisha Pamba Jiji katika mchezo utakaochezwa saa 12:30 jioni.

Mchezo huo unakuja baada ya Azam kutoka kupoteza kwa mabao 4-1 dhidi ya TRA United, kipigo ambacho kilikuwa cha kwanza kwa timu hiyo kwenye ligi msimu huu.

Azam itaingia kwenye mchezo huu ikihitaji kurejea kwenye njia ya ushindi, huku ikilenga kuendelea kulinda rekodi yake ya kutopoteza nyumbani. Katika uwanja wa nyumbani, Azam imeshinda mechi sita na kutoka sare nne.

Kikosi hicho pia kina kumbukumbu ya mchezo wa kwanza dhidi ya Pamba Jiji, ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2. Sare hiyo inaifanya mechi ya leo kuwa na uzito zaidi kwa Azam, hasa baada ya kutoka kwenye kipigo kizito dhidi ya TRA United.

Kwa upande wa Pamba Jiji, timu hiyo haina rekodi nzuri ikiwa ugenini. Imeshinda mechi mbili pekee za ugenini, huku ikipoteza tano na kutoka sare nne.

Kikosi cha Azam vs Pamba Jiji Leo 14/05/2026

Hiki Apa Kikosi cha Azam Kilichotangazwa Lep

  • 28 MANULA
  • 20 CHILAMBO
  • 12 MSINDO
  • 25 TWAIB
  • 3 YORO
  • 23 HIMID
  • 10 ABAH
  • 21 BIN ZAYD
  • 30 KITAMBALA
  • 6 FEI TOTO
  • 11 NADO

SUBS: FOBA, LUSANJO, ZITOUNE, ZOUZOU, ADOLF, KANOUTE, MZEE, ALOBGAST, ABDALLAH, NGITA

Rekodi ya Mechi za Karibuni

Pamba Jiji imekuwa na mwendo usioridhisha katika michezo yake ya hivi karibuni. Katika mechi nane zilizopita, imeshinda mchezo mmoja pekee, ikitoka sare nne na kupoteza mitatu.

Hali hiyo inaifanya Pamba Jiji kuingia kwenye mchezo huu ikiwa na presha ya kuboresha matokeo, lakini pia ikikabiliwa na changamoto ya kucheza dhidi ya Azam ambayo haijapoteza nyumbani msimu huu.

Umuhimu wa Mchezo kwa Azam

Kwa Azam, mchezo huu ni nafasi ya kujibu baada ya kipigo dhidi ya TRA United. Timu hiyo inahitaji kurejesha hali ya kujiamini na kuendelea kuitumia vizuri rekodi yake ya nyumbani.

Pamba Jiji, licha ya kuwa na rekodi ngumu ugenini, itakumbuka kuwa iliweza kuibana Azam kwenye mchezo wa kwanza uliomalizika kwa sare ya 2-2.

Mchezo wa leo unatarajiwa kutoa majibu kwa Azam baada ya kupoteza kwa mara ya kwanza kwenye ligi msimu huu, huku Pamba Jiji ikiingia ikitafuta matokeo bora zaidi ugenini.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Mashujaa vs Simba Leo 14/05/2026
  2. Kikosi Cha Simba VS Mashujaa Leo 14/05/2026
  3. Ratiba ya Ligi Kuu Ya NBC Leo 14/05/2026
  4. Dodoma Jiji Yaitungua Yanga 3-2 Singida na Kutibua Hesabu za Ubingwa
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo