Vilabu Bora Afrika 2026/2027 (CAF Club Ranking)

Vilabu Bora Afrika 2026/2027 (CAF Club Ranking)

Viwango vipya vya ubora wa klabu barani Afrika kwa msimu wa 2026/2027 vimetolewa na Shirikisho la Soka Afrika, vikionyesha mabadiliko makubwa katika ushindani wa vilabu. Katika orodha hii ya Vilabu Bora Afrika 2026/2027, klabu ya Mamelodi Sundowns inaongoza, huku klabu za Tanzania zikionyesha mwelekeo tofauti.

Orodha hiyo imetolewa baada ya kukamilika kwa hatua ya nusu fainali za michuano ya CAF, ambapo Mamelodi Sundowns na AS FAR Rabat zimefuzu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Kwa upande wa Kombe la Shirikisho, USM Alger na Zamalek zimefika hatua ya mwisho.

Mamelodi Sundowns inaongoza ikiwa na angalau pointi 68, ikifuatiwa na Al Ahly yenye pointi 66, huku Esperance de Tunis ikishika nafasi ya tatu na pointi 58. Nafasi ya nne inashikiliwa na RS Berkane (57), ikifuatiwa na Zamalek na Pyramids katika nafasi za tano na sita.

Vilabu Bora Afrika 2026/2027 (CAF Club Ranking)

Nafasi za Klabu za Tanzania

Kwa upande wa Tanzania, Simba imeshika nafasi ya 11 ikiwa na pointi 38. Kushuka huku kunatokana na msimu mgumu wa 2025-2026 ambapo ilimaliza mkiani mwa Kundi D la Ligi ya Mabingwa Afrika nyuma ya Stade Malien, Esperance de Tunis na Petro de Luanda.

Young Africans (Yanga) ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 35, ikiendelea kuonyesha uthabiti kwa kuzizidi baadhi ya klabu kubwa Afrika kama Wydad Casablanca, ASEC Mimosas, Orlando Pirates na TP Mazembe.

Klabu ya Azam imepanda hadi nafasi ya 38 ikiwa na pointi tano, sawa na Singida Black Stars. Mafanikio hayo yametokana na kufika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo Azam ilikusanya pointi tisa na kumaliza ya tatu kwenye kundi B nyuma ya Wydad Casablanca na AS Maniema Union.

Orodha ya Vilabu Bora Afrika 2026/2027 (CAF Club Ranking)

RankClub2021–222022–232023–242024–252025–26Total
(× 1)(× 2)(× 3)(× 4)(× 5)
1South Africa Mamelodi Sundowns3445≥5≥68
2Egypt Al Ahly5664366
3Tunisia Espérance de Tunis3453458
4Morocco RS Berkane5045457
5Egypt Zamalek2252≥4≥49
6Egypt Pyramids2216348
7Algeria USM Alger0532≥4≥47
8Morocco ASFAR Rabat0203≥5≥41
9Sudan Al-Hilal2223339
10Algeria CR Belouizdad3322338
11Tanzania Simba2334138
12Tanzania Young Africans0432235
13Morocco Wydad AC6520232
14Angola Petro de Luanda4230227
15Ivory Coast ASEC Mimosas1332024
16Mali Stade Malien0020.5323
17Algeria Mouloudia Algiers0003222
18Egypt Al-Masry2002220
19South Africa Orlando Pirates4004020
20Democratic Republic of the Congo TP Mazembe30.541020
21Morocco Raja CA3302017
22Morocco Olympic Safi0000315
23Nigeria Rivers United0220115
24South Africa Stellenbosch00030.514.5
25Democratic Republic of the Congo Maniema Union0001214
26Algeria CS Constantine0003012
27Angola Sagrada Esperança1012012
28Republic of the Congo AS Otôho1000211
29Algeria JS Kabylie0300111
30Zambia Power Dynamos0000210
31Mali Djoliba000119
32Ghana Dreams FC003009
33Democratic Republic of the Congo Saint-Éloi Lupopo010017
34Egypt Future00.52007
35Libya Abu Salim002006
Mauritania FC Nouadhibou002006
37South Africa Marumo Gallants030006
38Tanzania Azam000015
South Africa Kaizer Chiefs000015
Tanzania Singida Black Stars000015
41Tunisia Étoile du Sahel201005
42Guinea Horoya120005
43Angola Bravos do Maquis000104
Nigeria Enyimba000104
Senegal ASC Jaraaf000104
Angola Lunda Sul000104
Ivory Coast Stade d’Abidjan000104
48Botswana Jwaneng Galaxy101004
49Tunisia US Monastir020004
50Algeria ES Sétif400004

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Yanga Vs Muembe Makumbi Leo 21/04/2026
  2. Kikosi cha Yanga Vs Muembe Makumbi Leo 21/04/2026
  3. Ratiba ya Kombe la Muungano 2026
  4. Mshindi wa Kombe la Muungano Kubeba Kitita Cha Sh150 Milioni
  5. Simba Uso kwa Uso na TRA United, Yanga Wakipangwa na JKT Tanzania Robo Fainali CRDB Federation Cup
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo