Kikosi cha Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026

Kikosi cha Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga SC, leo Jumamosi wanashuka dimbani kusaka alama tatu muhimu dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa NBC Premier League utakaopigwa Uwanja wa KMC Complex.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 12:15 jioni na utarushwa mubashara kupitia AzamSports1HD. Yanga inaingia kwenye mechi hii ikiwa na lengo la kuendelea kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wake.

Yanga ina pointi 51 baada ya kucheza mechi 21, ikishinda 15 na kutoka sare sita. Timu hiyo imefunga mabao 47 na kuruhusu mabao matano pekee.

Coastal Union, ambayo ipo nafasi ya 12, imecheza mechi 21, ikishinda tano, kutoka sare saba na kufungwa tisa. Imefunga mabao 20, imeruhusu mabao 26 na ina alama 22.

Kikosi cha Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026

Kaimu kocha mkuu wa Yanga, Abdihamid Moalin, amesema timu yake ipo tayari kwa mchezo huo, akieleza kuwa falsafa yake ni kuona timu inatawala mpira na kuendeleza viwango bora vya wachezaji.

“Falsafa yangu ni kuhakikisha timu inatawala mpira na kuumiliki, kuhakikisha tunamentain viwango bora vya wachezaji, hivyo tupo tayari kwa ajili ya mechi hiyo,” alisema Moalin.

Kipa wa Yanga, Abdultwalib Mshery, amesema wachezaji wamejipanga kwa ajili ya mchezo dhidi ya Coastal Union na wako tayari kufuata mbinu za kocha.

“Kila kocha ana mbinu zake ambazo tutatakiwa kuzifuata, lakini Kocha Moalin tulikuwepo naye, amerejea kwa mara nyingine, lakini kuhusu mechi dhidi ya Coastal, tumejipanga kwa ushindi,” alisema Mshery.

Kwa upande wa Coastal Union, kocha Fikiri Elias amesema anatarajia mchezo mgumu na wa ushindani, huku akieleza kuwa timu yake imepata muda wa kuboresha maeneo muhimu kabla ya mechi.

“Natarajia mechi itakuwa ngumu na ya ushindani, tayari tumepata muda wa siku mbili kuboresha na kuimarisha baadhi ya maeneo ili kuhakikisha tunafanya vizuri,” alisema Elias.

Kikosi cha Yanga vs Coastal Union Leo 09/05/2026

Kikosi cha Yanga kitakachoanza katika mchezo wa leo dhidi ya Coastal Union kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 11 jioni, takribani saa moja kabla ya mchezo kuanza. Mchezo huo utapigwa Uwanja wa KMC Complex kuanzia saa 12:15 jioni, huku Yanga ikihitaji ushindi ili kuendelea kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea taji la Ligi Kuu Bara.

Mashabiki wa Yanga wanatarajia kuona kocha Abdihamid Moalin akianzisha nyota watakaoweza kuipa timu nguvu ya kutafuta bao mapema na kudhibiti mchezo tangu dakika za mwanzo. Kwa falsafa aliyoieleza ya kutawala mpira na kuumiliki, matarajio ni kuona Yanga ikiingia uwanjani kwa mfumo wenye kasi, umiliki na presha ya kushambulia.

Katika safu ya mbele, wachezaji tegemezi kama Pacome Zouzoua na Prince Dube wanatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya mipango ya ushambuliaji, hasa kutokana na mchango wao wa mabao msimu huu. Dube ana mabao tisa, huku Pacome akiwa na mabao saba, sawa na Mudathir Yahya.

Kwa upande wa ulinzi, mashabiki pia wanatarajia kuona safu imara itakayoweza kuzuia mashambulizi ya Coastal Union, ambayo ina wachezaji kama Maabad Maulid na Shiza Kichuya, kila mmoja akiwa na mabao manne msimu huu.

Hiki Apa Kikosi Kilichotangazwa

  • DIARRA
  • YAO
  • BOKA
  • MWAMNYETO
  • BACCA
  • ABUYA
  • MAXI
  • SHEIKHAN
  • DUBE
  • OKELLO
  • PACOME

Kwenye Benchi: Masalanga, Abubakar, Kibwana, Assink, Abdulnasir, Damaro, Faridi, SureBoy, Mwanengo & Depu

Umuhimu wa mchezo kwa Yanga

Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa imepishana na Simba kwa pointi tano. Hilo linaifanya mechi dhidi ya Coastal Union kuwa muhimu katika harakati zake za kuendelea kujiwekea mazingira ya kutetea taji la Ligi Kuu Bara msimu huu.

Coastal Union nayo itahitaji matokeo mazuri dhidi ya timu yenye rekodi bora ya ushindi, mabao mengi ya kufunga na idadi ndogo ya mabao ya kuruhusu katika mechi 21 ilizocheza.

Mbali na mchezo wa Yanga dhidi ya Coastal Union, ratiba ya NBC Premier League leo pia ina michezo mingine miwili. Saa 10:00 jioni, Singida Black Stars watakuwa nyumbani dhidi ya Mtibwa Sugar, wakati saa 2:30 usiku JKT Tanzania wataikaribisha Mbeya City Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.

Macho ya mashabiki yataelekezwa KMC Complex kuona kama Yanga itaendeleza mwendo wake katika ligi au Coastal Union itaondoka na matokeo chanya kwenye mchezo huo wa saa 12:15 jioni.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Yanga Yaanza Mchakato wa Kumsaka Mrithi wa Pedro
  2. Vikosi Mechi ya TRA United VS Azam Fc Leo 08/05/2026
  3. Mambo 6 Yaliyosababisha Pedro Kufungashiwa Vilago Yanga
  4. Harry Kane Aifikia Rekodi ya Cristiano Ronaldo Ligi ya Mabingwa Ulaya
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo