Msimamo wa EPL Leo 10/05/2026 Ligi Kuu ya Uingereza

Msimamo wa EPL Leo 10/05/2026 Ligi Kuu ya Uingereza

Baada ya michezo ya leo Mei 10, 2026 kumalizika, Arsenal imezidi kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa EPL baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya West Ham United. Matokeo hayo yameifanya Arsenal kufikisha pointi 79 baada ya mechi 36, ikiwa mbele ya Manchester City yenye pointi 74 baada ya mechi 35.

Leandro Trossard alifunga bao pekee la Arsenal dakika nane kabla ya muda wa kawaida kumalizika. West Ham ilidhani imesawazisha kupitia Callum Wilson katika muda wa nyongeza, lakini bao hilo lilikataliwa baada ya ukaguzi wa VAR.

Msimamo wa EPL Leo 10/05/2026 Ligi Kuu ya Uingereza

Msimamo wa EPL Leo 10/05/2026

NafasiTimuPWDLGFGAGDPointi
1Arsenal36247568264279
2Man City35228572324074
3Man Utd361811763481565
4Liverpool361781160481259
5Aston Villa36178115046459
6Bournemouth36131675652455
7Brighton3614111152421053
8Brentford36149135249351
9Chelsea361310135549649
10Everton361310134646049
11Fulham36146164450-648
12Sunderland361212123746-948
13Newcastle36137165052-246
14Crystal Palace351111133844-644
15Forest361110154547-243
16Leeds351013124752-543
17Tottenham35910164554-937
18West Ham3699184262-2036
19Burnley3649233773-3621
20Wolves3639242566-4118

Arsenal inaongoza msimamo ikiwa na pointi 79, huku Manchester City ikibaki nafasi ya pili kwa pointi 74. Manchester United ipo nafasi ya tatu kwa pointi 65, Liverpool nafasi ya nne kwa pointi 59, sawa na Aston Villa iliyo nafasi ya tano.

Bournemouth ipo nafasi ya sita ikiwa na pointi 55, Brighton nafasi ya saba kwa pointi 53, na Brentford nafasi ya nane kwa pointi 51. Chelsea na Everton zimefikisha pointi 49 kila moja, zikishika nafasi ya tisa na ya kumi.

Katika eneo la chini ya msimamo, West Ham ipo nafasi ya 18 ikiwa na pointi 36 baada ya kupoteza dhidi ya Arsenal. Burnley ipo nafasi ya 19 kwa pointi 21, huku Wolves ikiwa mkiani kwa pointi 18.

Matokeo ya Leo EPL Mei 10, 2026

Burnley na Aston Villa zilitoka sare ya 2-2 Turf Moor. Jaidon Anthony aliitanguliza Burnley, kabla ya Ross Barkley na Ollie Watkins kuifungia Aston Villa. Zian Flemming alifunga bao la kusawazisha na kuifanya Burnley kupata pointi moja.

Crystal Palace na Everton pia zilitoka sare ya 2-2 Selhurst Park. James Tarkowski aliipa Everton bao la mapema, Ismaïla Sarr akasawazisha, kisha Beto akarudisha uongozi wa Everton katika kipindi cha pili. Jean-Philippe Mateta aliingia akitokea benchi na kufunga bao la kusawazisha dakika ya 76.

Nottingham Forest ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya Newcastle United. Harvey Barnes aliifungia Newcastle dakika ya 74, lakini Elliot Anderson akasawazisha dakika ya 88 na kuipa Forest pointi muhimu.

West Ham United ilipoteza 1-0 dhidi ya Arsenal. Trossard alifunga bao la ushindi baada ya Martin Ødegaard kutengeneza nafasi ndani ya eneo la hatari.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo wa Ligi Kuu Ya NBC 10 Mei 2026 Baada ya Mechi za Leo
  2. Matokeo ya Simba VS Tanzania Prisons Leo 10/05/2026
  3. Simba VS Tanzania Prisons Leo 10/05/2026 Saa Ngapi?
  4. Washindi wa Tuzo Za BMT 2026
  5. Rekodi Nne za Azam FC Zavunjwa na TRA United Baada ya Kipigo cha 4-1
  6. Mabao ya Allan Okello na Maxi Nzengeli Yaipa Yanga Ushindi Dhidi ya Coastal Union
  7. Ratiba ya Ligi Kuu Ya NBC Leo 10/05/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo