Nauli za Treni ya Mwendokasi SGR 2024 | LATRA Yatangaza Nauli za SGR, Safari Kuanza Hivi Karibuni
Watanzania wanaosubiri kwa hamu uzinduzi wa safari za treni ya mwendokasi (Standard Gauge Railway – SGR) sasa wana sababu ya kutabasamu. Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imezindua rasmi nauli zitakazo tumika kwenye safari za treni ya mwendokasi kwa mwaka 2024, huku safari za abiria kutajwa kuanza hivi karibuni. Huu ni wakati wa kihistoria kwa sekta ya usafiri wa reli nchini, kwani SGR inatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika jinsi tunavyosafiri.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na LATRA, nauli za SGR zimewekwa kwa kuzingatia umbali wa safari na umri wa abiria, hivyo kuhakikisha kuwa usafiri huu wa kisasa unakuwa nafuu na haki kwa Watanzania wote. Kuanzia Dar es Salaam hadi Pugu, Morogoro, Dodoma, na hata mikoa ya mbali zaidi kama Makutupora, sasa unaweza kusafiri kwa treni ya kisasa, yenye kasi na urahisi usio na kifani.
Lakini kabla ya kuanza kwa safari hizi za zinazotegemea kua mkombozi mkubwa, LATRA imeweka masharti kadhaa muhimu ili kuhakikisha usalama na ufanisi wa huduma za SGR. Shirika la Reli Tanzania (TRC) linapaswa kutimiza masharti haya, ikiwa ni pamoja na kuwa na leseni ya usafirishaji, kuhakikisha miundombinu na mabehewa yapo salama, na kutumia mfumo wa kisasa wa utoaji tiketi za kielektroniki.
Huu ni mwanzo wa enzi mpya katika usafiri wa reli nchini Tanzania. SGR inakuja na ahadi ya safari za haraka, salama, na za kustarehesha, zikiunganisha miji na mikoa yetu kwa njia ya kisasa na ya kuaminika.
Muundo wa Nauli za Treni ya Mwendokasi SGR 2024
Nauli za SGR zimewekwa kwa kuzingatia umbali wa safari usika na umri wa abiria. Kwa watu wazima na watoto wenye umri zaidi ya miaka 12, nauli imetajwa kuwa ni Tsh. 69.51 kwa kila kilomita. Watoto wenye umri kati ya miaka 4 na 12 watalipa nusu ya bei hiyo, yaani Tsh. 34.76 kwa kilomita. Watoto chini ya miaka minne watasafiri bure, lakini taarifa zao zitahitajika kurekodiwa.
Hizi ndizo Nauli za Treni ya Mwendokasi SGR 2024 Kwa Abiria Wenye umri zaidi ya miaka 12
Mchanganuo wa nauli hizo kwa daraja la kawaida kulingana na umbali wa vituo kuanzia Dar es Salaam hadi Makutupora kwa watu wazima na watoto wenye umri zaidi ya miaka 12 ni kama ifuatavyo;
Safari | Umbali (Km) | Nauli (Shilingi) | |
Kutoka | Kwenda | Daraja la Kawaida | |
Dar es Salaam | Pugu | 19 | 1000 |
Dar es Salaam | Soga | 51 | 4000 |
Dar es Salaam | Ruvu | 73 | 5000 |
Dar es Salaam | Ngerengere | 134.5 | 9000 |
Dar es Salaam | Morogoro | 192 | 13000 |
Dar es Salaam | Mkata | 229 | 16000 |
Dar es Salaam | Kilosa | 265 | 18000 |
Dar es Salaam | Kidete | 312 | 22000 |
Dar es Salaam | Gulwe | 354.7 | 25000 |
Dar es Salaam | Igandu | 387.5 | 27000 |
Dar es Salaam | Dodoma | 444 | 31000 |
Dar es Salaam | Bahi | 501.6 | 35000 |
Dar es Salaam | Makutupora | 531 | 37000 |
Nauli za Treni ya Mwendokasi SGR 2024 Kwa Abiria Wenye umri Kuanzaia Miaka 4 hadi 12
Aidha, mchanganuo wa nauli kwa daraja la kawaida kulingana na umbali wa vituo kuanzia Dar es Salaam hadi Makutupora kwa watoto wenye umri kuanzia miaka minne (4) hadi 12 ni kama ifuatavyo;
Safari | Umbali (Km) | Nauli (Shilingi) | |
Kutoka | Kwenda | Daraja la Kawaida | |
Dar es Salaam | Pugu | 19 | 500 |
Dar es Salaam | Soga | 51 | 2000 |
Dar es Salaam | Ruvu | 73 | 2500 |
Dar es Salaam | Ngerengere | 134.5 | 4500 |
Dar es Salaam | Morogoro | 192 | 6500 |
Dar es Salaam | Mkata | 229 | 8000 |
Dar es Salaam | Kilosa | 265 | 9000 |
Dar es Salaam | Kidete | 312 | 11000 |
Dar es Salaam | Gulwe | 354.7 | 12500 |
Dar es Salaam | Igandu | 387.5 | 13500 |
Dar es Salaam | Dodoma | 444 | 15500 |
Dar es Salaam | Bahi | 501.6 | 17500 |
Dar es Salaam | Makutupora | 531 | 18500 |
Masharti Kabla ya Safari Kuanza
LATRA imetoa masharti kadhaa ambayo yanapaswa kutimizwa kabla ya kuanza kwa safari za SGR. Masharti haya ni pamoja na:
- Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuwa na leseni ya usafirishaji
- Miundombinu ya reli na mabehewa kuwa na ithibati ya usalama
- Matumizi ya mfumo wa utoaji tiketi za kielektroniki
- Kuunganishwa kwa mfumo wa tiketi na mifumo ya LATRA
- Uwepo wa watumishi waliothibitishwa na waliosajiliwa na LATRA
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply